Binti wa Kitanzania auawa kwa kukatwakatwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
(Mwananchi)

SIKU chache tu, baada serikali ya Tanzania kushutumiwa na nchi za Ulaya kuhusu mauaji ya kinyama ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, Sauda Ibrahim (20), ametekwa nyara na kuuawa kinyama na watu wasiojulikana wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Mwanamke huyo mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kijiji cha Kagondo, Kata Runazi aliuawa saa 2:00 usiku Septemba 3, mwaka huu akiwa matembezini.

Baada ya kumteka nyara, watu hao walimcharanga mapanga na kisha wakatokomea kusikojulikana na mkono wake wa kulia.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Arthur Magoti, amethibitisha tukio hilo na kwamba jeshi hilo linaendelea na msako mkali kuwatafuta watu hao.

Tukio hilo linafanyika huku kukiwa na taarifa kutoka Bunge la Jumuiya za Nchi za Ulaya (EU) inayohimiza serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti zaidi kukomesha mauaji hayo ya kinyama yanayotawaliwa na imani za kishirikina.

Kamanda Magoti alisema wauaji hao walimteka nyara albino huyo njiani na kuanza kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi alipopoteza maisha.

Alieleza kuwa baada ya kuhakikisha kuwa ameshafariki, walimkata mikono yote, wachukua wa kulia na kuacha wa kushoto na viungo vyake vingine katika sehemu ya tukio pamoja.

Alisema hadi sasa hakuna mtuhumiwa aliyekwisha kamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na watu wanaohusika na vitendo hivyo.

Mkoa wa Kagera nao umeanza kukabiliwa na mauaji ya albino yanayotokana na imani za kishirikina ambayo hapo awali yalitikisa mikoa minmgine jirani ya kanda ya ziwa.

Huyu ni albino wa pili kuuawa ndani ya miezi mwili baada ya watu wasiojulikana walimvamia nyumbani kwake Jovin Majaliwa (46) mkazi wa Kijiji cha Nyantakara wilayani Chato na kumuua kwa kumcharanga mapanga.

Hivi karibuni Bunge la Umoja wa Ulaya lilitoa azimio la kulaani vitendo hivyo na kuitaka Tanzania kuchukua hatua za ziada kukabiliana na mauaji hayo, ikiwa ni pomoja na kuelimisha jamii kuachana na imani hizo potofu ambayo imeshapoteza maisha ya albino zaidi ya 25.

Akizungumzia mikakati yake kuhusiana na suala hilo, Kamanda Magoti alisema kupitia programu ya polisi jamii na shirikishi wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi, ili waweze kuwafichua watu wanaojihusisha na mauaji ya watu hao.

My Take:
Usikose toleo la "Cheche" la kesho lenye habari zinazoendana na mkasa huu. Tungependa kuweza kusambaza kijarida hicho nyumbani kesho kwa kadiri tunavyoweza. Yeyote anayetaka kushiriki katika kukisambaza hasa mikoa ya magharibi, kusini na Kanda ya Ziwa atuandikie mhariri(at)klhnews.com ili upate nakala yako usiku huu tayari kwa kusambaza.

Tunasikitika na kuguswa kwa namna ya pekee na matukio haya ya kinyama ambayo yanafanywa kana kwamba katika Tanzania hakuna utawala wa sheria na kanuni ya msituni inatawala.
 
Akizungumzia mikakati yake kuhusiana na suala hilo, Kamanda Magoti alisema kupitia programu ya polisi jamii na shirikishi wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi, ili waweze kuwafichua watu wanaojihusisha na mauaji ya watu hao.

Sambamba na kutoa "elimu" Kamanda Magoti u need to act now...
 
this is too much!. serikali inabidi ichukue hatua za makusudi kuwalinda ndugu zet hawa
Ni muhimu kwa serikali kuu kushirikiana na serikali za mitaa ili kusambaza elimu,kama vile ni kitu gani hasa kinapelekea baadhi ya watu kuwa maalbino, na kwamba ushirkina ni adui wa maendeleo, kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kushirikiana na maalbino katika shughuli za uzalishaji mali, kutoa huduma za ziada kama afya na elimu ili kuwawezesha maalbino kujikwamua. na pia zitungwe sheria maalumu za kuwalinda ndugu zetu hawa
 
Mkjj hicho kijarida ni cha bure?

BTW nashindwa kuilewa serikali ambayo ina chombo kiitwacho TBC japo kutengeneza onyo hata ni la dakika moja tu kwenye TV ili kuokoa wananchi wake.

Serikali hata kama ingegharimu hilo tangazo/onyo kuliuza kwenye TV za biashara ili watanzania tuondokane na ujinga huu.
 
Inasikitisha, hivi kweli tuna jeshi la polisi? Mheshimiwa Masha, vipi, kazi inakushinda? Nenda kwa Mrema akakfundishe mbinu za kukomesha ujinga huo mara moja.
 
Sasa utaifa wa marehemu unahusika vipi na mauaji yake wakati ameuawawa ndani ya Tanzania? Mimi nilidhani kauwawa Ughaibuni ...
 
Sasa utaifa wa marehemu unahusika vipi na mauaji yake wakati ameuawawa ndani ya Tanzania? Mimi nilidhani kauwawa Ughaibuni ...

To get your attention.

Haya wewe unaliona vipi hili suala? maana hukuonyesha msimamo wako.

PS kauwawa magharibi ndani ya Tanzania mtanzania ni mtanzania, na mtanzania anayejali mwenzake lazima limshitue
 
Jambo hili linafanyiwa mzaha na serikali kama kawaida yetu we are not serious with anything, even our own safety. Kama serikali ingechukulia janga hili kwa makini nina imani hawa wapuuzi wenye imani za kijinga wangeelimika kidogo, hakuna uhusiano wowote kati ya ngozi ya albino na utajiri! hivi tutaelimika lini jamani? kweli Ujinga ni mzigo mzito kuliko yote duniani.. na tunazidi kudidimia kila kukicha.
Waziri wa mambo ya ndani amka usingizini; do something to help those souls, inauma sana kusikia haya mambo bado yanaendelea kuhatarisha maisha ya albino ambao still have a lot to deal with just being albino, besides worrying about their own safety now!
 
To get your attention.

Haya wewe unaliona vipi hili suala? maana hukuonyesha msimamo wako.

PS kauwawa magharibi ndani ya Tanzania mtanzania ni mtanzania, na mtanzania anayejali mwenzake lazima limshitue

Hii si sawa. Kama angeuwawa na raia wa kigeni ndani ya Tanzania au angeuwawa nje ya Tanzania ningeelewa. Ni muhimu kutumia context inayofaa kwenye kuandika habari, haswa vichwa vya habari. Vinginevyo inakuwa ku-sensationalize habari tu, na wasomaji wanaishia kuwa dissapointed and feel cheated.
 
Matukio kama haya yanaashiria jamii iliyo bado katika ujima. Imani....imani....imani...imani potofu?
 
(Mwananchi)

SIKU chache tu, baada serikali ya Tanzania kushutumiwa na nchi za Ulaya kuhusu mauaji ya kinyama ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, Sauda Ibrahim (20), ametekwa nyara na kuuawa kinyama na watu wasiojulikana wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Mwanamke huyo mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kijiji cha Kagondo, Kata Runazi aliuawa saa 2:00 usiku Septemba 3, mwaka huu akiwa matembezini.

Baada ya kumteka nyara, watu hao walimcharanga mapanga na kisha wakatokomea kusikojulikana na mkono wake wa kulia.

Mkoa wa Kagera nao umeanza kukabiliwa na mauaji ya albino yanayotokana na imani za kishirikina ambayo hapo awali yalitikisa mikoa minmgine jirani ya kanda ya ziwa.

Huyu ni albino wa pili kuuawa ndani ya miezi mwili baada ya watu wasiojulikana walimvamia nyumbani kwake Jovin Majaliwa (46) mkazi wa Kijiji cha Nyantakara wilayani Chato na kumuua kwa kumcharanga mapanga.

Hivi karibuni Bunge la Umoja wa Ulaya lilitoa azimio la kulaani vitendo hivyo na kuitaka Tanzania kuchukua hatua za ziada kukabiliana na mauaji hayo, ikiwa ni pomoja na kuelimisha jamii kuachana na imani hizo potofu ambayo imeshapoteza maisha ya albino zaidi ya 25.

Tunasikitika na kuguswa kwa namna ya pekee na matukio haya ya kinyama ambayo yanafanywa kana kwamba katika Tanzania hakuna utawala wa sheria na kanuni ya msituni inatawala.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuwa Wanadamu wanaofanya mambo haya wanaweza wakawa na majina ya Kikristo au Kiislam yaani ni watu ambao wanaamini kwa mungu.

Hawa watu wana majina yaliyo hai lakini nao wamekufa.

Shime viongozi wa DINI endeleeni kuwaelimisha waumini wenu maana mioyo ya watu imekuwa ya jiwe siku hizi.
 
Kama waganga wa tiba za kisasa wana chama chao ambacho huwa kinachukua hatua wakati daktari akiboronga...nadhani tunahitaji vyama vya aina hiyo kwa ajili ya kusajili waganga wote wa jadi na ku-monitor shughuli zao. Kwa vyovyote hawa wauaji watakuwa wamepewa hii kazi na mteja + mganga.

Kwa wingi wa waganga wa jadi ulivyo level za vyama inaweza kuanzia kwenye kata, wilaya etc...lakini la maana zaidi ni kwa watu wataokabidhiwa dhamana ya uongozi ya vyama hivi kuwajibika kweli kweli ili kuweza kumaliza tatizo hili kwa kushiriakiana na vyombo vya dola kama polisi, mahakama etc.....Ikibidi vile vile sheria zinazotawala masuala ya tiba za asili/uganga bunge linaweza kuzingalia kama zina udhaifu zikapewa nguvu zaidi.

Tusipoangalia yanaweza kurudi yale mauaji ya kuua wachawi kama ilivyokuwa maarufu miaka kadhaa nyuma hasa mikoa ya kanda ya ziwa.

Au serikali inakata kama haya hapa chini yaliyotokea ulaya karne 16 na 17 yaanze.....manaake wanaonekana kama wamelala kwenye suala hili

http://graphics8.nytimes.com/images/blogs/freakonomics/pdf/OsterWeatherWitchcraft.pdf
 
Back
Top Bottom