BRIGEDIA Jenerali mstaafu Hashim Mbita ameionya serikali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
BRIGEDIA Jenerali mstaafu Hashim Mbita ameionya serikali kama hakutakuwa na majadiliano baina yake na wananchi uwezekano wa kuvunjika kwa amani ni mkubwa.
Mbita alitoa onyo hilo jana jijini Dar es Salaam katika kongomano la uundwaji wa jukwaa la taifa la Asasi za Kiraia (AZAKI) la kitaifa na la kikanda.

Alisema tatizo kubwa lililopo katika serikali na utawala wa nchi nyingi za ukanda wa Afrika ikiwemo Tanzania ni kutokuwa na majadiliano ya pamoja kati yao na wananchi.
“…Shida kubwa iliyopo ni kukosa majadiliano ya pamoja kati ya watawala na raia, amani na utulivu inaweza kutoweka kwenye ukanda wa nchi za Afrika endapo majadiliano hayo hayatakuwepo,” alisema Jenerali Mbita.
Akitolea mfano kwenye nchi zilizokumbwa na machafuko zikiwemo za Libya na Tunisia, alisema nchi hizo zimefika katika hatua hiyo kutokana na kutokuwa na majadiliano kati ya watawala na raia wake.
Alisema kwa miaka ya hivi karibuni nchi nyingi za Afrika zikiwemo zile za Uarabuni zimekumbwa na matukio ya uvunjifu wa amani, hivyo hali hiyo inaweza pia kutokea katika nchi nyingine za Afrika kama hakutafikiwa kwa hatua hiyo.
“Kukosekana kwa majadiliano kati ya raia na watawala hawa kunaweza kuzaa malumbano na kutoweka kwa amani,” aliongeza. Jenerali Mbita ambaye pia ni Balozi mstaafu na Mdhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alisema lengo la AZAKI ni kufaya kazi kwa pamoja na serikali katika kutekeleza mipango mbalimbali na kuleta maendeleo ya nchi.
 
Mzee usitwange maji kwenye kinu, UVCCM na wengineo watakutukana sasahivi na kuambiwa unazengea Urais 2015. Ulishaambiwa sikio la kufa..................
 
Tatizo sio sikio la kufa CCM sasa hivi wameshakuwa viziwi, labda aje Bwana Yesu awaponye vinginevyo hakuna wakuwasaidia
 
sasa si jeshi lichukue nchi na kuinyoosha halafu iirudishe tena kwa raia baada ya kuiweka saw?
 
Naona labda kashajianda kupokea matusi ya makamba na UVCCM, na jumuiya ya wazazi wa ccm,kwani yawezekana akawa mwanachama wa ccm mfu!
 
Sekretarieti (Secretariaty) nzima au yote ya SISIEM inatakiwa ikapate kikombe kule Semunge kwa Babu.
 
Back
Top Bottom