Karibu Dar es Salaam, njoo uyashuhudie

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
JIJI linaitwa Dar es Salaam. Rapa wa Kimasai, marehemu Abel loshilaa Motika ‘Mr Ebo’ anaita Saridalama. Wenye mikogo wanatamka Das’lam. Watu na vifupisho, kuokoa nguvu na muda wanaita Dar.

Jiji linaitwa Bongo, kwamba ukiishi ndani yake lazima ubongo wako uchangamke. Sifa za jiji ni kubwa mno. Ukizaliwa mikoani katika maisha yetu pangu pakavu tia mchuzi, kufika Dar ni matamanio makubwa. Kukanyaga Bongo ni ndoto kugeuka kweli.

Jiji zamani liliitwa Mzizima kabla ya kubadilishwa na kuitwa Dar es Salaam yenye maana ya Bandari Salama. Ni neno sawa na Pwani Salama. Ndipo palipo na Ikulu, viongozi wote wa nchi wanaishi, wafanyabiashara karibu wote wakubwa, wasanii maarufu, warembo wenye kutikisa, makampuni makubwa.

Kimsingi Dar ndiyo mwanzo wa kila kitu katika nchi. Hata makao makuu ya serikali imeshindikana kuhamia Dodoma kwa sababu ya Dar. Viongozi wanaondokaje Dar? Jiji tamu hili.

Marapa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’, kila mmoja alipata kutoa wimbo wa kuelezea sifa za Dar es Salaam. Wa Sugu unaitwa Dar es Salaam na wa Profesa Jay ni Bongo Dar es Salaam.

Karibu Dar, karibu sana. Hata mimi nyakati hizo nilipokuwa naisikia tu, nilitamani kweli kufika. Baba yangu, marehemu Alhaj Swaleh Nyambo aliponiambia likizo ile ningesafiri kuja Dar hakika nilifurahi, hata wanafunzi wenzangu niliwasimulia. Sikumbuki kama kuna ambaye sikumwambia. Hata walimu walijua. Dar tena!

Una ndoto za kuishi Dar es Salaam? Karibu sana, njoo tuongeze msongamano. Mimi siyo kama wale wenye kukataza watu wasije, maana sijui riziki yako ilipo. Pengine wewe ni bilionea unayekuja, na kitovu cha ubilionea wako ni Dar. Hata mimi ningekubali makatazo yao ya “usije mjini”, nisingekuwa Dar, wala nisingekuwa mwandishi niliye leo.

Ukishakaribia Dar utayaona ya Mwanameka. Kabla ya harusi hupendwi, unaonekana upoupo tu. Ukishaoa au kuolewa ndiyo wenye kukupenda wanajitokeza, wanakupa mapenzi ya ghiliba mpaka unachanganyikiwa, ndoa yako ikishavunjika, mchepuko badala ya kufurahia kupata nafasi nzuri ya kujidai, nao unakimbia.

Wanaita Pwani ya Kiranga, kuna watu wenyewe wanachotaka ni mapenzi ya wizi tu. Hawataki kumiliki. Anaiba leo, akishaharibu anakwenda kuiba kwingine. Maisha yake yote ni hivyo. Ukimuuliza mbona haoi au haolewi, jibu lake ni woga wa kuibiwa. Mkuki kwa nguruwe bwana!

Yupo ambaye ni mkali kweli kwa wake au waume wa wenzie. Ila wake hataki aguswe. Ucheke na wa wenzio tu, wenzio wakicheka na wako ni nongwa. Hajui kuwa kuku akitoka lazima arudi bandani.

Dar kuna mseto wa mahaba bwana! Jamaa anaanzisha mapenzi na Mama Lishe (Mama Ntiliye) ili apate uhakika wa chakula cha bure.

Mrembo naye anajigonga kisha anajiweka kwa mwenye kibanda cha chipsi ili awe anakula chipsi, mayai, kuku na soseji za bure.

Dar watu wanajua kulenga. Mpangaji anafanya juu chini mpaka anamgeuza mwenye nyumba mchepuko wake ili asilipe kodi ya pango. Mwingine anampa mapenzi motomoto dereva wa bodaboda ili apate usafiri wa bure. Madereva taksi na bajaji ndiyo usiseme.

Watu na magari barabarani pamoja na mbwembwe za kuajiriwa kwenye maofisi ya maghorofa marefu, hayo wala yasikutishe. Dar wengi wanaishi kibandiabandia. Wa magari na ofisini wala hawana pesa, wamachinga, wauza mbogamboga, madereva bodaboda na bajaji wana vipato vikubwa zaidi.

Mtu anaamka alfajiri kuwahi kazini, anapanda kigari chake, anasubiri mwisho wa mwezi mshahara shilingi milioni moja. Dereva wa bodaboda au bajaji anatengeneza shilingi 100,000 mpaka shilingi 150,000 kwa siku. Hesabu ya mwezi shilingi milioni tatu mpaka nne na nusu. Wanaendana hao?

Mtu anafanya kazi ofisini, analipwa mshahara shilingi 500,000 mpaka 600,000 kwa mwezi. Ajabu ni kuwa kwa mshahara huohuo, mfanyakazi wa ofisini anamuona muuza mbogamboga na mchoma mahindi barabarani ana maisha magumu, wakati anaingiza kwa siku faida ya shilingi 30,000. Hesabu ya mwezi ni shilingi 900,000.

Kichekesho zaidi cha Dar es Salaam ni kuwa mwenye kulipwa mshahara wa shilingi 500,000 akinunua matunda kwenye genge, chenji ikibaki kidogo anamwachia. Wanaita tipu! Wa shilingi 500,000 anamuongezea wa shilingi 900,000.

Dar es Salaam vivutio vya utalii ni vingi, mtu ameajiriwa Mlimani City lakini akitaka chakula anatoka nje kwenda kwa mama ntiliye.

Yaani watu wapishana, wakati wengine wakitoka kwenye maeneo yao kwenda Mlimani City kula, wenye eneo wanakwenda kutafuta chakula nje. Ni mpishano.

Ukiuliza wanaokwenda kula Mlimani City wanafuata nini, jibu ni “misosi mitamu” au “misosi ya Kizungu.” Wengine wanafuata lile jengo, kuwepo pale ni sifa. Mtu yupo Lufungilo, akiulizwa kwenye simu alipo, anajibu Mlimani City.

Waulize pia wafanyakazi wa Mlimani City wanaotoka kwenda kula kwenye migahawa ya nje, jibu lao ni bei. Mishahara midogo kulinganisha na bei za chakula na mahitaji mengine. Nguo na viatu vipo Mlimani City kwa ubora mkubwa lakini mfanyakazi wa hapo anakwenda kufanya manunuzi Mwenge na Kariakoo.

Hali hiyohiyo, ibebe pia kwa maeneo kama Quality Centre, Pugu Mall, City Mall, Dar Free Market na vituo vikubwa vyote vya manunuzi Dar. Ni mfanyakazi lakini vilivyomo ndani yake havimhusu kimatumizi.

Inatokea Dar, mke, mume na watoto wote ombaomba. Kwao hiyo ni fursa. Wanagawana maeneo ya kuomba. Mchana wakikutana kama vile hawajuani. Usiku wakiwa nyumbani hesabu inafanyika. Ombaomba wana maisha mazuri kuliko wanaowasaidia.

Kuna watu Dar es Salaam maisha yao yana matokeo makubwa kuliko vipato vyao. Magari wanayoendesha na maghorofa wanayomiliki. Hata hivyo, hakuna wa kuwauliza fedha wanapata wapi.

Thubutu wewe upate mafao yako kisha ufanye matokeo ya harakaharaka, uone jinsi utakavyoandamwa na vyombo vya ulinzi na usalama, jumlisha maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Dar ndipo hasa kwenye kuonekana tofauti ya maskini na tajiri. Wakati mwizi wa TRA akimnunulia hawara yake Mercedes Benz C Class ya kutembelea na kumjengea nyumba ya ghorofa mbili Goba, mwalimu wa serikali ananyanyasika kwenye nyumba ya kupanga Tandale kwa Bibi Nyau.

Hakuna watu wa uchumi wa kati, ukiwaondoa matajiri, wote wanaobaki ni maskini. Hata hivyo, kundi hili la watu maskini ndilo lenye kelele kuliko, watu wanatambiana, kutishana na kuoneshana umwamba.

Njoo Dar kisha pitiliza maeneo yetu yenye kuitwa Uswahilini ujionee jinsi ambavyo michuano yetu maskini ilivyo. Watu wanashindana kununua TV mpya, wanaoneshana umwamba kwa kufungulia sauti kubwa ya muziki. Mikwara yetu nguo mpya. Wanasahau kuchanga karata za kuondoka kwenye lindi la umaskini, wao wanajikita kwenye mashindano ya kuimbiana Taarabu!

Nikujulishe mapema, Dar haina wabunifu. Ukija na wazo lako la kufungua duka la kuuza kucha za kuku, miezi mitatu mingi, katika huohuo mtaa wako kutakuwa na maduka arobaini ya biashara hiyohiyo. Nao wanauza kucha za kuku! Dar watu wanaishi kwa kutegemea vichwa vya wenzao.

Dar ya kamari. Siku hizi limeibuka la kubahatisha matokeo ya mpira basi kila kona ni kubeti. Ni kama ambavyo watu walivyovamia biashara ya maduka ya nguo. Tena asikwambie mtu, anayeiga anaweza kufanikiwa kuliko mwasisi.

Siku hizi hatupumui na dawa za kupunguza unene. Wataalamu wamekuwa wengi kwenye mitandao ya kijamii. Mara dawa kutoka China. Siku akifa mtu ndiyo tutasikia makatazo ya kutotumia dawa za kupunguza unene ambazo hazina TBS, lakini sasa hivi kimya kimetanda. Watu wanendelea kutengeneza pesa kienyeji.

Ndani ya Dar, mbunifu wa dawa ya asili ya kuongeza makalio atapata utajiri mkubwa. Sijui watu huwa wanatafuta nini? Makalio makubwa, hipsi pana! Eti awe na mvuto, mwisho ni kutaka tu kuvutia wanaume. Achana na Dar, siku hizi mpaka mashoga wanatumia dawa za kukuza makalio na hipsi.

Wanasema Dar njoo na akili tu, tabia utazikuta hukuhuku. Jiji limejaa watu wachafu kupata kuona. Mvua inyeshe, jiji zima linanuka kinyesi. Magari ya kufyoza maji taka yapo lakini wanaona gharama, mvua ikinyesha kidogo tu chemba zinafunguliwa.

Hujiulizi kwa nini Dar ndiyo kiongozi wa kila kitu? Ukahaba, ushoga, uvivu, utapeli, majungu, ufisadi, uchawi, ulevi, foleni na mengine mengi ya ajabu, ila utafanya kosa kubwa kama utasahau kuhusu kipindupindu na utitiri wa waganga wa kienyeji.

Ukiwa mganga wa kienyeji Dar unakuwa na nguvu kubwa. Viongozi wa kitaifa watakuheshimu na kuja kukupigia magoti utafikiri wewe ni Mungu. Mganga wa kienyeji anaaminika kuwa anatoa vyeo, anampa mtu pesa, anampa mtu nguvu za kiume, anampa mtu mume, anatuliza nyumba isiyumbe, anamfanya mlevi aache pombe. Kama unaijua mizizi japo miwili, njoo Dar soko ni rahisi mno.

Watu wengi Dar wanaamini fedha za kulala na kuamka tajiri zinapatikana. Ukifika Dar jitangaze wewe ni Freemason na unagawa pesa. Weka wazi namba zako za simu. Mwenyewe utatamani kuzima simu jinsi utakavyosumbuliwa. Na pesa utawalia.

Wapo waganga wa kienyeji matapeli na wanajulikana. Ni matajiri hasa, utajiri wao unamaanisha kuumizwa na kufilisiwa wengine walioamini wangefanikiwa kupitia mganga. Wanaendelea kuwepo. Ila kuwa makini, ukijifanya kama wao ukaingia kichwakichwa utafungwa, wenzako wana mitandao. Humuoni Manyaunyau yupo jela?

Najua una hamu ya kuja Dar, karibu sana ila ukifika, ukiona watu wanafanya mazoezi usiku au alfajiri, jifiche, wengi ni vibaka, watakupora kila kitu. Ukiwa pembezoni mwa barabara na ukaona pikipiki inakukaribia, shtuka mapema, ni vibaka hao.

Ukiwa Dar ndani ya gari dirishani unachati na simu ama unaongea kwenye foleni au eneo ambalo barabara ni mbovu, moja kwa moja vibaka hupiga mahesabu ya sehemu ya kukimbilia baada ya kukupora, maana tayari wanahesabu simu yako ni mali yao. Vibaka wa Dar wana mikono myepesi utadhani mshale wa sekunde.

Unaijua Mahakama ya Simu wewe? Eneo linaitwa Tandale Kwamtogole. Wapo vijana wanajua kupora simu utadhani walisoma kozi maalum. Wanaweza kuiba simu kwenye gari lililo kwenye mwendo. Funga milango sawasawa, tia loki, vibaka wa Kwamtogole hawajawahi kuwa watu wema kwa wamiliki wa simu.

Ni Dar ya fursa. Matapeli wapo ‘bize’ kama mtu mwenye kazi nyingi za kiofisi. Wapo watu wanapelekwa mpaka Ikulu, wanaoneshwa mlango wa rais, baada ya hapo wanatapeliwa kwa jina la mkuu wa nchi. Usiulize kuhusu muhuri wa Ikulu au saini ya rais, hayo ni mambo madogo mno kwa watoto wa mjini.

Fika Dar kisha nunua kiwanja na nyaraka zote uwe nazo, kesho nenda kaulizie kiwanja, utapelekwa kwenye kilekile kiwanja chako. Utaoneshwa mmiliki mwingine ambaye yupo tayari kwa biashara. Umeshaambiwa njoo Dar na akili yako, maana ndiyo itakayokuongoza kuishinda mikikimikiki ya jiji.

Dar zipo dakika 60 za ajabu mno, zinabadili kabisa mandhari ya jiji. Ndiyo, ni dakika 60, yaani saa moja tu. Amka saa 10 usiku, tembea barabarani maeneo mengi utajiona peke yako. Endesha gari, utajikuta wewe pekee ndiye unaitawala barabara utakavyo.

Ingia barabarani saa 11 alfajiri uone, tayari foleni za magari kila mahali. Ni dakika 60 tu lakini tofauti yake ni kubwa. Sijui watu wa Dar huwa wanaambiana kitu gani kuhusu saa 11.

Barabarani nako kila mtu mbabe. Ukiwa dereva Dar lazima ujue kutukana. Barabarani Dar hakuna mnyonge, watu wanaweza kusababisha foleni kwa kubishana tu. Shida ni kuwa hakuna mtu mvumilivu wala wa kukubali kushindwa.

Mtu anaendesha gari akiongea na simu matokeo yake anasababisha foleni. Gari lingine linatembea kama kinyonga, kumbe ndani ni wapenzi wapo kwenye mapenzi yao. Foleni za Jiji la Dar zinasababishwa na mambo mengi.

Kama utafanikiwa kumiliki gari au hata ukitumia la kazini au la ndugu, usiku usikimbize sana. Malori na magari ya kuzoa taka yanaharibika hovyo barabarani na yakiwa kwenye mwendo hutembea taratibu mno. Huwezi kuliona mbele yako maana huwa hayana alama yoyote, hayana taa wala ‘riflekta’. Ajali nyingi za usiku ni magari madogo kuyavamia malori.

Yote hayo yanatokea kwa sababu barabarani hakuna taa. Mwanga pekee ni wa taa za gari. Na ukiwa Barabara za Kawawa na Mandela ongeza umakini usiku. Mandela malori, Kawawa magari ya taka. Ajali nje-nje. Barabara za Ali Hassan Mwinyi, Nyerere, Bibi Titi na Sam Nujoma, zina upendeleo. Taa za kuangazia barabarani zipo.

Ndani ya Dar, unaweza kudhani mwalimu wa madereva wa bodaboda ni memba wa Al Qaeda au Isis. Uendeshaji wao ni wa kujitoa mhanga. Analiona gari lipo kasi, analikimbiza, analichomekea kwa mbele halafu anakata kona. Ukiwa na roho ndogo, ukipanda bodaboda Dar, unaweza kuzimia au pengine kufa bila kugongwa kwa mshtuko wa matendo ya dereva.

Magari ya Mwendo Kasi yapo Dar na yalipoanzishwa ukaibuka upinzani wa jadi mwingine mjini. Achana na Simba dhidi ya Yanga, Ali Kiba dhidi ya Diamond Platnumz, Manji dhidi ya Mengi, uhasama mkubwa uliopo kwa sasa ni kati ya madereva wa mabasi ya mwendo kasi dhidi ya bodaboda.

Tangu mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi uzinduliwe rasmi, vifo vya waendesha bodaboda vimeharakishwa zaidi. Barabara za mabasi hayo ndizo zinazotumiwa na bodaboda, ni tabu juu ya shida.

Huwezi kuliona Dar ni jiji la matukio kama hushangazwi na ajali za magari mengine dhidi ya Mabasi ya Mwendo Kasi. Magari hayo yana njia zake, sasa ajali inatokea vipi? Watu wabishi Dar, unakuta katikati ya mabasi ya mwendo kasi kuna gari la kawaida na wala dereva hana wasiwasi. Anajiona anazo haki zote.

Watu wengi Dar ni ‘jobless’. Usione msongamano Kariakoo ukadhani watu wapo ‘bize’, wengine wanakwenda kupoteza muda na kuangalia vya kuokota. Ukitaka kutambua hilo, ona jinsi tangazo la mabasi ya mwendo kasi, lilipoeleza usafiri ni bure. Watu kutwa nzima waling’ang’ania magari, vituo vikajaa. Kariakoo watu walipungua. Vibaka wote walihamia kwenye magari ya mwendo kasi.

Dar ndiyo jiji la watu wenye kuamini vitu vya kufikirika kwa haraka. Anzisha tu uzushi wako kuwa kuna mtu alikuwa anatembea Kariakoo, kikatokea kiumbe cha ajabu kikamkwapua na kupaa naye mawinguni. Stori itaenea hiyo na vyombo vya habari vitaripoti huo uvumi.

Usibishe, ilishatokea habari ya mwanamke kuota manyoya kwenye mkono baada ya kumpa pesa ombaomba, Selander Bridge. Eti baada ya muda yule mwanamke aliyeota manyoya alianza kulia mkono wake kisha naye akatoweka na gari nalo likatoweka. Watu wakaamini, vyombo vya habari vikaripoti. Dar usiichezee!

Dar watu wapo bize sana lakini ubize wao ni ngono. Na kama ingekuwa ni amri yao, wasingekuwa wanafanya kazi. Maofisini utoro na ruhusa nyingi lakini wakipata pesa ni pombe na ngono zembe. Mishahara ikishalipwa tu watu hawaonekani kazini. Baa na nyumba za kulala wageni zinajaa. Akili za watu wa Dar zinawatoshaa wenyewe!

Vituko vya Dar, kwa kawaida mvua ikinyesha ni ishara ya neema, mashambani mazao yatastawi, hivyo kuleta matokeo mazuri kipindi cha mavuno. Kwa Dar mvua ikinyesha tu nyumba za kulala wageni zinajaa. Watu wanakwenda kujifungia vyumbani kupeana joto nyakati za baridi. Usiseme Dar imelaaniwa!

Wapo watu kuingia gesti ni lazima kuliko kula. Yupo radhi akope pesa au aende gesti akatumie chumba kwa mkopo. Hata kondomu wanakopa. Anayefanya yote hayo, nyumbani kwake ana mke ambaye hajagoma kumhudumia. Akili za baadhi ya watu wa Dar ni kama zimeliwa na mchwa!

Ni Dar ambako kiongozi wa kanisa anatuhumiwa kupora mke wa mtu na kudhulumu mali za mume, kisha kesi inafika mahakamani, mwingine ananyooshewa kidole kumjaza mimba mke wa mtu, lakini Jumapili inayofuata makanisa ya viongozi hao yanajaa kuliko mwanzo. Vivutio vya utalii ni vingi Dar.

Shehe naye anafumaniwa na kibinti kidogo, anafungishwa ndoa ya mkeka, asubuhi anaamkia Msikitini, anapita mbele anasalisha kisha anatoa mawaidha ya kuonya kuhusu zinaa. Ni hapo ndipo unaambiwa achana na matendo, zingatia maneno.

Dar kila kitu kina upambe. Wapo wapambe wa biashara, wapo pia wa wanawake. Yupo mtu Dar kazi yake ni kutafuta wanawake wazuri ili akamshawishi tajiri fulani wapate pesa. Utakuta mtu yupo ‘bize’ kutafuta warembo utadhani anaandaa shindano la mamisi, kumbe anahangaikia ugali wake. Kazi za watu wengine Dar, hata kujitambulisha wanafanya kazi gani wanaona aibu.

Ukishaingia Dar, ukiwa na pesa wapambe watakufikia tu. Wao wakijua tu pesa ipo lazima waje. Watakuchunguza kitu unachopendelea na baada ya kukuelewa mahitaji yako, utategwa mpaka utaingia.

Ukija Dar sitaki maswali ya kijinga. Usije kuniuliza mzee wangu Reginald Mengi alimpataje Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lynn’.

Tutagombana ukinihoji ni kwa nini Wema Sepetu anaonekana anaishi maisha bei mbaya mjini wakati mapato yake hayaakisi chochote katika matumizi yake.

Ukitaka nikukatie simu na siku nyingine ukinipigia nisipokee, basi uniulize ni kwa nini viongozi serikalini wanawatolea udenda wasanii wa kike Bongo Movie na kwa nini kila mmoja hujifanya yupo nao karibu ili awasaidie, wakati watu wengi tu wenye uhitaji mkubwa hawasaidiwi. Ni kawaida yangu tangu kitambo kwamba huwa sipendi maswali chonganishi.

Usirogwe kuniuliza ni kwa nini warembo maarufu siku hizi wanakuwa na uswahiba na mashoga. Yaani kumkuta Kajala au Jokate na shoga ni kitu cha kawaida. Usiniulize kwa nini kwa sababu sitaki tu kuingilia maisha ya watu. Na ukisema kuwa mashoga hao wana kazi maalum kwa warembo hao, sitajibu kitu.

Warembo wengi Dar wamechoshwa na wanaume, wanasema ni pasua kichwa, wamevamia fani ya usagaji. Mwanamke na mwanamke wanavyobembelezana na kuoneana wivu ni shida! Kama huko ulipo hayajafika njoo Dar uyashuhudie.

Ukifika Dar kama ukitaka kumbi za starehe zenye kuonesha shoo za wanawake wakiwa watupu, zipo. Na zina leseni. Maonesho ya ngono pia yapo. Labda tu kama wewe hujui maeneo.

Ukitaka kumbi za starehe Dar zimejaa. Utapata kila burudani uitakayo. Unafahamu balaa la vituo vya massage wewe? Ukifika sikushauri uende, vinginevyo utakuwa kila mara mtaji unakata kwa massage. Ndiyo ni massage na wengi wao siyo massage tu, ni massage timilifu.

Dar ya vurugu mechi, vigogo wanachepuka na mabinti wadogo, wake zao nao wanajidai na vijana wadogo. Hakuna kazi ngumu kwa mtoto wa kiume kama kuwapaka wanawake rangi za kucha na kuwachua miguu yao. Siku ukiambiwa ukamkande miguu nyumbani kwake jiandae tu. Usisahau kuhusu uwepo wa maradhi. Kumbuka pia mwenye mali akikukuta ni kiyama chako.

Akina dada nguo zimekuwa nzito, hawataki kuvaa. Viguo vifupi vyenye kubana. Mavazi ya kuonesha maungo ya faragha. Mwanafunzi anavyovaa hana tofauti na changudoa anayejipanga barabarani.

Machangudoa Dar ni zaidi ya unaowajua. Wapo wanawake maofisini wanafanya mapenzi kwa pesa. Askari polisi, wanajeshi, viongozi mbalimbali na kada nyinginezo. Wapo pia wake za watu, makundi yote hayo yanafanya mapenzi kwa pesa. Ni kujiuza tu!

Hii ndiyo Dar, mke wa mtu anatoka na gari nyumbani kwake, anafika analipaki Dar Free Market, kisha anapanda gari la mchepuko, wanakwenda kufanya yao. Mtu akiliona gari pale, anaamini yupo ndani kwenye manunuzi. Baada ya kazi anarudishwa palepale, anachukua gari lake, anaendesha kurudi nyumbani. Dar kwa ubunifu wa ngono watu wamefuzu.

Karibu sana Dar, uje uone Bismini, yaani ule Mnara wa Askari ambao kama yule mbunge wetu atakuwa rais siku zijazo, basi utageuzwa kuwa Sanamu la Diamond Platnumz.

Ndimi Luqman MALOTO
 
JIJI linaitwa Dar es Salaam. Rapa wa Kimasai, marehemu Abel loshilaa Motika ‘Mr Ebo’ anaita Saridalama. Wenye mikogo wanatamka Das’lam. Watu na vifupisho, kuokoa nguvu na muda wanaita Dar.
Jiji linaitwa Bongo, kwamba ukiishi ndani yake lazima ubongo wako uchangamke. Sifa za jiji ni kubwa mno. Ukizaliwa mikoani katika maisha yetu pangu pakavu tia mchuzi, kufika Dar ni matamanio makubwa. Kukanyaga Bongo ni ndoto kugeuka kweli.
Jiji zamani liliitwa Mzizima kabla ya kubadilishwa na kuitwa Dar es Salaam yenye maana ya Bandari Salama. Ni neno sawa na Pwani Salama. Ndipo palipo na Ikulu, viongozi wote wa nchi wanaishi, wafanyabiashara karibu wote wakubwa, wasanii maarufu, warembo wenye kutikisa, makampuni makubwa.
Kimsingi Dar ndiyo mwanzo wa kila kitu katika nchi. Hata makao makuu ya serikali imeshindikana kuhamia Dodoma kwa sababu ya Dar. Viongozi wanaondokaje Dar? Jiji tamu hili.
Marapa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’, kila mmoja alipata kutoa wimbo wa kuelezea sifa za Dar es Salaam. Wa Sugu unaitwa Dar es Salaam na wa Profesa Jay ni Bongo Dar es Salaam.
Karibu Dar, karibu sana. Hata mimi nyakati hizo nilipokuwa naisikia tu, nilitamani kweli kufika. Baba yangu, marehemu Alhaj Swaleh Nyambo aliponiambia likizo ile ningesafiri kuja Dar hakika nilifurahi, hata wanafunzi wenzangu niliwasimulia. Sikumbuki kama kuna ambaye sikumwambia. Hata walimu walijua. Dar tena!
Una ndoto za kuishi Dar es Salaam? Karibu sana, njoo tuongeze msongamano. Mimi siyo kama wale wenye kukataza watu wasije, maana sijui riziki yako ilipo. Pengine wewe ni bilionea unayekuja, na kitovu cha ubilionea wako ni Dar. Hata mimi ningekubali makatazo yao ya “usije mjini”, nisingekuwa Dar, wala nisingekuwa mwandishi niliye leo.
Ukishakaribia Dar utayaona ya Mwanameka. Kabla ya harusi hupendwi, unaonekana upoupo tu. Ukishaoa au kuolewa ndiyo wenye kukupenda wanajitokeza, wanakupa mapenzi ya ghiliba mpaka unachanganyikiwa, ndoa yako ikishavunjika, mchepuko badala ya kufurahia kupata nafasi nzuri ya kujidai, nao unakimbia.
Wanaita Pwani ya Kiranga, kuna watu wenyewe wanachotaka ni mapenzi ya wizi tu. Hawataki kumiliki. Anaiba leo, akishaharibu anakwenda kuiba kwingine. Maisha yake yote ni hivyo. Ukimuuliza mbona haoi au haolewi, jibu lake ni woga wa kuibiwa. Mkuki kwa nguruwe bwana!
Yupo ambaye ni mkali kweli kwa wake au waume wa wenzie. Ila wake hataki aguswe. Ucheke na wa wenzio tu, wenzio wakicheka na wako ni nongwa. Hajui kuwa kuku akitoka lazima arudi bandani.
Dar kuna mseto wa mahaba bwana! Jamaa anaanzisha mapenzi na Mama Lishe (Mama Ntiliye) ili apate uhakika wa chakula cha bure. Mrembo naye anajigonga kisha anajiweka kwa mwenye kibanda cha chipsi ili awe anakula chipsi, mayai, kuku na soseji za bure.
Dar watu wanajua kulenga. Mpangaji anafanya juu chini mpaka anamgeuza mwenye nyumba mchepuko wake ili asilipe kodi ya pango. Mwingine anampa mapenzi motomoto dereva wa bodaboda ili apate usafiri wa bure. Madereva taksi na bajaji ndiyo usiseme.
Watu na magari barabarani pamoja na mbwembwe za kuajiriwa kwenye maofisi ya maghorofa marefu, hayo wala yasikutishe. Dar wengi wanaishi kibandiabandia. Wa magari na ofisini wala hawana pesa, wamachinga, wauza mbogamboga, madereva bodaboda na bajaji wana vipato vikubwa zaidi.
Mtu anaamka alfajiri kuwahi kazini, anapanda kigari chake, anasubiri mwisho wa mwezi mshahara shilingi milioni moja. Dereva wa bodaboda au bajaji anatengeneza shilingi 100,000 mpaka shilingi 150,000 kwa siku. Hesabu ya mwezi shilingi milioni tatu mpaka nne na nusu. Wanaendana hao?
Mtu anafanya kazi ofisini, analipwa mshahara shilingi 500,000 mpaka 600,000 kwa mwezi. Ajabu ni kuwa kwa mshahara huohuo, mfanyakazi wa ofisini anamuona muuza mbogamboga na mchoma mahindi barabarani ana maisha magumu, wakati anaingiza kwa siku faida ya shilingi 30,000. Hesabu ya mwezi ni shilingi 900,000.
Kichekesho zaidi cha Dar es Salaam ni kuwa mwenye kulipwa mshahara wa shilingi 500,000 akinunua matunda kwenye genge, chenji ikibaki kidogo anamwachia. Wanaita tipu! Wa shilingi 500,000 anamuongezea wa shilingi 900,000.
Dar es Salaam vivutio vya utalii ni vingi, mtu ameajiriwa Mlimani City lakini akitaka chakula anatoka nje kwenda kwa mama ntiliye. Yaani watu wapishana, wakati wengine wakitoka kwenye maeneo yao kwenda Mlimani City kula, wenye eneo wanakwenda kutafuta chakula nje. Ni mpishano.

Ukija Dar sitaki maswali ya kijinga. Usije kuniuliza mzee wangu Reginald Mengi alimpataje Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lynn’. Tutagombana ukinihoji ni kwa nini Wema Sepetu anaonekana anaishi maisha bei mbaya mjini wakati mapato yake hayaakisi chochote katika matumizi yake.

hongera mkuu kwa andiko zuri
 
mkuu unaonaje Kama tukatengenezea movie itakuwa poa sana
 
Aisee umenishinda tabia
 
Safi
 
Back
Top Bottom