Biashara ya vipuri vya pikipiki: Ushauri, michango, mawazo

Sidhani kama Mtaji wa milioni moja utatosha,labda nikuulize hapo ume include kodi ya pango,kumlipa muuzaji etc.Nikupe mfano tairi ya pikipiki size ya san lg kubwa moja ni 50000 jiulize na spea zingine itakua bei gani?

Kaa chini survey uone vifaa gani vinahitajika sana kwa watumiaji ambapo unaenda kufungua duka,andika list yake na bei za manunuzi.

tazama faida ya kila kifaa angalia makadirio ya mauzo ghafi na baadae faida halisi utakayopata ukikamilisha hayo angalia kamtaji kako kama kanatosha.Ili uweze kufanikiwa ni lazima ujenge network na bodaboda owners ili waje kwako na ikiwezekana walete wenzao..

Unaweza kuwa unawapa motisha wakileta wateja hata kuwapunguzia kidogo bei ilimradi isiathiri profit margin yako!

Wengine ongezeeni.
 
Habari zenu wanaJF. natumaini mnaendelea vema na shughuli zenu za kimaendeleo. ninaomba msaada wa kutambua maeneo yenye wakazi na watumiaji wengi wa vifaa vya pikipiki. endapo kuna mtu anaweza kunisaidia hilo, tafadhali nijulishe kwa whatsap 0784-419775. natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote atayenisaidia kunishauri eneo.
nawatatika kazi njema.
 
Habari zenu wanaJF. natumaini mnaendelea vema na shughuli zenu za kimaendeleo. ninaomba msaada wa kutambua maeneo yenye wakazi na watumiaji wengi wa vifaa vya pikipiki. endapo kuna mtu anaweza kunisaidia hilo, tafadhali nijulishe kwa whatsap 0784-419775. natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote atayenisaidia kunishauri eneo.
nawatatika kazi njema.
hayo maeneo yanajulikana hata wewe unayajua. Ukiona mtaa una bodaboda nyingi si ndio hapo unapopahitaji!!! Maswali mengi namna hiyo mwishowe ukishaambiwa utaanza kuuliza faida ikoje. Ingia kwenye business take risk. Kama mtaji unao jitose na mtegemee mwenyezi mungu. Watu wanashindwa sana kuelewa masuala ya kufanikiwa katika maisha muwezeshaji ni yeye Rabbana. Mtu anaanza na mtaji wa milioni moja anakuwa milionea na wewe unaanza na milioni 50 unaishia kuganga njaa tu.
 
Mkonowapaka kwa mtaji wako mimi naweza kukuunganisha na kiwanda cha spea za piki piki kule China na utaweza kuagiza mwenyewe na utapiga hela sawa na hao wahindi.

Wewe ukiwa tayari utaniconsult, mimi ni importer wa vitu vingine ila kuna jamaa yangu niliwahi kumpa huo mchongo ila akakosa mtaji.

Konzogwe, tafadhali naomba nami uniunganishe na hawa jamaa, nimetafuta muda mrefu kupata contact kama hii.
 
Angalia video hii uone MAAJABU ya tube za WAWA SUPPER RUBBER
Check out this video on YouTube:


Mkuu gkileo, mi nina frem ya biashara napenda kujua nikiwa na milion moja na.nusu naweza kufanya biashara hiyo ya vifaa kwa rejareja?
 
Konzogwe, tafadhali naomba nami uniunganishe na hawa jamaa, nimetafuta muda mrefu kupata contact kama hii.
Mtite una mawazo kama.yangu...biashara ya vifaa vya pikipiki kwa kweli inalipa ukizingatia kwa sasa pikipiki ni nyingi sana mtaani
 
Nina wazo la kufungua biashara ya spea za pikipiki, kwa mwenye uelewa anijuze ni aina gani ya spea zinatumika au kuhitajika zaidi, na ni maeneo gani mazuri kuweka hii biashara. Je ni mtaji kiasi gani unahitajika.
 
Back
Top Bottom