Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Bili yamponza aliyejirusha ghorofani
Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 31st December 2010 @ 23:5
KIFO cha mwanamke anayedaiwa kujirusha ghorofani juzi kilitokana na yeye kujaribu kukimbia bili ya vinywaji na vyakula akiwa na wenzake kwenye baa iliyoko ndani ya jengo la Benjamin Mkapa Tower.
Mwanamke huyo alianguka kutoka ghorofa ya tatu na kupasuka kichwa na kuvunjika mkono akikwepa kulipa Sh 95,000 alizokuwa akidaiwa, Polisi imesema.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema jana kuwa marehemu ambaye hadi sasa hajatambuliwa jina, aliingia katika baa ya Savanna ghorofa ya tatu akifuatana na rafiki yake wa kiume na dereva teksi aliyewapeleka hapo.
Alisema akiwa hapo na rafiki yake huyo ambaye pia hajajulikana na dereva teksi huyo, walikunywa vinywaji mbalimbali na kula kuku hali hata kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Baada ya hapo wahudumu walisema mwanamume alijifanya kwenda chooni na kutokomea
huku nyuma wenzake wakimsubiri, aliongeza.
Inadaiwa mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30 na mwenzake waliosalia walitaka kuondoka, lakini uongozi wa baa hiyo uliwazuia mpaka walipie vinywaji na chakula.
Kwa mujibu wa Shilogile, hali hiyo ilisababisha malumbano na ndipo mmoja wa wafanyakazi wa baa hiyo alipomdhamini dereva kwa kumlipia Sh 42,000 huku marehemu huyo akitakiwa kulipa Sh 43,000 zilizosalia.
Kutokana na kutokuwa na fedha, alianzisha malumbano huku akiondoka kwenda nje ya baa huku akifuatiwa na walinzi, lakini kabla hajafikiwa, alijirusha chini ya ghorofa na kufariki dunia.
Aidha, alisema kwa sasa Jeshi lake linaendelea na upelelezi kumtafuta mwanamume aliyekuwa naye huku likisaidiwa kwa karibu na dereva teksi huyo kwa madai kuwa huenda akawa anamfahamu.
Alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa kuwa bado haujatambulika na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.