Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Na Ramadhan Semtawa
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema hakuna mtumishi wake miongoni mwa wanaotuhumiwa katika upotevu wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), atakayesalimika katika mchakato wa kuwashughulikia utakaokamilika hivi karibuni.
Onyo hilo lilitolewa jana na Gavana wa BoT, Prof Benno Ndulu, kufuatia tuhuma dhidi ya Kamati Maalumu ya Nidhamu kuwa, limewatoa kafara baadhi ya maafisa wa kati wa benki hiyo huku wa ngazi za juu waliohusika na ufisadi wa fedha za EPA wakiachwa na kuonya itawalipua vigogo wa juu wanaoachwa.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma hizo, Prof Ndulu alisema, BoT katika maamuzi yake imekuwa ikizingatia ripoti ya kitaalamu ya Kampuni ya Ernst & Young kuhusiana na suala hilo.
Kampuni hiyo ndiyo iliyobaini ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni za EPA katika hesabu za mwaka 2005/06, ufisadi ambao awali uliibuliwa na Kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini, kabla ya kusitishiwa mkataba ghafla.
Prof Ndulu alifafanua kwamba, ripoti hiyo iliweka bayana kila idara na udhaifu wake pamoja na wahusika, hivyo wanafuata ushauri huo.
Kwa ufafanuzi zaidi, Prof Ndulu alisema baada ya BoT kupitia kwa kina ripoti hiyo, ilifanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa adhabu kwa watuhumiwa.
"Sielewi wanachokisema, tunaongozwa na ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Ernst & Young waliobaini wahusika, huko ndiko tulikoanzia sisi," alisema Prof Ndulu na kuongeza:
"Hata sisi tulifanya uchunguzi wetu wa kina, hatumuonei mtu wala hatutamuogopa mtu yeyote katika kuchukua maamuzi na hatua za kinidhamu. Subirini mchakato ukamilike mtaona, kama kuna atakayeonewa au atakayeachwa, mchakato bado unaendelea."
Wakati Prof Ndulu akisema hayo, taarifa zinasema kuwa, mchakato huo wa kung'oa baadhi ya watumishi bado unaendelea huku wengine wakienda likizo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya watu ambao majina yao yanatajwa na yameonekana zaidi katika nyaraka za malipo ya EPA na ambao wamo katika ripoti ya Ersnt & Young, wako likizo za mwezi mmoja ikiwa ni sehemu ya kupisha uchunguzi.
Hata hivyo, baadhi yao ambao tayari walipewa barua za kuachishwa kazi wamekata rufaa na kwamba bado zinapitiwa na jopo Maalumu la Kamati ya Nidhamu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kuna uwezekano mkubwa wa baadhi yao kupewa barua za kuachishwa kazi muda tu baada ya kurejea au hata kabla ya kurejea, kisha wataruhusiwa kukata rufaa kama walivyofanya baadhi yao.
Mchakato huo wa BoT kung'oa watumishi waliohusika kutia taifa hasara katika EPA, unafanyika kwa makini ili kuondoa uwezekano wa benki kushtakiwa na kuweza kuwalipa watuhumiwa mamilioni ya fedha.
Hata hivyo, kumekuwa na tuhuma ya kuwepo taarifa kwamba, BoT katika mchakato huo wa kuwaadhibu watuhumiwa wa EPA imekuwa ikitoa kafara maafisa wa kati huku wale wa juu zaidi wakiachwa, hali ambayo imefanya baadhi yao kuapa kuwalipua vigogo zaidi.
Wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma wiki mbili zilizopita, Rais Jakaya Kikwete, alisema BoT kwa kutumia mamlaka yake itachukua hatua kwa wahusika na kisha itatoa taarifa kwa umma.