Binti hajawahi kuniona uso kwa uso ila ananiomba hela

Kuna binti enzi za o-level nilimfukuzia kumpata kwa bahati mbaya sikuweza kupata chance hata ya kuongea nae...Kwa bahati fulani ivi binti alichaguliwa kujiunga O-level form one kipindi kile 2012...wakati anajiunga mimi ndo nilikiwa namaliza Form 4,,, basi bwana kwa bahati mbaya sikuweza kupata ukaribu wake wakati huo...japo yeye alikuwa hanifahamu ila mimi ndo nilikuwa namjua..

Mwaka..2017 kwny pita pita za Facebook..nikaweza kupata mawasiliano yake,tukawa tunachati Fb...nikaamua kumfungukia kuwa nilimpenda sana tangu way back miaka hiyo ya 2012 mpaka sasa bado nampenda..tukabadilishana namba za Whatsapp ,tukaanza kuchati kupitia huko...Tatizo binti hanifahamu mimi zaidi ya kuona picha zangu tu za Facebook ila mimi namfahamu..

Baada ya hapo binti kanikubalia tukawa wapenzi japo hajawai kuniona uso kwa uso...
KINACHONISHANGAZA...
Binti anaanza kuniomba PESA eti nimsaidie ana shida...

SWALI LANGU...
..SASA BINTI ATAWEZAJE KUNIOMBA PESA WAKATI HATUJAONANA?

Si zitakuwa dalili za Mizinga hizi?[/QUOTE
mwambie mfanye barter trade, no free lunch :D:D
 
Wadada wengi wa cku hizi wanapenda sana mizinga, mimi ndo wakiniambia tu “baby nikuambie kitu " hapohapo nakata simu na kuzima. Ngoja kwanza hizo buku tano nimlishe mama angu aliyenisomesha kwa shida na taabu.
Hata wale wanaohongaga sio kwamba hawana wazazi kila Mtu Ana nafasi yake kwako
 
Maswali mengine, nyie wanaume mnajitia aibu.

Kwani kafanya kosa, wewe si mpenzi wake au? Unataka upate tunda ndio useme wako?

Kingine jua kuwa haumfajamu hata tabia (hilo lingine).

Muwe mnajiongeza jamani, baadae mkizidiwa akili mnajua kulalamika kama kihivi. Mpe pesa kwani unafikiri data ya kumshindisha mnachati unataka akawaombe wazazi wake? Na si ni mwanafunzi au leo hujui...

Mkijiendekeza na kusoma ya humu na kuyaweka maishani, mtakosa wake wema.
Asante
 
Hey mrushie hela ya vocha mtoto wa watu ili achat na wewe vizuri maana inaonekana mma huitaki
 
We umafikiri kwann amekukubalia hata bila kukufahamu, anataka pesa uyo..!
 
Huwezi jua mkuu,anaweza kuwa si kama umdhaniavyo ama udhaniavyo. Cha msingi wewe mtu mzima pima toka muanze mahusiano anamwelekeo upiI{character} ingawa si kipimo saaana. Si wote wanakuwa wapigaji kama udhaniavyo.
Mimi hapa ni shahidi wa hili. Wife tulijuana kwa njia ya simu tu na tukafanya mwendelezo wa mawasiliano ambayo mwisho wa siku yalizaa mahusiano na mpaka kufikia kuafikiana kuwa mke na mme.
So usimhukumu zaidi ni wewe mwenyewe kupima mwenendo wenu na si lazima umpe hela nyiingi. Kwa kuwa ulisha amua,nenda naye taratibu mwisho wa siku hata likubuma iwe ni hasara ndogo ambayo haita kuumiza
 
Mwanaume mwenzangu nawe, cha ajabu nn sasa? Mbona ww ulimwomba muwe wapenzi na akakubali. Nawe mkubalie pia ombi lake tu. Wanasema mwanaume bila pesa ni sanamu nae anapima ucje ukawa ni sanamu eti
 
Maswali mengine, nyie wanaume mnajitia aibu.

Kwani kafanya kosa, wewe si mpenzi wake au? Unataka upate tunda ndio useme wako?

Kingine jua kuwa haumfajamu hata tabia (hilo lingine).

Muwe mnajiongeza jamani, baadae mkizidiwa akili mnajua kulalamika kama kihivi. Mpe pesa kwani unafikiri data ya kumshindisha mnachati unataka akawaombe wazazi wake? Na si ni mwanafunzi au leo hujui...

Mkijiendekeza na kusoma ya humu na kuyaweka maishani, mtakosa wake wema.
Nh mmmmm mmmmm mmmmm mmmmm mmmmm mmmmm ni shdaaaahh
 
Wadada wengi wa cku hizi wanapenda sana mizinga, mimi ndo wakiniambia tu “baby nikuambie kitu " hapohapo nakata simu na kuzima. Ngoja kwanza hizo buku tano nimlishe mama angu aliyenisomesha kwa shida na taabu.
Kwel mkuu... Na tunavojisahaug sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom