BRELA jitafakari sana kuhusu kusajili kampuni kwa njia ya mtandao

PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
335
496
Usajili wa kampuni kwa njia ya mtandao imekuwa shida sana, ukijaza taarifa zinazotakiwa ukatuma unajibiwa na kupewa sababu ambazo siyo relevant na nikatika mazingira ambayo huwezi kujibu au kuhoji.

Ukiwapigia simu zao zote hazipokelewi,ila nasikia ukiwatumia vishoka unakamilisha mara moja. Kama ni mwendo wa vishoka basi ondoeni hiyo huduma ya mtandao tujisalimishe kwa vishoka.

Nyie ndio mnakwamisha jitihada za Mhe.Rais kufungua nchi, hapo kwa majirani zetu Rwanda inachukuwa masaa sita tu kufungua kampuni online na hivyo kuhamasisha uwekezaji na wawekezaji wa ndani na nje.
 
Back
Top Bottom