NIDA yaanza usajili wa Vitambulisho kwa njia ya Mtandao

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetambulisha mfumo wa usajili wa watu kwa njia ya mtandao utakaowezesha wananchi wenye sifa za kuomba vitambulisho vya taifa kwa kujaza fomu mtandaoni.

Waombaji wa awali watajaza fomu mahali popote walipo bila kulazimika kwenda ofisi za usajili za wilaya au vituo vya usajili vya Nida kupitia tovuti eonline.nida.go.tz katika mtandao na kufuata malekezo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha NIDA, Geofrey Tengeneza amesema mfumo huo hautawahusu wale ambao tayari wana vitambulisho na wanahitaji kuvihuisha ifikapo Januari 2023 kwani watalazimika kwenda moja kwa moja ofisi za Nida kwa ajili ya kuingiza baadhi ya taarifa mpya na kupiga picha.

“Mfumo huu unalenga kupunguza usumbufu kwa waombaji wa vitambulisho vya taifa ambao kwa sasa wanalazimika kufika ofisi za Nida kuchukua fomu za maombi lakini kupitia mfumo huu mtu atajisajili popote kwa kutumia kifaa chenye uwezo wa kupokea mtandao wa mawasiliano,” amesema Tengeneza.

Amesema baada ya kujaza fomu, mwombaji atatakiwa kuchapa fomu na kuipeleka Serikali ya mtaa anapoishi kwa ajili ya kuthibitisha ukaazi wake kisha atatakiwa kupeleka fomu yake ofisi za Nida iliyopo wilaya anayoishi.

Meneja usajili na utambuzi Nida, Julien Mafuru amesema mfumo huo utapunguza muda unaotumika katika kusajili taarifa za mwombaji kwa kuwa usajili wa taarifa za mwombaji utakuwa umefanywa na mwombaji mwenyewe.

“Pamoja na kurahisisha huduma ya usajili kwa raia na wageni wakaazi, utapunguza pia gharama zinazotumika katika kuchapisha fomu za usajili na gharama za uchakataji wa taarifa,” amesema Julien.

MWANANCHI
 
Nani aliwaambia NIDA kuwa tatizo kubwa la sasa kwa watu ni namna ya kujiandikisha?

Kuna mamilioni ya watanzania walishajiandikisha NIDA kwa miaka kadhaa na bado hawajapata vitambulisho vya NIDA. Hao wapewe vitambulisho vyao kwanza, sio hizo dana dana nyingine.
 
Kapigwa mtu Mil 300 so tutangaze. ..huu mfumo ulikuwepo ila ulikua on/off ambao ulikua unatumika kuthibitisha I'D pia. ..kweli wangetoa vya mwanzo Ingekua poa sn
 
qvm@nin@ zao, watoe kwanza walivyonavyo kwa zaidi ya miaka 5, pumbav kabisa
 
KWA YEYOTE MWENYE SHIDA NA NAKALA YA KITAMBULISHO CHA TAIFA ANICHEKI WHATSP NIMUHUDUMIE 0687872141 ( UWE SERIOUS UNAPOKUJA INBOX HATUPO KWA MAJARIBIO)
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2022-12-20 at 12.36.04 AM.jpeg
    WhatsApp Image 2022-12-20 at 12.36.04 AM.jpeg
    127.7 KB · Views: 17
Back
Top Bottom