Ehud
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 2,685
- 337
Hayawi hayawiiii....sasa yamekua...ktk hali ambayo haikutegemewa na wengi...bodi ya Utalii Tanzania(TTB), imeanza kuitangaza tiba inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Kijiji cha Sumange, wilayani Loliondo.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa bodi hiyo, Geofrey Tengeneza, alisema wameanza kutengeneza picha na taarifa kuhusu tiba inayotolewa na babu huyo na kuzitangaza.
Alisema taarifa hizo zimeanza kusambazwa katika mitandao mbalimbali, ili kuueleza ulimwengu, aina mpya ya utalii inayopatikana nchini.Alisema tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni aina mpya ya utalii, inayopatikana hapa nchini na kwamba mataifa mengine hayana aina hiyo ya utalii.
"Sisi kama bodi tumeliona hilo na tumeanza kulifanyia kazi kwa sababu medical tourism ni aina ya utalii ambayo ni mpya hapa kwetu,"alisema.
Ofisa huyo alisema kazi yao ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwamba kazi hiyo imeanza kuzaa matunda baada ya kujitokeza kwa watu kutoka mataifa mbalimbali.
Tangu Mchungaji Mwasapile aanze kutoa tiba hiyo, mamia ya watu kutoka ndani na nje ya nchi, wamekuwa wakifurika katika Kijiji cha Samunge, kupata tiba hiyo.
Bodi ya Utalii yaanza rasmi kumtangaza Babu!