Mizizi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,275
- 391
Ni dalili ya wazi kwamba ile dhana ya uzalendo iliyodumu kwa muda mrefu hapa Tanzania imeelekea kutoweka!
Kikubwa na cha kushtusha ni kusikia taarifa ya Lundenga kwamba alipata taarifa saa tisa alasiri, wakati bado roho za watanzania zikiwa zinaendelea kuelea ndani ya maji ya kina kirefu kwenye bahari ya hindi.
Ila lingine la kusikitisha ni kwamba, katika wadau wa tukio hilo ni Mtoto wa aliyekuwa katibu mkuu wa ccm taifa hivi karibuni! Hii inaonyesha udhaifu wa hawa viongozi wetu katika malezi na makuzi ya vijana wao katika masuala ya uzalendo na tamaduni za watanzania. Kama viongozi wetu wanatoa pruducts kama hizi majumbani mwao, tusitegemee mazuri kwenye utendaji wao kama methari ya kingereza inayotafsirika kwa kiswahili "nionyeshe rafiki yako, nikuambie tabia yako"
Nilichojiuliza hapa ni kwamba, Mdhamini ndie mwenye influence katika project yeyote kutokea, sasa hapa vodacom hawawezi kwa namna yoyote ile kujiondoa kwenye lawama juu ya kadhia hii!
Kufanya tukio la Miss Tanzania huku roho za watanzania zikiwa zinahangaika majini kuokoa uhai wao ni dharau kubwa kwa wahanga ha tukio hilo
Pia Tukio hilo halikuwa na hadhi kuitwa miss Tanzania, kwa kuwa baadhi ya watanzania walikuwa katika ajali, na wengine walikuwa ni maiti zinazoelea majini!
Ushauri wangu ni kwamba!
1. Vodacom inatakiwa ijitokeze na kuomba radhi wa tz na wazanzibari kwa dharau waliyoionyesha juu ya hili
2. Serikali ya Muungano itoe tamko juu ya hili kabla ya kuongeza mpasuko juu ya muungano wetu
3. Watanzania wanaotoka znz wasusie, huduma, matukio, na misaada yoyote itokayo vodacom hadi pale watakapoomba radhi kwa dharau waliyoonyesha kwao!
Nawasilisha