Bila Kutumia Uchawi Chama Hawezi Kucheza Vizuri Kwenye Mechi Ngumu.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Kuna ule msemo kuwa Chama ni mchezaji wa mechi ndogo, leo umeanza kuniingia kichwani. Inafika kipindi unawaza, hivi huenda labda kwenye mechi hizi za Ligi huwa hawatumii Uchawi ndio maana Chama anaonekana wa kawaida.

Kwenye mechi kama hizi mchezaji tegemeo wa timu ndipo unapaswa kutokea na kuibeba timu kwa uwezo wako binafsi. Sio kungoja mpaka mechi ifanyike kwa Mkapa ndio unafanya vizuri.

Binafsi bado nitaendelea kumuweka PACOME juu ya CHAMA kwasababu ndogo ndogo kama hizi.

Mchezaji mzuri huwa anakuwa na consistace isiyo na shaka.

Mchezaji mzuri hachagui uwanja wa kufanya vizuri.

Nina shaka. Huenda Juju zinam-boost jamaa katika baadhi ya mechi hata kuwafanya watu wa Simba kuomini kuwa yule ndio mfalme wao.
 
Sio juju muzeee chama ni mchezaji wa vimechi vidogo vidogo akikutana na watu wa maana hua hana madhara.
Ukitaka kuamini hili tazama mechi zote ngumu kama ulimuona chama akifanya yale ya Jwaneng Galaxy au Horoya..
Bado tu unahangaika na chama? mechi mliyopigwa 4-1 na Simba ilikuwa nyepesi?Mechi ya Simba na Nkana Chama akatupia goli la 3 ilikuwa nyepesi?
 
Kuna ule msemo kuwa Chama ni mchezaji wa mechi ndogo, leo umeanza kuniingia kichwani. Inafika kipindi unawaza, hivi huenda labda kwenye mechi hizi za Ligi huwa hawatumii Uchawi ndio maana Chama anaonekana wa kawaida.

Kwenye mechi kama hizi mchezaji tegemeo wa timu ndipo unapaswa kutokea na kuibeba timu kwa uwezo wako binafsi. Sio kungoja mpaka mechi ifanyike kwa Mkapa ndio unafanya vizuri.

Binafsi bado nitaendelea kumuweka PACOME juu ya CHAMA kwasababu ndogo ndogo kama hizi.

Mchezaji mzuri huwa anakuwa na consistace isiyo na shaka.

Mchezaji mzuri hachagui uwanja wa kufanya vizuri.

Nina shaka. Huenda Juju zinam-boost jamaa katika baadhi ya mechi hata kuwafanya watu wa Simba kuomini kuwa yule ndio mfalme wao.
Mambo ya kitoto kumfananisha zidane na huyo komwe iwe mwanzo na mwisho
 
Simba ni mbovu kasoro wachezaji wachache mmoja mmoja wakati huo yanga wako vizuri kila idara.huyo pacome wako ukimpeleka simba ya sasa unaweza ukampiga na vibao.Unaweza ukawa na mchezaji mzuri lakini kama kazungukwa na wachezaji wa kawaida huo uzuri wake hauwezi kuonekana au kua endelevu ata kama atapambana vip.mpira ni mchezo wa wachezaji 11 hao wazuri wanang'arishwa na wazuri wengine.
 
Kwa hiyo mechi mbili tuu ngumu ndio amefanya vizuri?
Chama keshawafunga Al Ahly goli mbili peke yake,kawafunga AS Vita iliyokuwa bora ya akina Nelson Munganga,Makusu,Ngoma na Bangala,anashika namba 8 ya wafungaji bora wa muda wote na hizo goli 18 zote kazifunga timu zilizoanzia makundi Klabu bingwa,hatua ambayo Yanga ameshindwa kuingia kwa zaidi ya miaka 25
 
Back
Top Bottom