Bondia Changarawe afanya kweli usiku huu italy, amtwanga mvenezuela kwa KO

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,220
BREAKING: BONDIA CHANGARAWE
AFANYA KWELI USIKU HUU ITALY, AMTWANGA MVENEZUELA KWA KO!

Na Nsangu Kagutta, Italy

Yusufu Luccasi Changarawe usiku huu ameing'arisha Tanzania baada ya kushinda pambano lake la kwanza la kutafuta kufuzu kushiriki kwenye mashindano ya
Olympic jijini Paris, Ufaransa, yatakayofanyika baadaye mwaka huu.

Changarawe ambaye anapigana katika uzito wa Light Heavy wa Kilo 80, ameshinda kwa knock out ya raundi ya kwanza kwa kumcharaza kwa ngumi nzito bondia wa Venezuela, Perreira Diego.

Bondia wa huyo Venezuela aliingia kwa mkwara na kujaribu kumchanganya
Changarawe ambaye alionyesha utulivu wa
hali juu kudhihirisha uzoefu na mbinu
alizonazo za mchezo wa ngumi.

"Jamaa ni mzuri sana na ilikuwa vigumu kumsoma maana sikuwahi kumuona hata kwenye mitandao" alisema Yusufu Wakati akiongea na Wabongo Ughaibuni Media.

Changarawe, anayetakiwa kushinda mapambano manne ili kufuzu, anaingia tena ulingoni kesho Alhamisi kupambana na bondia wa Norway.

Mshindi huyo wa medali ya Shaba wa Michezo ya Jumuiya ya Madola, ameongozana na mwalimu Mohamed Abubakari Mohamed na Makamu wa Rais wa kamati ya Olympic Tanzania, Henry
Tandau.
1709703440745.jpg

1709703444356.jpg
 
View attachment 2925746
View attachment 2925747
Pongezi ziende Kwa mama anaupiga mwingi
 
Si kweli. Huyo mama anaupiga mwingi ulingoni alipanda yeye?
Hajamaanisha, hiyo ni DHIHAKA sababu siku hizi imekuwa kila kitu pongezi kwa mama, hata mvua ikinyesha pongezi kwa mama, yule mtoto wa lowasa akamshukuru mama bila ya mama, baba yake asingeongezewa muda wa kuishi. 😂
 
Back
Top Bottom