Bomu la askofu Gwajima laisambaratisha CCM

Fandre

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
320
225
By Fandre

Baada ya Askofu Gwajima wa Ufufuo na Uzima kumlipua Dr Slaa na kuwasambaratisha kabisa wale waliokua wamemnunua ili kumdhoofisha Mh. Lowassa sasa hali Si shwari ndani ya kambi ya Chama cha Mapinduzi baada ya Silaha yao ya mwisho kuwaunguza wao wenyewe.

Askofu Gwajima alikemea wazi tabia ya Vyombo vya Usalama wa Taifa hili kupendelea upande mmoja huku wakisahau ya kuwa vyombo hivyo vipo kwa ajili ya Watanzania wote na sio CCM pekee kama vile ambavyo vyombo hivi vimekua vikitumika kuimarisha Utawala wa Chama cha Mapinduzi Kwa muda mrefu sasa.

Hongera sana Askofu Gwajima Kwa kusema UKWELI Kwa UJASIRI MKUBWA. Nchi hii haitakuja kuendelea kama watu wake hasa wale waliopewa dhamana kubwa ya kuzungumza Kwa niaba ya wananchi wengi wanyonge hawataamua kuusema ukweli.

Kwa Miaka mingi sasa CCM imekua ikivitumia vyombo hivi na taasisi mbalimbali za Nchi Katika kukandamiza upinzani nchini huku wakikosekana Watu Sahihi na wenye Dhamiri ya kweli ya kukemea jambo hili Kwa UJASIRI.

Sisi wananchi tunaohitaji Mabadiliko nje ya Mfumo uliochoka na kushindwa wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Kwa niaba ya Watanzania wote na familia zao waliopoteza uhai wao na viungo vya miili yao kwa sababu ya Ukombozi wa Pili wa Taifa hili, tunasema AKHSANTE SANA na uendelee mbele katika kuwatetea Watanzania.

Tunafahamu viongozi wengi wa dini tunaowaheshimu Kuwa wanaweza kukemea uovu wa serikali na uonevu wa vyombo vya usalama wamenunuliwa na serikali ya CCM ili kutetea maslahi ya chama hicho Lakini uwepo wa viongozi wachache wa aina ya Askofu Gwajima unatupa moyo kuwa bado wapo viongozi wasafi na wenye uwezo mkubwa kutetea haki zetu.

Tumefurahi sana Kujua Kuwa wewe ndiye uliyesaidia junkets Mh. Edward Lowassa katika kambi ya UKAWA Kwani Marple yake yanaonekana Kuwa ni makubwa ndio mana Serikali ya CCM itakuandama Sana Kwani tayari imeshapoteza mwelekeo.

Askofu Gwajima wewe ni KINGS' MAKER na Taifa pamoja na ulimwengu kwa ujumla umeshuhudia hili.

Leo CCM imerudi nyuma Sana Kwa sababu tu ya BOMU ulilomlipua Dr Slaa, na kila kona wana CCM wanapiga kelele kuashiria kuwa Kumbe wao ndio walimtuma Dr Slaa.

Mwaka huu Mabadiliko haya tuliyoyatafuta na kuyalilia kwa muda mrefu Lazima yapatikane.

Miaka 54 ya CCM inatosha. Kama wameshindwa Miaka yote hiyo kubadili Mfumo wa Chama chao ili kuwasaidia Watanzania basi hata sasa HAWATAWEZA Kwa muda WA Miaka Mitano Kwani Kila mtu wao amemezwa na Mfumo huo.

Ni zamu ya UKAWA sasa, ni zamu ya Lowassa.

LOWASSA ANAFAA NA ANATOSHA KWA URAIS.

#Chagua Lowassa
#Chagua UKAWA
#Mwaka wa Kuunda Tanzania Mpya
 
Fandre

Kwa mtizamo wangu, sizani kama ni jambo la maana kuendeleakuwatumia viongozi wetu wa dini kwenye mambo ya Siasa, Kufanya hivi ni kujaribu kuweka jambo lasiasa kweny mambo ya dini.

Kumbuka Siasa ni jambo la mda tu tena ni jambola mpito lakini imani zetu za dini hudumu kizazi hadi kizazi.
Kufanya hivyo kunaweza kuleta utofauti kati yaGwajima na wafuasi wake hasa wale wanachama wa chama cha mapinduzi na wafuasiwa magufuli kwa kipindi hiki. Vingozi wetu wa dini tunaomba wajikite kwenyemalengo yao hapa duniani.

Tufanye siasa za siasa na tuachane na siasa zadini. Mungu ibariki Tanzania. Mungu tupe kiongozi bora hapo october 2015!Tudumushe udugu wetu.
 
Kama askofu unaona ccm wanavuruga amani na unanyamaza kimya, we we hufai kabisa, utaamini na wewe lazima umevuta mkwanja
 
CCM are a dying horse which kicks most prior to death. mwaka huu magamba lazima watafute vichaka vya kujificha.
 
Wananchi wameamua kuchoma moto kitanda chenye kunguni maana kimewasumbua kwa mda sasa na wamepata kitanda kingine.
 
alipoongelea usalama kulinda bahadhi ya watu ikiwa na CCM. ukumbi wote ulifurahi. basi hiyo ndiyo reflection ya jamii kwa watu usalama. wengi hawana imani nao tena
 
Ila hawa ccm wanaweza kuamuru gwajima akamatwe tena km walivofanya wkt wa sakata na pengo.
cm WANAPUMULIA MASHINE
 
JF Member

CCM wanunua watu kama SLAA alafu anakuja kutukana,bahati mbaya hajui hotuba ya kumezeshwa na CCM hatimaye kafanya presentation kama la pili vile.

 
Last edited by a moderator:
JF Member

Napingana na wewe, viongozi wa dini nao ni raia, uongozi ukiwa mbaya unaathiri moja kwa moja yeye, familia yake na waumini wake pia. Tena kwa sababu wao wanafanya kazi ya Mungu wana nafasi kubwa kuona tusiyoaona wengine. Sio sahihi kusema wakae kimya hata kama wanaona mambo yanaenda mrama na ukweli wanao. Gwajima angekaaje kimya wakati anaujua ukweli? Kwanza angemkosea Mungu na sisi. Mimi Nampa big up !!:peace:
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom