Biteko: Watanzania wanataka umeme, kama hakuna umeme hawatuelewi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
45,536
52,594
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko ameitaka Bodi ya Tanesco kuhakikisha Umeme unapatikana Kwa Watanzania vinginevyo hawawaelewi Wala hawataielewa Serikali.

Amewataka viongozi walioaminiwa na kubeba dhamana ya Rais kuhakikisha Umeme unapatikana kwamba ndio salama Yao vinginevyo atalazimika kutafuta mchawi.


My Take: Ni hatua nzuri ila mheshimiwa punguza hotuba za Matumaini fanya kazi umeme na mafuta vipatokane Ili uwe Waziri Bora kama ulivyosema.
 
Umeme, maji, mafuta( diesel, petroleum, kerosene etc.) hizi ni resources muhimu mno ktk maendeleo ya nchi yoyote Ile bahat mbaya hizi resources serikali wahazitilii maanani San,,

umeme unaweza kata hata 3 day bila serikali kuchukua hatua yoyote bila kujali kuwa Kuna wafanya biashara bila umeme kazi zao haziendi na still end the day TRA, pango la frem hawataelewa kuhusu hiz loss( za kukatika Kwa umeme).
 
Yaani ni kama wanamjibu kwamba haliwezekani. Leo wamekata umeme toka saa mbili hadi muda saa 12 jioni hawajurudisha . Tusipofanya maamuzi magumu kuikataa ccm watanzania tutabaki masikini
Anatakiwa ajue tatizo liko wapi kusema haamini kwenye pesa ila rasilimali ya watu ni empty words zisizo na msingi.

Saizi Yuko kwenye Fungate ikiisha tuu ajiandae na balaa.
 
Ni moja ya kauli bora ya kutia matumaini ambayo haijawahi kusikika ndani ya miaka miwili ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo ya Mh Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ni kama imeibua shangwe na kuenea almost kila kona ya Tanzania tangia itoke jana.

Nadhani huko aliko Mh Rais anasema, kweli hapa nimelamba dume,uteuzi wa Mh Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh Biteko ni kulamba dume kwa Serikali ya awamu ya Sita, moja ya Uteuzi bora sana.

Tusubilie sasa uwake na lazima uwake, nipo pale.

 
Mh Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati @ Dotto Biteko ukitaka kufanikiwa kutanzua kikwazo cha ufanisi wa TANESCO sambaratisha hiyo bodi ya wafanyabiashara iliyorundikwa kwa kupanga bei za juu kwa maslahi binafsi utakuja kushukuru hilo dubwana ukiling'oa maana wamewekwa na aliyekuwa waziri mbishi na jeuri wa milimani kama uchochoro wa kukwapua jasho la Watanzania bila haki.
 
PRESIDENCIAL MATERIAL.
#Tatizo lipo kwenye uzalishaji (insufient) umeme?
#Tatizo lipo kwenye supply ya umeme?
Wapi penye tatizo
-BILA UMEME WA UHAKIKA MAENDELEO NI NDOTO!
Dk. Samiah fanya umeme kukatika iwe istoria ndani ya Tanzania,kazi hii moja tu inatosha.
 
Hata bwawa likianza uzalishaj kiukwel cwez aminishwa tatizo la umeme limekwisha. Labda uzalishaj ufanyike mfululizo ndan ya miaka mitatu bila tatizo la umeme, hapo ntaamin!!
 
Hata bwawa likianza uzalishaj kiukwel cwez aminishwa tatizo la umeme limekwisha. Labda uzalishaj ufanyike mfululizo ndan ya miaka mitatu bila tatizo la umeme, hapo ntaamin!!
Mgao hautakuwepo ila blackouts zitaendelea
 
Hawaeleweki hawa wanaweza kutukatia ili mradi tuu na sisi tuteseke.. wakat saiv umeme ukikata hata dakika 10 watu tunajiuliza kuna nn leo!!
Kama Zambia wanauza umeme bei kubwa watakata na kuweka wa kwetu
 
Nimemsikia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Comrade Biteko akisema Watanzania wanahitaji umeme. Ndio, shida yetu ni umeme,sio maneno matupu wala marathons.

Hii inaweza kuwa kweli,maana kwa siku tatu mfululizo sasa,umeme haujakatika.Hii haikuwahi kutokea kabisa katika kipinfi cha January Makamba. Kama Biteko ataendelea hivi,itakuwa na maana moja tu, kwamba Makamba alikuwa anawahujumu Watanzania kwa maslahi yake binafsi au kwa kutumwa.

Hata hivyo naamini hakuna mtu timamu aliyewahi kudhani kwamba Makamba will deliver,na hata Wizara ya Mambo ya Nje ambapo kapelekwa,naami kabisa mambo hayatakuwa tofauti.

Nimepata taarifa nyingi kuhusu Comrade Biteko.Nikiri kwamba taarifa zote nilizopata zina-prove kwamba ni mchapakazi hodari na committed to whatever he does.Siajabu Samia amem-retain pamoja na kunyanyapaa wateule wengi wa Hayati Magufuli. Siajabu pia kwamba Samia amemteua kuwa Naibu Waziri Mkuu,ili kuimarisha utendaji katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

So far so good Biteko,keep it up.I wish you all the best of luck and success to whatever you do.Tunaomba tu
usituangushe Watanzania kama mtangulizi wako January Makamba.
 
Back
Top Bottom