BoT mulikeni huu wizi kwenye benki unaitwa "Processing fee"

Naunga mkono hoja. Mkopo una riba ndogo sana. Maranyingi watu hawaangalii muda wa mkopo. Miaka9 kwa hiyo riba ni rafiki sana.
Watu hawaangalii time value of money (TVM), mtu binafsi unaweza fanya huo ujinga kumkopesha mtu 15M akulipe 26M miaka 9 ijayo?

Benki hapo wamesaidia sana. Hiyo gharama nyingine tunayoona wala benki hawaichukui yote. Wanalipa kodi serikalini, wanalipia mifumo ya kibenki na usalama, wanalipia bima, gharama za uendeshaji, corporate social responsibility, etc.

Mkopo sawa na bure huo
 
Acha kukopa..unajipeleka mwenyewe afu unakuja hapa kulia Lia..mtu yeyote ukiwa na nidham na fedha zako hutokopa daima hata kama Kuna project unataka kuanzisha utaanza nayo taratibu Kwa pesa uliyonayo...

Kuchukua mkopo ni tamaaa zilizomo ndani ya binadamu maskin wa fikra..na mtakoma Kwa hzo tamaa zenu...lipa mkopo
 
nilitaka kutopup mkopo nichukue 1.7 baada ya deni la awali kukatwa miezi 8,nikiwa sielewi nikauliza hivi zile gharama za mkopo zitakuwepo akanambia ndio yaani ile 1.5.

kwamba nitareset deni halafu nichukuel laki 2,nikatoka bank huku nacheka sana.
Hapana bhana,
Bank Gani hiyo?
Kwa benk nyingi makato ya bima na processing fee ya mkopo vinakatwa percentage wise..
 
Benki za Tanzania nyingi ni wezi wanaoptata faida kwa makato badala ya biashara .Ukingalia account kenye ATM makato,Ukiweka laki lazima wabaki na elfu ishirini,themanini ndiyo ya kwako,ukiprint receipt makato.Wanafahmu Watanzania hatupo serious kwenye issues kama hizi,acha tupigwe mpaka tutakapojitambua.
Hili ni tatizo.Halafu wanapofunga mahesabu huwa wanasoma faida waliyopata kwa sauti kuuubwaaa.Kumbe ni fedha za wizi kimaandishi.
 
Hapana bhana,
Bank Gani hiyo?
Kwa benk nyingi makato ya bima na processing fee ya mkopo vinakatwa percentage wise..
mzee usibishe babu.

hao ni NMB na kama inapungua kidogo hapo nilipotaja basi ni laki au laki na nusu.
kuna bima hapo na ada,zote hizo ndio gharama zake hizo.

kama ni 17%-16% ya mkopo unadhani unadhani itakuwa shilingi ngapi kwa 15ml??
 
Huo mkopo una riba ndogo sana kama unakopa 15M, unapata 13.5 alafu utarudisha 26M kwa miezi 108.
Yaani kwa miaka 9 yote unafanya mrejesho wa mara mbili ya thamani ya sasa ya hela. Ningepata mkopo kama huu ningeukumbatia kwa nguvu zote.

Miaka 9 ijayo thamani ya TZS itakuwa imeshuka sababu ya inflation, si ajabu milioni 13.5 ya leo itakuwa sawa na milioni 20 ya 2033. Yani unipe hela leo alafu useme ndani ya miaka 9 niirudishe mara mbili yake tu, mbona kicheko kwangu.
Watanzania tunatumia mikopo vibaya. Unakopaje mkopo wa kulipa miaka 5 - 9. Hapo lazima bank wakufurahie.

Kopa mkopo wa miezi 12 - 24
 
Kama tujuavyo kwa sasa mfanyakazi anaweza kukopa online moja kwa moja kupitia ESS bila kwenda bank.

Lakini cha ajabu bado Riba ni kubwa na kuna Bima ya mkopo kubwa. Tukiachana na hayo ya bima na riba bado benki wanakata "Processing Fee" (gharama za mkopo, au ada ya mkopo).

Najiuliza mfanyakazi anaomba mwenyewe kwa mb zake, bado anakatwa riba ya mkopo asilimia 16-17, sasa hii gharama ya mkopo ni nini? Ni ya nini kama sio wizi? Yaani huo mkopo unagharamiwa nini?

Mfano, ukikopa ml. 15 NMB kwa miezi 108 utalipa ml 26+, utakatwa bima 1.2 m, gharama za mkopo 300k.

So katika mil 15 utakatwa 1.5, utapata 13.5 then uje kulipa milioni 26.
Ukitaka riba ipungue shusha miaka ya kufanya marejesho iwe angalau miaka mitatu. Ila ni lazima uwe na vyanzo vingine vya mapato vinginevyo mambo yatakuwa magumu sana. Mkopo uko fair huo
 
Naomba unieleweshe kuhusu hiyo PBZ Kwa Mimi niliyeko Huku mpanda na hakuna wakala nakopaje?
Njoo Dodoma au nenda Dar ndio wana matawi yao. Njoo ukiwa na viambatanisho vyote.

Cha kwanza ona kama nao wameshaanza kukopesha kupitia Watumishi Portal. kama bado, ndio uje. CRDB na NMB wao teyari wameshajiunga na huu mfumo wa online wa serikali. PBZ walikuwa bado ila inawezekana na wao teyari hivyo hutahitajika kusafiri.
 
Back
Top Bottom