Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,915
- 30,259
Kiatu...Sheikh Mohamed Said tupe kidogo juu ya Kambona na Bibi Titi ukaribu wao ulikuweje
Katika TANU kulikuwa na wasemaji kwa maana ya wahutubuaji wakubwa
wawili nao walikuwa ni Nyerere na Bi. Titi Mohamed.
Hawa wawili ndiyo walikuwa vinara wa harakati.
Kambona alikuja baadae katika TANU na yeye alikuwa na uwezo mkubwa
pia lakini hakumzidi Bi. Titi katika kukibeba chama.
Kwa kipindi kile cha kudai uhuru Bi. Titi alikuwa juu zaidi aking'ara zaidi ya
Kambona.
Kambona alikuja kuwa juu baada ya uhuru kwani haukupita muda Bi. Titi
na Nyerere wakakuruzana mwaka wa 1963 Nyerere alipoonysha dalili za
kutaka kuifungia East African Muslim Welfare Society (EAMWS).