Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,237
Salaam Jukwaa,
Ni muda sasa nimekuwa nikikereketwa na jinsi ambavyo wizara yetu ya elimu ilivyoamua kushughulika na ugawaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo hapa nchini na wengineo wanaokwenda kusoma nje.
Uchunguzi wangu binafsi unaonesha kuwa hii bodi sasa imekuwa kama a bunch of robbers,yaani kundi la wanyang'anyi wanaotafuta means ya kuchukua pesa kwa watoto wa masikini bila kujali utu wa kuona haya.
Imejulikana kwa muda sasa kuwa bodi hii imekuwa ikikaribisha maombi ya mikopo kutoka kwa vijana walio tayari kuingia kwenye elimu ya juu,ambapo wakati mwingine,kwa sababu yenye sura ya utapeli kabisa,imewaagiza vijana kujiandikisha kwa ajili ya kuomba mikopo hiyo kabla hata matokeo yao ya form six hayajatoka.Hii inamaanisha kuwa kijana anaweza kufeli mitihani lakini akawa ameshaichangia bodi hii Tshs 30,000 ambayo ni gharama ya kujiandikisha kwa kila aombaye mkopo.maana yake ni nini??
Katika mwaka wa masomo wa 2011-2012 bodi ya mikopo,kama vile haitoshi,ikabuni mbinu nyingine ya kukusanya fedha za watoto wa maskini.Pamoja na kuwa waombaji mikopo wote walishalipa ada ya uombaji ya TShs 30,000 kila mmoja,bodi iliagiza wote wanaotaka kukata rufaa na kuomba tena mkopo walipe tena ada ya shilingi 5,000 kila mmoja.Ijulikane kuwa mara zote hizi asilimia zaidi ya 70 ya waomba mikopo wamekosa mikopo hiyo.
Sasa kali zaidi imetokea hivi sasa,kwa wanafunzi wanaoomba mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2012-2013. Bodi kama ilivyo ada,imeagiza wanafunzi wote kulipa ada ya uombaji mkopo ya tshs 30,000 kila mmoja.Uombaji huu unatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao tu(yaani online loan application system-OLAS).Kitu cha kushangaza ni kuwa pamoja na kuwa wanafunzi wamelipa pesa hizo,database ya bodi,kwa kipindi chote cha kuanzia April 2012 mpaka leo tarehe 30 June ambapo ni mwisho wa kujiandikisha kwa ajili mikopo,imekuwa na matatizo yasiyoisha yaliyofanya wanafunzi washindwe ku-apply.Maana yake ni nini???
Mimi kama mwathirika,ni shahidi tosha wa wizi huu wa bodi ulio dhahiri.Baada ya kulipa fedha ya kuomba mkopo,toka mwanzoni mwa April 2012,nimekuwa nikijaribu kila siku iendayo kwa Mungu kukamilisha uandikishaji kupitia website hii lakini mara zote kumekuwa na "system error",na tatizo jingine la kushindwa kusubmit form ambayo umeshajaza kama hatua moja wapo ya uombaji huu.Kwa hivi,pamoja na kuwa mimi na wenzangu wengi tumelipa hiyo pesa ya kuomba kuapply kwa ajili ya mkopo,tumelazimika kukubali kushindwa na kukubali hiyo pesa ipotee.Je huu si wizi wa mchana??
Bodi hii inatupeleka wapi??ni juzi tu tumesikia ambavyo fedha zinatolewa bodi kama zinazopelekwa kwa wanafunzi wa vyuo lakini zikaishia mikononi mwa wajanja huku watoto wa masikini,wenye haja ya kusaidiwa wakiishia kuamua kudrop kutoka vyuo sababu ya kushindwa kumudu gharama(mimi ni shahidi wa hili).Kwanini bodi isiweke alternatives mbili ya kuapply kwa mikopo??yani kuwe na online system pamoja na manual system??nina uchungu sana na jinsi ambavyo sekta hii ya serikali imeendelea kujiendesha kama mradi wa wizi wenye lengo la kukusanya pesa badala ya lengo la awali la kusaidia watanzania.
Je serikali imekuwa long-con artists??
Inaniuma.