BOT yamwaga mikopo ya mamilioni kwa wafanyakazi wake-Ndio bailout ya serikali hiyo!!

Ni muhimu sana wafanyakazi wote wa serikali wakapatiwa fursa ya kupata mikopo kama hao wafanyakazi wa Benki Kuu. haingii akilini kuwa na sera tofauti kwa wafanyakazi wa serikali.
 
Hivi hizo pesa zinatoka kifungu gani cha bajeti? nafikiri hawa jamaa wamesahau kuwa hizo ni pesa zetu wote, ila katika mgawanyo wa kazi wao tumewapa dhamana ya kuzihifadhi. Kwa nini wasikope kwenye mabenki ya biashara ambayo wanayasimamia kama ilivyo kwa watumishi wengine wa UMMA? vinginevyo basi waajili wote wa serikali na watoe mikopo kwa watumishi isiyo na riba au ya riba nafuu.
Mfano hivi karibuni walimu waruhusiwa kuchukua mikopo NMB lakini wakienda hawezi kupata zaidi ya 3 million! na riba ni kubwa
 
hapa nimejaribu kuangalia ni jinsi gani baadhi ya watu humu wana upeo mdogo kifikra.
hivi ni makampuni mangapi yanakopesha wafanyakazi wake?
na huwakopesha kiasi gani?
hurudisha mkopo kwa muda gani?
je tumelinganisha na nani?, CRDB, NBC, NSSF, PPF, STANBIC, BARCLAYS, STANCHART, AKIBA ZAIN, VODACOM, TIGO LAPF. je haya hayawakopeshi wafanyakazi wake??
hawa wafanyakazi wa BOT hawana right ya kukopeshwa na mwajili wao?
KAMA SEKULA YAO ILIVYOONYESHA KUWA HII NI NYONGEZA AMBAYO WAFANYAKAZI WAMEIOMBA KWA MUDA MREFU. JAMANI MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI.
HIVI WHAT IS 30M KWA UJENZI WA NYUMBA??
AMA HAWA WACHANGIAJI HAWAJAWAHI KUJENGA NA KUONA GHARAMA ZA UJENZI??
HEBU TUUULIZIEN MAKAMPUNI MENGINE HUKOPESHA WAKURUGENZI WAKE KIASI GANI?? HAPO WE CAN ARGUE WITH EVIDENCE.
SIO KWA KUWA KULIKUWA NA SCANDAL YA EPA NA TWIN TOWERS BASI MAANA YAKE WAFANYAKAZI WALIO WENGI WASIPEWE HATA HAKI ZAO ZA MSINGI.

Sawa sote tunaupeo mdogo wa kufikiria wewe mwenye upeo mkubwa kaka hebu tukuulize BOT inatofauti gani na government institution zengine? Je sote tukienda kufanya kazi BOT madaktari watakuwapo, maengineer, watakuwapo? Je unajua mikopo kama hii wanachaji interest ngapi??? Umecompare na benki zengine kujua wanachaji interest kiasi gani??? Sio unasema hatufikirii tu watu wanachopigia kelele ni kwamba mikopo kama hii ni hatari kwa uchumi wa nchi ya tanzania.

Chukulia mfano watu 30 wakipewa mkopo wa milioni 100. Wana mshahara gani wakapata mkopo mkubwa kiasi hicho??? Na kama wana mishahara mikubwa kihivyo ukilinganisha na private sector zinaendana unakuta matokeo yake ni kwamba hawa jamaa wanakuwa na purchasing power kuliko wafanyakazi wengine wa sekta ya binafsi na serikali. Matokeo yake wanaspend kununua magari expensive kama ferrari, aston martin kwasababu purchasing power yao kubwa. Lakini ukijuliza pato la mtanzania ni kiasi gani?? unakuta $1500 Je kuna uwiano hapa!!!!.

Tuje katika sababu za wao kupewa mikopo kama hii unakuta ni kwasababu kwanza watoto wa vigogo wapo katika institution hiyo ambao hutumia influence za baba au mama zao kuongezewa mishahara mikubwa, Pili unakuta hao hao watoto wa wakubwa ndio wanalinda mali na madudu ya baba zao na mama zao serikali. EPA imekuja kugundulika aliyekuwa mkurugenzi wa EPA ni nani mtoto wa Lowassa, akaondolewa kulinda reputation ya mzee!! Kiufupi hatukatai kila organisation lazima iweke incentives kama hizo kwa wafanyakazi wake but kuweko uwiano na uhalisia wa malipo. Kama BOT inatoa milioni 100 Wizara ya Afya pia itoe mikopo hiyo na sekta zenginezo. Na sio BOT kuwapa mikopo mikubwa ili wasivujishe siri za madudu yaliyomo humo ndani.
 
Nanaomba niulize hivi serikali inapesa kweli kukopesha mikopo kama hii kwa mazalisho yepi!!! Our dependence on foreign aid kumeongezeka by 10%, Our economy inategemea zaidi service sectors ambapo ni hatari. Tumezalisha kitu gani????.

UK wanatoaga mikopo ya nafuu ikiwa pana mafaniki mfano budget surplus, economic growth, growth of profit. Tanzania tuna njaa, economic recession, substantial level of corruption, sijui private sector wanaperform vp but tunatoa mikopo kwasababu ipi cost of living???, inflation??? It is a disgrace aisee.
 
Ninadhani mikopo kama hii ni muhimu kwani inapunguza umaskini. Kwa mfano, wafanyakazi wa BoT watakapokuwa wanajenga majumba kwa kutumia pesa waliyokopeshwa, ni dhahiri kuwa ndugu zetu mafundi uashi n.k. watanufaika kwa kupata kazi. Additionally, wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi watapata biashara na kulipa kodi. At the end of the day, huo mkopo unakuwa na impact kuliko kulalia hizo hela hapo BoT. This is why nchi kama Marekani wanahaha kuhakikisha walaji wana pesa ya kutumia. Obama anahangaika kushawishi mabenki yakopeshe for the same reasons. So, sioni ubaya wa utaratibu kama huu wa kukopesha watumishi. Cha msingi ni kuweka utaratibu wa watu wengi zaidi kuweza kukopa. After all wasipokopeshwa watumishi, wajanja watakuja na maarifa tofauti (e.g. EPA) na pesa zitaishia kwenye mabenki ya Jersey, Uswisi e.t.c.

Nakubaliana na wewe, spill-over effect itakuwapo lakini jiulize swali BOT wanazalisha nini!!!! Wenzako marekani na UK civil sectors wanacut expenditure na kuongeza pesa katika sekta ya uzalishaji. Bail out imefocus katika sector za uzalishaji na sio huduma tujiulize BOT wanazalisha kitu gani???? Kiufupi spill-over effect inatatika iwepo kwa kuinject pesa katika mabenki na mabenki kutoa mikopo ya gharama nafuu kwa wananchi. Spill-over effect inatakikana kuwapo kwa mashirika kwa kuwezeshwa na misaada toka serikalini, wafanyakazi wa serikalini hawaitaji mikopo kama hii ikiwa sekta zengine muhimu haziwazeshwa.

Kilimo kwanza naweza kuona ndio muhimu zaidi kuliko kutoka mikopo ya ajabu kwa wafanyakazi wa sekta ambayo haizalishi kitu. To me it does not make sense
 
tatizo ni nini hapa ? au kwa vile ni BOT...? its all about staff wellfare,..ni moja ya faida kufanya kazi kwenye taasisi kama hiyo...wewe ulie leta hii mada ni kwa vile upo nje ya taasisi ungekua ndani i gues ungekua wa kwanza kuja fomu za maombi ya mikopo hiyo...
 
Ni vizuri wakakopeshwa kwa kuwa wako benki kuu na wanaziona zinavyoingia/nakutoka, ukiwa unafanya kazi sehemu nzuri hiyo ndo motisha na bado ni mkopo..

Ulizia TRA wanakopa ngapi??? kama si zaidi ya hizi kwa taarifa!!! wenyewe wanaenda benki yeyote wanajikadilia wenyewe.

Wafanyakazi wa Taasisi/Serikalini kote huko waajili wao wamejiwekea mikataba kwenye mabenki na sitegemei kama kuna mfanyakazi wa serikali ambaye hadaiwi na benki.

Sasa hivi nimeona PPF inashirikiana na SACCOS za mashirika ya umma/Serikalini inawagawia mikopo, kukopa hadi miaka mitano hivi leo tunavyoongea.

Mitaani watu wamejiimalisha kwenye SACCOS kibao za makanisa na vijiji kwenda mbele wanakopa.

BOT wapeni wafanyakazi wenu MIKOPO kwani mkopo ni mkopo utarudishwa hata mtu afe hii siyo EPA.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, hawa wafanyakazi wanastahili kupata mikopo waliyopewa, mwajiri wao amewaboreshia wafanyakazi ili wapate nyumba nzuri na kuinua morali ya kazi, hata institutions/ organisations nyingine nyingi tu zinatoa mikopo kwa wafanyakazi wake to mention few EWURA, NSSF, PPF etc. Na nyie mlio sehema ambazo hakuna mikopo tumieni hii kama changamoto kwa waajiri wenu ili wabuni mbinu za kuwawezesha kupata mikopo
 
tatizo ni nini hapa ? au kwa vile ni BOT...? its all about staff wellfare,..ni moja ya faida kufanya kazi kwenye taasisi kama hiyo...wewe ulie leta hii mada ni kwa vile upo nje ya taasisi ungekua ndani i gues ungekua wa kwanza kuja fomu za maombi ya mikopo hiyo...

Sidhani ni mada hapa na wala sina wivu na wafanyakazi BOT suala ni je mikopo kama hii inamotisha kwa wananchi??? Mfano tukienda kujazana wote BOT tutafika???? Usiangalie upande moja tu. Kuna walimu kila siku wanapelekeshana mbio na Wizara ya Elimu walipwe malimbikizano yao ya mshahara hawa wanazalisha maengineer, makarani niambie BOT wanazalisha kitu gani!!!!
 
Benki Kuu ya nchi inaanza kutoa mikopo ya ujenzi? mweh!!

Nakubaliana na wewe hii Historia ya kwanza Benki Kuu duniani kukopesha wafanyakazi wake kwa ujenzi. BOT wanaweka historia za ajabu saa zengine. Mfano EPA inakadiriwa kuwa the biggest Central Bank Scandal in the World. Sasa hivi wanatoa kali BOT inakopesha wafanyakazi wake mikopo ya ujenzi hivi wameshasahau sijui role za BOT Tanzania na kugeuka kuwa Commercial Bank???
 
Tatizo siyo mikopo, ila nadhani ni nani anastahili. Wanajuaje kwamba mfanyakazi X hana nyumba kwa hiyo akopeshwe pesa ya kujenga nyumba ili kumsaidi huyo mfanaya kazi??? Kumbuka hata nyumba za serikali walizoamua kuuza walisema wanawasaidia wafanyakazi ili wasikose mahali pa kuishi baada ya kustaafu...Ukweli ni kuwa wengi wao walisha kuwa na majumba mengi tu. Na mpka leo, wengi walipozinunua zile nyumba walizibomoa na kujenga ma kasri yao ambayo wanapangisha kwa serikali na taasisi zake.

Hii ndiy hofu yangu, ingawa pia sioni kama itakuwa rahisi kujua kuwa mtu X ndiye anayehitaji nyumba kwani hana kabisa.

Yaani, mtindo huu unaendeleza yale yale ya mwenye nacho huongezewa, na asiye nacho huponywa hata kile kidogo alichonacho.
 
Huu ni uonevu kwa watumishi wengine wa taasisi za serikali. Kuwe na justice!!! Lo!!! Taasisi ya EPA na skendo lukuki. Wanajineemesha wao. Lo!
 
ila watanzania tuna kasumba mbaya sana ya mikopo...
1.hatufanyi kwa jinsi inavyotakiwa....uliichoomba hukifanyii haki...(umekopa ajili kujenga utaenda fungua bar)

2.tunaamini mikopo ni sadaka....unaanz akukimbia kimbia kulipa...usumbufuu kama sio wewe uliekuwa unalilia lia kuomba upewe...unatamba bar zote kuwa una pesa.....

3..................nyumba ndogo zaongezeka....

4.magari mapya na bei kubwa yanaongezeka kama lipo moja yanakuwa ma 3 mke baba na watoto......na ingine ya nyumba ndogo....
 
..tatizo hakuna taasisi za kukopesha wananchi mikopo ya kujenga nyumba.

..tuliwahi kuwa na Tanzania Housing Bank[THB] ambayo meneja wake mkuu wa kwanza alikuwa Daniel Yona.

..Tanzania Housing Bank ilikuja kutufia chini ya Mzee Mwinyi,JK,Dr.Rashid,na Kibonde.

..binafsi natoa tahadhari kwa BOT kwamba wawe makini ktk kuhakikisha mikopo hiyo inatumika kwa manunuzi/ujenzi wa nyumba ni siyo shughuli nyingine.

..labda BOT wangeingia mkataba na shirika la umma kama NSSF, NHC, ili watumishi wao wakopeshwe nyumba na mashirika hayo.

..kwa wengine nadhani tuache kulalamika hapa. hizo milioni 30 mpaka 100 zitaingia kwenye circulation na kwa wale walioko kwenye biashara inayohusiana na ujenzi tunaweza kufaidika nazo pia.

..sasa kwasababu BOT wamepewa mikopo hiyo, taasisi nyingine za umma nazo zishinikize serikali kuweka utaratibu na mazingira kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata mikopo ya nyumba. tuachane na roho za kikorosho kwamba "wote tukose", badala yake tuwe na roho za "wote tupate."
 
Tatizo letu wengi bado tuna hangover ya siasa za ujamaa na kujitegemea. Eti binadamu wote ni sawa! Kivipi?

Jamani, ingawa ukweli ni kwamba inauma..kwamba Tanzania umaskini umekithiri lakini hebu tuangalie upande mwingine wa shillingi. Hawa jamaa hawapewi hizo hela bure. Wanakopeshwa. Na watarudisha. Hivi inatofauti gani na mtu anayenunua nyumba kwa mortgage huko ulaya au kwingineko na akatakiwa kulipa kwa kipindi cha miaka 30?

People, lets face it. Umasikini TANZANIA hautaisha kwa Gavana Ndullu kuwanyima mikopo wafanyakazi wake. Rather umasikini utaisha kwa wale wanaokabidhiwa dhamana ya kuongoza haya mashirika kwa kuchapa kazi kwa ufanisi kusudi waweze kutoa incentive kwa wafanyakazi wao. Alichokifanya Ndullu ni halali kabisa. Sema tunaona ni abnormal kwa sababu ya umasikini wetu..... wote macho yetu yako BOT. Infact kama mashirika yote yangekuwa yanaendeshwa kwa ufanisi...hii ingekuwa ni namna ya kumotivate watu wachape kazi...

Msisahau kwamba jamani..human being is inherently selfish. Mtu huwezi kumwambia amalize PhD yake Harvard au kwingineko..then aje umpe mshahara wa nyanya! Na mikopo ya namna hii ni mojawapo ya kutoa incetives za kuwa attract wataalamu makini. Hivi Ndullu na PhD yake ya Northwestern..mnadhani angekosa kazi makini huko World Bank au kwingineko? Lets face it. Ndo ukweli unaouma huo.

I may be wrong, lakini nadhani this is a good strategy, as long as watu wanafanya kazi. Harafu tusitake kumsingizia Ndullu..anayeharibu ni JK na serikali yake kwa kushindwa kupambana na ufisadi..there enough for all of us..but when you allow the few to rip off the whole country..even hard working men and women...wanakuwa victims.... Let every hard working man and woman be rewarded. Huwezi sema kwamba kwa vile we are the poorest nation on earth basi mimi Masanja na PhD yangu (mfano) nisipate kitu kusudi tulingane. Hizo ni zama za ujima!

Kama alivyosema Waberoya, its only hard work which can liberate a person from the equation of poverty. Hata hawa wananchi lazima wafike kipindi..wajue kwamba na wao wana obligation kama raia..siyo kutetewa tuu. Mfano wanapohitajika kupiga kura..let them elect serious and responsible leaders. Leo unapewa tshirt unampigia kura fulani..kesho jamaa akijineemesha na wewe unakufa kwa njaa..utamlaumu nani? Otherwise..poverty is here to stay..whether Ndullu gives out Largesse za BoT kwa wafanyakazi wake or not.

Tuache kusingizia ufisadi kila kitu..I say Ndullu amefanya jambo jema. Cha muhimu kuwe na transprency na accountability.

Masanja,
 
Hakuna mtu anaye pinga kiongozi wa sehemu ya kazi kuwapa motisha au maslahi bora wafanya kazi wake.
Tunachopinga ni kuwa Bank kuu ni taasisi ya serikali ambayo mimi na wewe tunahisa pale.
Pili ndio chombo chenye kuratibu vyombo vya fedha ikiwemo mikopo iwe ya biashara au ya kujenga nyumba.
Tatu kuna upungufu/mapungufu kwenye eneo hilo la mikopo hasa hasa ya kujenga nyumba, kwa wafanyakazi na wakulima na wafanya biashara kwa asilimia kubwa.
Sasa ikiwa BOT ndio msimamizi wa hayo mabenki na kuna tatizo hilo katika nchi hii, basi wao wangekuwa wa kwanza kutengeneza sera ambayo itafanikisha jambo hili kwa watanzania walio wengi.
na kama tunasema kuhusu kustimulate the economy na mambo mengine, suala la mikopo ya nyumba ni la muhimu, maaa kutokana na nyumba bora, afya za watu zitakuwa bora, utendaji mzuri wa kazi utakuwepo, wizi utapungua, shinikizo za damu nk zitapungua, watoto wetu watapata nafasi nzuri zaidi ya kujisomea jioni, wateja na waumeme wataongezeka, maana kwenye nyumba ya matope au nyasi ningumu /haiwezekani kuweka umeme hivyo kurahisha utumiaji wa majiko ya gesi na umeme kutapunguza ukataji wa miti nk nk.
nne kwa sababu hiyo sio biashara ya Bank kuu kutoa mikopo, kwa staff basi utaona watakuwa na limitation ya mtaji wa fungu la mikopo/au ukasababisha washindwe kutimiza majukumu ya kuanzishwa kwa BOT
Tano kuna kiongozi moja aliwahi kupoteza kazi BIMA kwa kutoa mikopo kwa Staff ambao baadae walitumia kinyume cha walivyo tarajiwa kwa sababu shirika hilo au mkurugenzi huyo alishindwa kufuatilia matumizi yake, maana anamajukumu ya uongozi na kuendesha biashara ya bima.
Lakini leo hii kama ukienda Azania Bank kwa sababu wao ndio oja ya biashara zao wana njia za kukufuatilia na ku-minimise risk.
Sasa sijui Human resource/Finance Dept ya BOT baadae wanafualia na kuhifadhi hizo hati za viwanja za wakopaji? na ku-kokorotoa interest rate kila mwenzi kama sio free.
 
Back
Top Bottom