Bonyokwa Wakumbukwa: DAWASA wanajenga kituo cha kusukuma maji (Booster pump), ujenzi wafikia 30%

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
DAWASA yaanza mwaka na wakazi wa Bonyokwa

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na uboreshaji wa huduma maji za maji katika eneo la Bonyokwa ambapo ujenzi wa kituo cha kusukuma maji (Booster pump) unaendelea kwa kasi na hadi sasa mradi umefikia asilimia 30 ya utekelezaji wake.

Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Ndugu Everlasting Lyaro amesema utekelezaji wa kazi hiyo unaridhisha na kuwataka wananchi wa Bonyokwa na maeneo jirani kuwa wavumilivu wakati mradi huu ukiendelea.

"Kazi hii inalenga kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wanaopata maji kwa msukumo mdogo ambao wanaathiriwa na jiografia ya maeneo yao ambayo mengi ni miinuko kama vile eneo la Kisiwani na maeneo jirani." amesema.

Ndugu Lyaro amesema kazi hii ni muendelezo wa jitihada zinazoendelea kufanywa na DAWASA za kufikisha huduma ya majisafi katika maeneo korofi ndani ya jiji ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuongeza msukumo wa maji.

"Tutoe rai kwa wananchi wanaohudumiwa na DAWASA kwamba kukamilika kwa kazi hii ya Bonyokwa kutaenda kuboresha huduma ya maji kwa kaya 1200 na na ambazo ni takribani wakazi 5000 na kazi hii inategemewa kukamilika mwezi Februari mwaka huu" amesema.

Kwa upande wake Ndugu Mlale Khalfan, mkazi wa Mavurunza amesema huduma ya maji inafika kwa kiwango kidogo kutokana na ongezeko kubwa la watu pamoja na jiografia katika eneo hili, na kuishukuru DAWASA kwa kutekeleza mradi huo

"Tunafarijika kuona kazi inaendelea kwa sababu upatikanaji wa maji haukuwa wa kuridhisha, tunaomba DAWASA iongeze kasi katika utekelezaji ili tupate huduma iliyo bora." amesema.

Ujenzi wa kituo cha kusukuma maji (Booster pump) katika eneo la Mavurunza unajumuisha uwekaji wa pampu yenye uwezo wa kusukuma lita 144,000 kwa saa utakaoboresha huduma ya maji katika maeneo ya Bonyokwa kwa Kichwa, Bonyokwa stendi, Kwa Dani Mrwanda, Shedafa, Macedonia, mnara wa voda, Chuo cha Masanja, Bonyokwa Kisiwani, JKT B, Msikiti wa Kijani, Mwisho wa Rami, Viwanja vya JKT na baadhi ya maeneo katika kata ya Kisukulu.
IMG-20240115-WA0018.jpg
IMG-20240115-WA0019.jpg

Pia Soma:
- RC Chalamila: Rais Samia kaelekeza Bonyokwa iongezewe fedha ili maji yatoke Saa 24

- DOKEZO - Tabata Bonyokwa hatujaona tone la maji wiki ya tano sasa, DAWASA mnatuona manyani?
 
Back
Top Bottom