BoT ituletee sarafu ya Tsh 600

Mr. Marangu

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,565
1,516
Benki kuu ya Tanzania inafaa sasa wafikirie kutuletea sarafu ya Tsh 600 kutokana na wimbi la vitu vilivyokua vikiuzwa Tsh 500 sasa vinauzwa 600, hali hii imepelekea kuwapo kwa usumbufu wa upatikanaji wa chenchi, hali inayopelekea mnunuzi wa huduma kufikia kisamehe ama kudai kiasi cha chenchi

Ikiwapendeza pia sasa wafute sarafu ya Tsh 50.

Nawasilisha mapendekezo yangu.
 
Kwa hii mikopo ya Trillion 91. Lazima pesa ishuke thamani tu. Kenya noti kubwa ni ksh 1,000. Tz ni Tshs 10,000 nayo ni haina hiyo value practically
 
Kwahiyo 100 hazikusaidii?
Sijataja 100 mkuu, ukifanya tathmini vizuri hamsini inanunua pipi moja kwanini wasiondoe ili mtu akitaka kununua pipi atoe tsh 100 apewe mbili
50 kwenye matumizi ya cash zinasumbua nadhani hizo zibaki kwenye malipo ya kadi za kuchanja since huko unaeza lipa hata tsh93 na hakuna usumbufu wa cheji
 
Nafikiri vinginevyo Serikali itengeneze mazingira ya kusisitiza malipo ya mtandaoni tutoke kwenye cash hizi fedha ndogo zimegeuka kua kero sana kulingana na mfumuko wa bei
Ukitaka jaribu kutoa tsh 10,000 ununuevocha uone moto
 
Nafikiri nikwavile wao hawatumii sana cash
Kutumia digital money ina stimulate mtoa huduma kufanya discount
Assume umeenda kwa Mangi akakuambia soda 597 badala ya 600
So digital money nadhani nisuluhisho sijui serikali inapata kigugumizi gani kuelekea huko
Tozo zinazokatwa kwenye mfumo huo wa
Digit ni dalili tosha ya kuonesha serikali haitaki tuelekee huko
 
Jifunzeni kuacha 'tip' kwenye huduma, kudai mia mia ni dalili ya ufukara sana.
Sawa dalili ya ufukara haya ungekuwa ww unauza soda jumla unauziwa 500 kwa soda moja kaja mtu na elf 1000 utamrudishia mia 500 hutadai 100 sio hali yakuwa umezipoza kweny frij hapo
 
Sawa dalili ya ufukara haya ungekuwa ww unauza soda jumla unauziwa 500 kwa soda moja kaja mtu na elf 1000 utamrudishia mia 500 hutadai 100 sio hali yakuwa umezipoza kweny frij hapo
Sehemu ngapi soda hiyo hiyo inauzwa 1000 au 2000 na watu wananunua?

Mia ni kubwa kwa muuzaji na sio kwa mteja.
 
hii itatusaidia sana wazee wa Pepsi, Coca-Cola imepanda tena bei saiz ni 700, walete na sarafu za 700
 
Back
Top Bottom