Bidhaa za Uturuki Diamond Jubilee: Leo bei karibu na bure, kesho bure!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi, kuna msemo wa Kiswahili usemao, " kizuri kula na nduguzo", hivyo nimeikuta hii imekaa vizuri, nikaona nilete tule na wana JF.

Kuna maonyesho ya bidhaa mbalimbali yanayoendelea kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Hall tangu juzi, na yanatarajiwa kuisha kesho.

Jambo zuri nililolishuhudia kwenye bidhaa hizi za Uturuki ni kiwango cha ubora wa hali ya juu ukilinganisha na bidhaa za kutoka China zilizofurika maduka yetu.

Wale wenye nafasi, sio vibaya ikipita tuu na kujionea, ila nimedokezwa leo bei zimepoozwa karibu na bure na kesho kuna uwezekano baadhi ya bidhaa hizo zikagawiwa bure kabisa.

Dokezo hilo limefuatia Waturuki hao kuja kuonyesha bidhaa nyingi zenye ubora wa hali ya juu kwa viwango cha nchi za Ulaya, kwa matumaini ya kutosheleza kiu la soko la Tanzania kwa upande wa quality products, wamepigwa butaa kukuta Watanzania wameshaleweshwa na bidhaa za China sio kwa sababu ya poor quality, bali kwa sababu ni za bei chee, hivyo Waturuki kujikuta lazima hizo bidhaa zao, nao waziuze kwa bei chee.

Maonyesho hayo, yatamalizika kesho hivyo kupelekea baadhi ya bidhaa kugaiwa bure kutokana na gharama za kuzisafirisha kuzirudisha Uturuki ni kubwa kuliko kuzitelekeza hapa nchini.
Aina ya bidhaa hizo iko kwe attachment.
Asanteni
 

Attachments

  • Maonyesho ya Bidhaa za Uturuki.pdf
    402.4 KB · Views: 145
Nimekwenda jioni leo kwenye saa 11 na nusu. Nimeona vitu kadhaa wanauza whole sale na sio rejareja. Kati ya nilivyoona vinauzwa rejareja ni music systems za gari, decoders etc., asali, na mashati na suti. System ya gari yenye screen ya TV niliuliza bei ni $650. Mashati yalikuwa yanauzwa ya ubora wa 100% cotton. Bei ni Tshs.elfu 30 au $20 - saizi za XXL zilikuwa chache sana. Kwa kweli nilinunua mashati kadhaa. Mabanda mengine niliona hayani kitu nadhani ni dalili muda umefika ukingoni. Mengine niliyoona ni majani ya kijani ya bandia, samani za plastiki, sweets n.k.
 
Nimekwenda jioni leo kwenye saa 11 na nusu. Nimeona vitu kadhaa wanauza whole sale na sio rejareja. Kati ya nilivyoona vinauzwa rejareja ni music systems za gari, decoders etc., asali, na mashati na suti. System ya gari yenye screen ya TV niliuliza bei ni $650. Mashati yalikuwa yanauzwa ya ubora wa 100% cotton. Bei ni Tshs.elfu 30 au $20 - saizi za XXL zilikuwa chache sana. Kwa kweli nilinunua mashati kadhaa. Mabanda mengine niliona hayani kitu nadhani ni dalili muda umefika ukingoni. Mengine niliyoona ni majani ya kijani ya bandia, samani za plastiki, sweets n.k.
.

Asante Mubii kwa kwenda, hizo bei zisikutishe, kesho watagawa mpaka bure maana kuzisafirisha kuzirudisha kwao ni more costly kuliko kuziacha hapa Tz.
 
Wacha wagawe bure tu maana hata wao wana kasumba ya kuwa Dar ndo kila kitu. Waende mikoani huko watapata wadau. Kuna Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya bila kusahau Kilimanjaro. Utasikia mdahalo Dar, Maonyesho Dar! Jama kila kitu Dar! Kesho mtaandika Waturuki wagawa bure Dar! Haya tunasubiri taarifa za bure
 
nimekwenda jioni leo kwenye saa 11 na nusu. Nimeona vitu kadhaa wanauza whole sale na sio rejareja. Kati ya nilivyoona vinauzwa rejareja ni music systems za gari, decoders etc., asali, na mashati na suti. System ya gari yenye screen ya tv niliuliza bei ni $650. Mashati yalikuwa yanauzwa ya ubora wa 100% cotton. Bei ni tshs.elfu 30 au $20 - saizi za xxl zilikuwa chache sana. Kwa kweli nilinunua mashati kadhaa. Mabanda mengine niliona hayani kitu nadhani ni dalili muda umefika ukingoni. Mengine niliyoona ni majani ya kijani ya bandia, samani za plastiki, sweets n.k.

umesahau kusema na zile mbu zilizokuwa zikipishana kama ndege zinatoka jiji gan la uturuki??
 
hawa masikini wa ulaya nao wanaleta nini hapa, waondoke zao tu hapa. european union haiwataki, waarabu nao hawawataki...kisa, dini ya msalime mtume...
 
Back
Top Bottom