Biashara za Kitanzania ni za ajabu sana

weka na hiyo picha ya Insta mkuu
Bro Mimi Mpenzi mzuri Sana Teva...hizo design tofauti za Teva huwa kweli zinafika mpaka 250000 TSH na zaidi especially ukipita kwenye maduka ya vitu original kabisa au MTU akuletee toka nje. ...unyayo ukiulaza kwenye OG shoes bro kuna raha take kaka. Kuna sandals za Olukai ukizivaa hata usimame muda mrefu miguu still inarelax wacha kabisa bro.
 

KWa hiyo hauoni tofauti yoyote?

WaTanzania Wengi tunapenda kujaza matakataka ndani kwa Madai ya nimenunua Bei rahisi
 
Ukinunua bidhaa kutoka mataifa haya italy,france na uk utatumia bidhaa hiyo miaka mingi sana bila kuhalibika muachane na bidhaa za china low quality kidogo thailand wanajitahidi ubora na bidhaa bei cheap
 
Yaani nimeona sendozi aina ya Teva inauzwa instagram 250,000! Nimepita huku mtaani nikazikuta kwa mmachinga, mpya kabisa. Nimempa elfu ishirini akapokea kiroho safi maisha yanaendelea!
Picha?
 
Niliona kiatu kikali mno online.

Kuagiza , nilichoka mwenyewe.

Hizo picha wanazopost online sijui wanazifanyaje aisee.
Wafanyabiashara wanapiga picha ya bidhaa ambayo hata hawana ukienda dukani wanakuambia imeisha. Lengo lao ufike dukani hata isipokuwepo iyo ununue nyingine. Siku moja nipo manzese ndani ya daladala inayopitia njia ya sinza naangalia mtandaoni nikaielewa all star moja hivi imepostiwa kwenye page ya vunjabei instagram basi nikashukia dukani kwao pale sinza niiangalie vizuri nikawaonesha wale wahudumu screenshot ya kiatu katika simu nikaletewa kiatu tofauti na kwenye picha nikawaambia sio chenyewe kwanza wakabisha baada ya kuonesha tofauti ya vile viatu kilicholetwa na kwenye picha ndio mmoja wao akaniambia design ya kwenye picha imeisha. Nikashangaa yaani picha imepostiwa ndani ya nusu saa tu na caption inasema new stock halafu sasa hivi zimeisha kimoyo moyo nikajua tu wababaishaji hawa.
 
Ukinunua bidhaa kutoka mataifa haya italy,france na uk utatumia bidhaa hiyo miaka mingi sana bila kuhalibika muachane na bidhaa za china low quality kidogo thailand wanajitahidi ubora na bidhaa bei cheap
mkuu, nothing last forever, ! sisi wenyewe ni wa muda mfupi. sendo laki mbili na nusu? wateja ni mafisadi!!!!


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Back
Top Bottom