Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
(Mwananchi)
SIKU chache tu, baada serikali ya Tanzania kushutumiwa na nchi za Ulaya kuhusu mauaji ya kinyama ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, Sauda Ibrahim (20), ametekwa nyara na kuuawa kinyama na watu wasiojulikana wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Mwanamke huyo mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kijiji cha Kagondo, Kata Runazi aliuawa saa 2:00 usiku Septemba 3, mwaka huu akiwa matembezini.
Baada ya kumteka nyara, watu hao walimcharanga mapanga na kisha wakatokomea kusikojulikana na mkono wake wa kulia.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Arthur Magoti, amethibitisha tukio hilo na kwamba jeshi hilo linaendelea na msako mkali kuwatafuta watu hao.
Tukio hilo linafanyika huku kukiwa na taarifa kutoka Bunge la Jumuiya za Nchi za Ulaya (EU) inayohimiza serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti zaidi kukomesha mauaji hayo ya kinyama yanayotawaliwa na imani za kishirikina.
Kamanda Magoti alisema wauaji hao walimteka nyara albino huyo njiani na kuanza kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi alipopoteza maisha.
Alieleza kuwa baada ya kuhakikisha kuwa ameshafariki, walimkata mikono yote, wachukua wa kulia na kuacha wa kushoto na viungo vyake vingine katika sehemu ya tukio pamoja.
Alisema hadi sasa hakuna mtuhumiwa aliyekwisha kamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na watu wanaohusika na vitendo hivyo.
Mkoa wa Kagera nao umeanza kukabiliwa na mauaji ya albino yanayotokana na imani za kishirikina ambayo hapo awali yalitikisa mikoa minmgine jirani ya kanda ya ziwa.
Huyu ni albino wa pili kuuawa ndani ya miezi mwili baada ya watu wasiojulikana walimvamia nyumbani kwake Jovin Majaliwa (46) mkazi wa Kijiji cha Nyantakara wilayani Chato na kumuua kwa kumcharanga mapanga.
Hivi karibuni Bunge la Umoja wa Ulaya lilitoa azimio la kulaani vitendo hivyo na kuitaka Tanzania kuchukua hatua za ziada kukabiliana na mauaji hayo, ikiwa ni pomoja na kuelimisha jamii kuachana na imani hizo potofu ambayo imeshapoteza maisha ya albino zaidi ya 25.
Akizungumzia mikakati yake kuhusiana na suala hilo, Kamanda Magoti alisema kupitia programu ya polisi jamii na shirikishi wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi, ili waweze kuwafichua watu wanaojihusisha na mauaji ya watu hao.
My Take:
Usikose toleo la "Cheche" la kesho lenye habari zinazoendana na mkasa huu. Tungependa kuweza kusambaza kijarida hicho nyumbani kesho kwa kadiri tunavyoweza. Yeyote anayetaka kushiriki katika kukisambaza hasa mikoa ya magharibi, kusini na Kanda ya Ziwa atuandikie mhariri(at)klhnews.com ili upate nakala yako usiku huu tayari kwa kusambaza.
Tunasikitika na kuguswa kwa namna ya pekee na matukio haya ya kinyama ambayo yanafanywa kana kwamba katika Tanzania hakuna utawala wa sheria na kanuni ya msituni inatawala.