Bila uzalendo Jakaya Kikwete asingemteua Hayati Magufuli

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Amani iwe nanyi wadau

Pamoja na kwamba Jakaya Kikwete amekuwa kiongozi kwa muda mrefu hadi kuwa rais wa Tanzania kwa miaka kumi ,nakiri wazi sikuwahi kuujua uzalendo wake kwa nchi ya Tanzania hadi leo November 2018 ndiyo nimegundua!

Nimejiridhisha pasina shaka kuwa Jakaya Kikwete ni mzalendo wa kweli wa nchi kuliko tunavyonfikiria.
Jakaya Kikwete ndiyo alikuwa na uamuzi wa mwisho nani awe rais ajae wa Tanzania lakini akatuletea Magufuli.

Jakaya Kikwete alikuwa anamjua Magufuli kuliko mtu mwingine yoyote , alikuwa anajua kabisa Magufuli hapendi rushwa na ufisadi ,alikuwa anajua kabisa Magufuli ana msimamo mkali usioyumba hata kwa dakika moja ,alikuwa anajua kabisa Magufuli kwake ni Tanzania kwanza na haoni shida kugombana na yeyote anayekanyaga masilahi ya Tanzania!

Swali kwa nini Kikwete pamoja na kuyajua yote haya bado akamteua Magufuli?

Jibu ni rahisi tu ,Kikwete ni mzalendo wa kweli ndiyo maana alitaka amwachie nchi mzalendo wa kweli mwingine( Simba huzaa Simba). Kama Kikwete angekuwa ni fisadi kamwe nasema kamwe asingeruhusu Magufuli awe rais wa Tanzania na uwezo huo alikuwa nao.

Hotuba ya rais Magufuli leo kwenye kongamano pale udsm imeweka kila kitu wazi na kuacha bila shaka yoyote kwamba Magufuli anaijua Tanzania na ni mzalendo wa kweli kweli kwa nchi yake. Amezungumza kwa facts na data nchi ilipotoka ,ilipo na inaelekea wapi !

Magufuli ameonyesha wazi mchana kweupe kuwa ana uelewa mkubwa sana na inahitaji akili kubwa kumwelewa .Akili ndogo (chadema) kwa sasa hawatamwelewa Magufuli watakuja kuelewa baada ya miaka 20 ijayo.

Asante mzalendo Jakaya Kikwete kwa kuzaa mzalendo John Magufuli kwa manufaa ya nchi yetu .

Mungu akubariki sana na akupe maisha marefu.
 
Leo ni november 2018 ama madhara ya copy and paste bila ku edit ?

"Pamoja na kwamba Jakaya Kikwete amekuwa kiongozi kwa muda mrefu hadi kuwa rais wa Tanzania kwa miaka kumi ,nakiri wazi sikuwahi kuujua uzalendo wake kwa nchi ya Tanzania hadi leo November 2018 ndiyo nimegundua!"
 
Back
Top Bottom