Bila kufanya haya, tusahau suala la kuondokana na Mgao wa Umeme

Tatizo letu kwenye suala la umeme kama nchi wala sio upungufu wa umeme bali uongozi unaosimamia taasisi husika, wafanyabiashara wahuni pamoja na wanasiasa wasio wazalendo.
 
Bado sijapata hoja yako vizuri ndugu ingawa unaonekana unayo.

Hiyo storage concern issue yake ni nini hasa? Umeme wa Solar si unazalishwa kila siku?

Hizo nchi za Uarabuni mbona hatusikii iyo unayosema storage concern?
Issue ni energy mix solar ni percent ngapi ya wanachozalisha ? Umeme tuseme ni kama maji yanatoka kwenye mpira kwahio yakitoka ni either unayatumia kwa wakati huo (kuoga au kumwagilizia) au kuyatunza kwenye ndoo.., Sasa issue ni hapo kwenye utunzani (kama tukirely percent kubwa kwenye solar na upepo inamaanisha tuwe na ndoo za kutosha za kutunza ili usiku wakati hakuna jua tuweze kutumia ule tuliotengeneza mchana... Battery za Lithium ni expensive ingawa ni efficient; kwa watu kuona hilo ndio maana sasa hivi watu wanaangalia option nyingine za battery hio mfano mechanical (kunyanyua vitu vizito au cranes kwenye mashimo ya caves na old mines wakati wa jua linawaka au umeme unatengenezwa ili kutunza umeme huo) hii ni very inefficient..., au storage kwenye hydrogen cells (storage hydrogen bado not as efficient) au kwa kutumia new materials carbon graphene (hii bado ipo kwenye uchunguzi ingawa ni promising)

Kwahio the most efficient large scale battery to date ni HEP (Hydro Electric Power Plants) kama Bwawa la Nyerere.., Umeme wa jua ukizalishwa mchana au upepo ukivuma unawekwa kwenye Grid na offpeak times unatumika kupump maji kutoka reservoir ya chini na kuyarudisha juu ili ikifika usiku au peak time same maji yanaachiwa tena ili kuzalisha umeme...

Bila hivyo huenda tukahitaji kununua Battery za kuweza kuhifadhi ma-Mega Watts ya Umeme jambo ambalo at current technology is not an easy feat...; au tuhakikishe mchana tunatumia solar pekee alafu usiku another option jambo ambalo kwa GRID kucheza na hizo hesabu is not practical...

Ndio maana nikasema whatever we do kwa infrastructure yetu Bwawa linaweza likatumika kama kiungo cha kumfanya kila Mtanzania kuwa Mzalishaji wa Umeme kwenye Paa lake la Nyumba
 
Hii ni fedhea. Haiwezekani karne hii ya 21 tuna wasomi na viongozi tunaoamini wana exposure ila wanaishia kuhubiri umeme wa maji tu. Ni kielelezo kuwa tuna shida kwenye bongo zetu
Upo sahihi...kwa kuongezea, maji yanayoenda Nyerere ndiyo hayo hayo yanapita na vyanzo vingine kule juu: kihansi, kidatu na mtera...chukua ramani na uangalie flow ya ile mito...they depend on each other!

This means kama kukiwa na ukame kama wa last season huko upcountry then all hydro dams zitakuwa affected at varying degrees na kwa hivyo power generation itayumba!

Kwa kweli wasomi wanatufelisha sana na ndiyo sababu Msukuma anahoji kila mara kwamba huko chuo wanasomea ujinga na wizi?
 
Hii ni hoja ya msingi sana,maeneo kama Singida na Dodoma jua linawaka mwaka mzima,lakini tunawaza Nishati za kale ambazo hazina uhakika kwa siku za usoni.
Ila kwenye Nuclear plants hapo Mzee namna ya kutunza bila kuathiri binadamau,maana watumishi wa Shirika letu kwa uzembe hawajambo.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Tulete wazungu waendeshe...sisi hata maji yametushinda kusambaza hatuna uwezo wala umakini wa kusimamia nuclear power plants...elimu ya mzungu haijatusaidia zaidi ya kuzalisha wezi na wajinga kama anavyosema Msukuma kule mjengoni!
 
Issue ni energy mix solar ni percent ngapi ya wanachozalisha ? Umeme tuseme ni kama maji yanatoka kwenye mpira kwahio yakitoka ni either unayatumia kwa wakati huo (kuoga au kumwagilizia) au kuyatunza kwenye ndoo.., Sasa issue ni hapo kwenye utunzani (kama tukirely percent kubwa kwenye solar na upepo inamaanisha tuwe na ndoo za kutosha za kutunza ili usiku wakati hakuna jua tuweze kutumia ule tuliotengeneza mchana... Battery za Lithium ni expensive ingawa ni efficient; kwa watu kuona hilo ndio maana sasa hivi watu wanaangalia option nyingine za battery hio mfano mechanical (kunyanyua vitu vizito au cranes kwenye mashimo ya caves na old mines wakati wa jua linawaka au umeme unatengenezwa ili kutunza umeme huo) hii ni very inefficient..., au storage kwenye hydrogen cells (storage hydrogen bado not as efficient) au kwa kutumia new materials carbon graphene (hii bado ipo kwenye uchunguzi ingawa ni promising)

Kwahio the most efficient large scale battery to date ni HEP (Hydro Electric Power Plants) kama Bwawa la Nyerere.., Umeme wa jua ukizalishwa mchana au upepo ukivuma unawekwa kwenye Grid na offpeak times unatumika kupump maji kutoka reservoir ya chini na kuyarudisha juu ili ikifika usiku au peak time same maji yanaachiwa tena ili kuzalisha umeme...

Bila hivyo huenda tukahitaji kununua Battery za kuweza kuhifadhi ma-Mega Watts ya Umeme jambo ambalo at current technology is not an easy feat...; au tuhakikishe mchana tunatumia solar pekee alafu usiku another option jambo ambalo kwa GRID kucheza na hizo hesabu is not practical...

Ndio maana nikasema whatever we do kwa infrastructure yetu Bwawa linaweza likatumika kama kiungo cha kumfanya kila Mtanzania kuwa Mzalishaji wa Umeme kwenye Paa lake la Nyumba
Hapo umeeleweka.

Swali langu. Hizi challenges mbona hatuzioni kwenye nchi zinazotegemea umeme wa Jua? Mbona kwa sasa Solar energy ndo inaonekana inakimbiliwa sana? Hata uzallishaji wa panels umeongezeka mara dufu Mf. China?
 
Tatizo letu kwenye suala la umeme kama nchi wala sio upungufu wa umeme bali uongozi unaosimamia taasisi husika, wafanyabiashara wahuni pamoja na wanasiasa wasio wazalendo.
Hapana. Tuna upungufu wa umeme. Nimepita njia ya mtera mara kadhaa miezi 3 mfululizo. Ukipita unaona kabisa hapa kuna shida bila hata kuambiwa.

Sehemu ya pili ya mto unaona uzalishaji hauendelei na sehemu ya bwawa unaona kabisa kina kimepungua sana.
 
Upo sahihi...kwa kuongezea, maji yanayoenda Nyerere ndiyo hayo hayo yanapita na vyanzo vingine kule juu: kihansi, kidatu na mtera...chukua ramani na uangalie flow ya ile mito...they depend on each other!

This means kama kukiwa na ukame kama wa last season huko upcountry then all hydro dams zitakuwa affected at varying degrees na kwa hivyo power generation itayumba!

Kwa kweli wasomi wanatufelisha sana na ndiyo sababu Msukuma anahoji kila mara kwamba huko chuo wanasomea ujinga na wizi?
Ndo mana nasema in the long run, lile bwawa halitakuwa na efficiency tunayoitegemea au kuaminishwa.
 
Tulete wazungu waendeshe...sisi hata maji yametushinda kusambaza hatuna uwezo wala umakini wa kusimamia nuclear power plants...elimu ya mzungu haijatusaidia zaidi ya kuzalisha wezi na wajinga kama anavyosema Msukuma kule mjengoni!
Wasomi wetu wanatuangushaga sana. Ila kubwa zaidi wanasiasa wetu.
 
Hapo umeeleweka.

Swali langu. Hizi challenges mbona hatuzioni kwenye nchi zinazotegemea umeme wa Jua? Mbona kwa sasa Solar energy ndo inaonekana inakimbiliwa sana? Hata uzallishaji wa panels umeongezeka mara dufu Mf. China?
Solar kwa mtu mmoja mmoja ni rahisi na ndio ina ufanisi zaidi..., unafunga kwako unaweka kwenye battery yako ndogo unatumia kwenye matumizi yako au sehemu zenye smart meter mfano USA not sure kuhusu UK hata bila battery unazirudisha kwenye mita unapewa credit yaani kama umewapa units kumi kwahio unawadai units kumi siku jua halijawaka au umetumia umeme kidogo.....

Biggest Solar farms yaani mithili ya Grid changamoto yake moja ni unreliability kwahio itahitaji kuwa na means nyingine sambamba ili kuweza kufanya kazi wakati hizo hazifanyi production.....

Mbili kwa kutumia ardhi ambayo huenda ingetumika kwa mambo mengine kuweka solar huenda pia isiwe busara (ndio maana suggestion yangu ni kuweka kwenye mapaa ya watu na sio kutumia ardhi ambayo tungelima mchicha na kuweka solar)..., Ingawa storage ingekuwa rahisi huenda panels zingewekwa huko kwenye ma-desert..;

Pia Solar imekuwa kwa kasi sababu bei ya panels imeshuka sana (lakini ushukaji huo haujaenda sambamba na battery) pia kumbuka panels zina lifespan baada ya kufeli muda wake tutakuwa tunahitaji replacement ambayo nayo lazima tuiweke kwenye equation..., na mpaka leo lithium batteries ambazo ni efficient na zina energy density kubwa matumizi yake yameongezeka sana (kumbuka uchimbaji wa hii kitu pia umeongezeka na hii kitu sio renewable itafika wakati itakwisha), lakini huenda by the time imekwisha tukawa na storage nyingine; Au kwa our case we don't even need it because we have Julius Nyerere HEP ambayo tunaweza kuitumia kama Battery ya Solar na Wind (Ila kama nilivyosema hapo awali watawala wanajali percent watakazokula kwahio jambo rahisi kama hili hawawezi kulifanya) watataka projects kubwa kubwa zenye ulaji kwao...
 
Ushauri wangu.
1. Kuna teknolojia mpya salama zaidi ya kutengeneza plant ndogo za nyuklia. Serikali ialike wataalam kutoka nchi za Ujerumani au Scandinavia wajenge hata plant moja ya namna hiyo kwenye moja ya mikoa yenye bahari/ maziwa hapa Tanzania. Tukipata megawat hata 10,000 au 20,000 sio mbaya. Uzuri madini ya uranium tunayo kinachotakiwa ni teknolojia tu.

Naomba kuwasilisha.
Umeme wa Nucler plant ni umeme wenye teknolojia ya juu sana na umakini kuliko kitu chochote kwa sababu ikitokea tatizo basi madhara yake ni makubwa.

Umeme huu hutengenezwa na uranium ya isotope -235 na husabisha joto ambalo kuzimika kwake huchukua mda mrefu kutokana na radiation zisizo pungua wakataki wa uchavushaji joto.

Gram 1 ya uranium ni sawa na makaa ya mawe yenye uzito wa kilo 2,500kg.
kama tutakuwa na kilo moja uranium ina weza kuzalisha umeme sawa kwh 2,500,000,000 bila kuzima.

Tatizo linakuja kushindwa kuwa na mfumo huu :

1. Ufinyu wa wataalamu na umakini
-Bado nchini kwetu tuna sababu ya kutoweka kwa sababu idadi ya watalaamu ni ndogo au hakuna kabisa kuendesha na pia umakini kuepuka kulipuka au kuungua.

2. Usalama na matumizi mbadala
-Uchavushaji wa uranium wa kuzalisha umeme hupelekea watu kutumia vibaya na ndio maana hupelekea kutengeneza silaha

3. Hatari ya Nuclear plant
kama mtakumbuka Ukraine 26 April 1986 chernobyl kilivyolipuka na kusababisha mji mzima kuondolewa na kubaki kama pori.

Sasa tulivyo kuwa na sifa utakuta tumekiweka Ubungo pale au Tabata Kinyerezi ikatokea kama hii.
wote Dar es Salaam tunahama na kukuacha kama kulivo.

4. Umoja wa nguvu za atomic kwenye siasa na usalama
-Umoja huu huogopa au kukataza watu kufanya mifumo hii kwa nchi zinazotaka kujaribu kuhofia zinaweza kujiingiza kwenye mambo haya.

Elimu ya Nuclear ni nzuri kama ukielewa na ina faida kubwa kwenye swala maendeleo ya nishati ya umeme
 
Hii ni fedhea. Haiwezekani karne hii ya 21 tuna wasomi na viongozi tunaoamini wana exposure ila wanaishia kuhubiri umeme wa maji tu. Ni kielelezo kuwa tuna shida kwenye bongo zetu
Nani amesema kwamba umeme wetu uwe WA maji Tu. Na zaidi ya hapo ukizungumzia ukame kama kizuizi siku zijazo, China wasinge Jenga the three gorges .
Uzalishaji wa umeme kwa Tanzania utatokana na uzalishaji tofauti tofauti, lakini Kwa sasa ni Maji, pili ni gesi, ndio tuangalie upungufa wa baadae ujazwe Kwa uzalishaji upi, kama upepo, jua, uraniam au gas n.k
 
Kwenye mihimili mitatu Bunge, serikari na Jeshi tuongezwe mhumili wa nne Food and Energy . Maana ilivyo sasa tunaenda kisiasa na biashara hatujawahi ona nishati na chakula kama janga
 
Hapo umeeleweka.

Swali langu. Hizi challenges mbona hatuzioni kwenye nchi zinazotegemea umeme wa Jua? Mbona kwa sasa Solar energy ndo inaonekana inakimbiliwa sana? Hata uzallishaji wa panels umeongezeka mara dufu Mf. China?
Na wanatengeneza solar farms za uhakika.
 
Kuna watu wanaamini kabisa kuwa Bwawa la Umeme la Rufiji likianza kazi basi suala la Mgao wa umeme litakuwa historia kwenye nchi hii.

Kwa namna ninavyosoma taarifa mbalimbali za kiutafiti zinazohusu masuala ya Mazingira napenda kuwaambia hawa watu wakiwemo viongozi wetu kuwa inawezekana wakawa sahihi kwa muda fulani ila kwa muda mrefu hawatakuwa sahihi

Kwa hali ya mabadiliko ya hali ya hewa ilivyo inasemwa kuwa huko mbeleni suala la ukame litakuwa jambo la kawaida sana duniani na inawezekana hata uzalishaji wa chakula ukapungua sana.

Kwa haya ni sahihi kusema kuwa hata Bwawa la Nyerere inawezekana lisiwe efficient kwa miaka mingi ijayo kutokana na changamoto hizi.

Kwa upande mwingine kuna vyanzo ya umeme vinavyoonekana kuwa vya uhakika zaidi katika miaka mingi ijayo. Vyanzo hivyo ni pamoja na Nyuklia na Jua ambavyo kwa bahati nzuri sana vyote kwa hapa Tanzania tunavyo.

Ushauri wangu.
1. Kuna teknolojia mpya salama zaidi ya kutengeneza plant ndogo za nyuklia. Serikali ialike wataalam kutoka nchi za Ujerumani au Scandinavia wajenge hata plant moja ya namna hiyo kwenye moja ya mikoa yenye bahari/ maziwa hapa Tanzania. Tukipata megawat hata 10,000 au 20,000 sio mbaya. Uzuri madini ya uranium tunayo kinachotakiwa ni teknolojia tu.

2. Kuna mikoa/ sehemu hapa nchini ambayo Jua linawaka kwa uhakika kwa miezi si chini ya 10 au 11. Serikali iwekeze haraka uzalishaji wa Umeme Jua kwenye mikoa hii hata megawat 3000 - 5000

Inawezekana watu wakasema tuna gesi ila kiuhalisia gesi tuliyonayo ni ya matumizi ya miaka 30- 50 kama sikosei hivyo inawezekana huko mbeleni nayo ikaisha.

Naomba kuwasilisha.
heko sana kiongozi ama hakika ada za wazazi wako katika shule na chuo kikuu hazijaenda bure kwani umezitendea haki kwa maelezo yako haya yenye madini makubwa na elimu toshelezi kwa sisi wasomaji wako
 
Bila hivyo huenda tukahitaji kununua Battery za kuweza kuhifadhi ma-Mega Watts ya Umeme jambo ambalo at current technology is not an easy feat...; au tuhakikishe mchana tunatumia solar pekee alafu usiku another option jambo ambalo kwa GRID kucheza na hizo hesabu is not practical...
Bado uko nyuma kuhusu teknolojia ya solar (UV tech)

Imeboreshwa sana mkuu

Nchi za wenzetu hadi umeme wa solar umeingizwa kwenye grid ya taifa
 
Back
Top Bottom