Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,226
- 12,733
Leo hii duniani hakuna ugonjwa unaoua watu wengi kama kuzeeka. Zaidi ya asilimi 60 ya watu wanaokufa leo hii wanakufa sababu ya uzee.
Ugonjwa wa kuzeeka unatokea pale seli za mwili zinapoacha kugawanyika na kutengeneza seli mpya. Inadaiwa kuwa kwa wastani seli ya binadamu inaweza kugawanyika mara 50 tu katika maisha yake yote. Baada ya hapo mwili unaanza kuzeeka sababu hauundi seli mpya.
Kuna viumbe havikabiliwi kabisa na ugonjwa huu. Viumbe kama bakteria na miti havisumbuliwi na ugonjwa wa kuzeeka.
Binadamu anaweza kutibu ugonjwa huu wa kuzeeka. Mfano anaweza kubadili genetic yake na kufanya seli zake zisiache kuunda seli mpya? Anaweza kujipandikiza genes za wanyama kama kobe ili kuchelewesha ugonjwa huu wa kuzeeka? Kuna namna binadamu anaweza kufanya kukabiliana na ugonjwa wa kuzeeka?