Biashara ya Zantel network marketing

hustlehard

New Member
Feb 3, 2015
1
0
Fursa ya Zantel ya kupata kipato cha mwezi hadi TZS 1,000,000 na zaidi kwa kwa mtaji wa TZS 76,500

Zantel wameingia mkataba na distributor wao mkubwa ili bidhaa zao ziuzwe kwenye mfumo wa mtandao.

Ili kujiunga kwenye mtandao, unalipia TZS 76,500 kwenye ofisi za kampuni ambapo utatakiwa kutaja jina lako la kwanza, jina lako la ukoo, namba ya kitambulisho chako, namba yako ya simu na reference number ya mtu anayekuingiza kwenye mtandao.

Ukishalipia unapata vocha ya TZS 10,000 ya Zantel, line ya Zantel, kitabu cha maelezo ya mtandao jinsi unavyofanya kazi na matarajio ya malipo na kadi yenye namba ya siri ya kujiungia pamoja na maelezo ya jinsi ya kujiunga.

Kama una line ya Zantel iliyosajiliwa basi utaitumia hiyo. Vinginevyo utatakiwa kuisajili line mpya utakayopata pale ofisini hivyo itabidi uende pale na photocopy ya kitambulisho chako (Cha kupigia kura au cha uraia au passport au barua ya serikali za mitaa inayokutambulisha wewe) kwa ajili ya kusajilia hiyo line yako mpya.

Baada ya hapo utaingiza vocha ya TZS 10,000 kwenye line yako ya Zantel halafu utaanza kujisajili kwa kubonyeza nyota namba ya siri nyota jina lako la kwanza nyota jina la ukoo nyota namba ya kitambulisho nyota mkoa nyota mwaka wa kuzaliwa nyota namba ya mdhamini wako (nitakupatia mimi) halafu unamalizia kwa kubonyeza alama ya reli kisha unaituma kwenda kwenye namba ambayo utapewa kwenye kadi yako utakayoipata mara baada ya kulipia ada ya kiingilio.

Baada ya kutuma utasubiri kupata message kutoka kampuni inayokufahamisha kwamba umefanikiwa kujiunga. Ndani ya message hiyo kutakuwa na reference namba yako kwa ajili ya kuwaunganisha watu wako ili uweze kupata kipato cha mtandao.

Kila mtu utakayemdhamini kwenye mtandao huu kwa kufuata taratibu hizo hapo juu kupitia reference namba yako basi utapata TZS 10,000 kwa kila mtu atakayejiunga kupitia kwako kwenye kizazi chako cha kwanza. Watu wa kizazi chako cha kwanza nao watawaalika watu ambao watakuwa kwenye kizazi chako cha pili ambapo utapata TZS 4,000 kwa kila mtu atakayejiunga kwenye kizazi chako cha pili. Utapata TZS 2,000 kwa kila mtu atakayejiunga kwenye kuanzia kizazi chako cha tatu mpaka kizazi chako cha tisa. Kizazi cha kumi utapata TZS 4,000 kwa kila mtu atakayejiunga. Malipo yote ya mapato yako yanafanyika kupitia Ezypesa. Kiwango cha juu zaidi kitahamishwa hadi akaunti yako ya benki.

Tuangalie matarajio ya malipo kwa kualika watu watano tu (unaruhusiwa kualika watu wengi uwezavyo) ndani ya mwezi na hao watu watano wakaalika watu watano tu ndani ya mwezi huo huo kwa vizazi vitano tu kwenda chini. Mapato yako ya mwezi huo yatakuwa kama ifuatavyo kwenye mwezi husika:

Team Malipo kwa kichwa Jumla
Kizazi cha 1 watu 5 10,000 50,000
Kizazi cha 2 watu 5X5=25 4,000 100,000
Kizazi cha 3 watu 25XX5=125 2,000 250,000
Kizazi cha 4 watu 125X5= 625 2,000 1,250,000
Kizazi cha 5 watu 625X5=3125 2,000 6,250,000
Jumla kuu kwa mwezi 7,900,000

Malipo haya ya kujiunga ni malipo ya wiki ambayo hulipwa kila Jumatano. Utaweza kuona watu unaowaingiza kwenye mtandao na hela unazopata kupitia ofisi yako ya hewani utakayopata mara baada ya kujiunga ambapo uta login kwa kutumia namba simu yako uliyojiungia (anza na 255 halafu acha zero, weka namba zilizobaki za simu yako) kama username na password itakuwa namba ya siri uliyotumiwa baada ya kupata message ya usajili kutoka Zantel. Kulipwa malipo haya ya wiki, utatuma ujumbe mfupi (kipato) kwenda kwenye namba utakayopewa.

Malipo ya pili ni malipo ya mwezi. Utapata fursa ya kulipwa malipo haya kama utakuwa umenunua vocha ya Zantel isiopungua TZS 10,000 kupitia kampuni katika mwezi husika. Malipo haya hulipwa kutokana na jumla ya manunuzi yako ya vocha za Zantel na manunuzi ya wanachama walioko kwenye mtandao wako kwa vizazi 10 kwenda chini.Kizazi cha kwanza na cha kumi utapata 1% ya manunuzi ya wanachama ndani ya mtandao wako. Kizazi cha pili hadi tisa utapata 0.5% ya manunuzi yao. Utapata kipato hiki kwenye tarehe 10 ya kila mwezi. Kupata malipo haya utatuma ujumbe (kipato) kwenda kwenye namba utakayopewa.

Tuchukulie una watu 10 kwenye kizazi chako cha kwanza ambao wamelipia kiwango cha chini cha TZS 10,000 cha manunuzi ya airtime kwa mwezi ambao nao wana watu 10 chini yao waliolipia hiki kiwango cha TZS 10,000 kwa vizazi vitano tu kwenda chini (Utalipwa mpaka vizazi kumi kwenda chini). Malipo yako ya mwezi yatakuwa kama ifuatavyo:

Team Malipo kwa kichwa Mapato
Kizazi cha 1=10 10,000 1,000
Kizazi cha 2 (10X10)=100 10,000 5,000
Kizazi cha 3 (100X10)=1000 10,000 50,000
Kizazi cha 4 (1000X10)=10000 10,000 500,000
Kizazi cha 5 (10000X10)=100000 10,000 5,000,000
Jumla kuu kwa mwezi 5,556,000

Malipo ya tatu ni malipo utakayoyapata kwa kugawa lines za Zantel bure kwa kuwasajili watu. Haya utayapata ukishawadhamini watu watano kwenye mtandao wako. Utapata 20% ya pesa itakayowekwa kwa mara ya kwanza na mtu uliemsajili. Kiwango hiki cha 20% utakipata kwa mda wa miezi mitatu. Baada ya hapo utakuwa unalipwa kwa kiwango cha 10%.

Malipo ya nne ni zawadi mbalimbali utakazozipata kutegemeana na idadi ya watu kwenye mtandao wako kwa vizazi 10 kwenda chini. Ukifikisha watu 15,000, utapata zawadi ya kiwanja. Watu 25,000 utapata zawadi ya kutembelea mahali patakatifu (Kwa waislamu Makka, kwa Wakristu Izrael), watu 40,000 utapata zawadi ya gari. Watu 70,000 utapata zawadi ya Luxury Car. Watu 120,000 utapata zawadi ya jumba la kifahari.

Vilevile Zantel wana huduma ambapo unalipa TZS 1,500 na kuweza kupiga simu Zantel kwenda Zantel bure kwa mwezi.


Kama upo tayari kujiunga piga namba 0754891344
 
mbona mkuu hyo biashara yako unayoipigia chapuo inahusiana na zantel wakati wewe unatumia line ya voda??????
 
HATA MM SIJAMUELEWA LABDA KUTAKA KUJUA ZAIDI INABIDI TUWAULIZE WENYEWE ZANTEL PALE OFISINI KWAO MANA ISIJEKUWA NI DANGANYA TOTO HII TAPELO YA AINA YAKE :embarrassed1:
mbona mkuu hyo biashara yako unayoipigia chapuo inahusiana na zantel wakati wewe unatumia line ya voda??????
 
Naomba uni PM Kwa maelezo zaidi hii ni kweli kabisa na haina uongo. kwani mie ndo nimeanza kuifanya
 
Back
Top Bottom