marandu2010
JF-Expert Member
- Aug 7, 2010
- 1,199
- 435
Wakuu kwa mara nyingine tena:
Pikipiki zimeenea sana sasa hasa katika jiji letu la Dar es salaam.Hii inanifanya nione biashara ya spea za pikipiki itakuwa inalipa sana?
Sijajua upande mwingine wa shillingi. Hebu nipate mawazo yenu wakubwa.
Mna maoni gani katika hili?
Asanteni sana wakuu.
===
2.
Natumaini hamjambo wanajamii wa JF especially jukwaa hili,
Mimi ni kijana niliyeajiriwa sekta ya umma..nimeamu nijitose kwenye ujasiriamali...hasakwenye sekta ya usafirishaji hususani spea za pikipiki kama nilivyoainisha.
Kwa kuanzia nimefanya uchunguzi wa kutosha sehemu ninyaoishi ina pikipiki nyingi ila spea ndio hamna...sehemuitapatikana ila nahitaji kama kuna yeyote anaefahamu zaidi jins ya kuplan business hii anaipe some inputs.
Kama starting capital,vifaa vizur vya kuanzia kununua,bei na mengineyo.
Ninachukua mkope hivi karibuni nimeonelea bora nitimize iyo ndoto ya ujasiriamali maana uthubutu tayari ninao.
Pia niatanunua pikipiki kama 2.
Nimetenga nusu ya mkopo wangu wa 8mil ndio nianzie busness is it enough?
Asanteni.
=> Maoni na Ushauri
Pikipiki na spea zake zina soko,ila lazima ununue spea feki za china,siyo feki ila ni spea zisizo madhubuti,inalipa sana kwa mtazamo wangu hasa ktk miji midogo ,siyo Dar, kwa Dar itakulazimu uuze bei ya jumla.
100% nakuunga mkono kabisa ulichoandika....ukitaka kuendelea ku-survive kwenye soko lazima uweke bidhaa feki za kichina, na sababu ni:
- Watanzania walio wengi ni wako sensitive kwenye price....ukiweka kifaa genuine automatically bei yake lazima iwe juu ...sasa basi waliowengi wana opt kununua za bei ya chini...ambazo ni brand za kichina ( Nimejifunza haya kutokana na biashara ninayoifanya ya vifaa vya ujenzi)
- Pikipiki zilizo nyingi nchini ni za kichina ( affordable kwa kila mtu) - hivo tumia simple formula Pikipiki za kichina= spea za kichina......hapa unakuwa uwewapa wateja kitu wanachokipata
- Suppliers wa spea za Pikipiki hasa za kichina ni wengi........ila kaka inatakiwa uwe makini sana kwenye manunuzi ......hiki ndo kitu nilichojifunza. Unaweza ukakwea pipa mwenyewe ukaingia China au Ukanunua kwa whole salers walioko kariakooo. Si kila muuza spea kariakoo anasafiri...wengine ni misheni town tu af maduka yao wame-display kama wholesalers
Wakuu heshima kwenu,
Baada ya kupita pilikapilika za uchaguzi, sasa tuachane nazo, maana watanzania hawataki mabadiliko, kila mmoja atakura kwa ulefu wa akiri zake.
Wakuu naomba mwenyeuzoefu wa hii biashara ya kuuza vifaa vya pikipiki, naomba anisaidie.
Je, mtaji wa milioni moja utafaa?
Vifaa gani muhimu kwenye duka?
Je, faida yake inakuaje, na hasara zake inakuaje na changamoto zake pia?
Mimi naishi Kimanzichana mkoa wa Pwani.
Asante
=====
Sidhani kama Mtaji wa milioni moja utatosha,labda nikuulize hapo ume include kodi ya pango,kumlipa muuzaji etc.Nikupe mfano tairi ya pikipiki size ya san lg kubwa moja ni 50000 jiulize na spea zingine itakua bei gani?
Kaa chini survey uone vifaa gani vinahitajika sana kwa watumiaji ambapo unaenda kufungua duka,andika list yake na bei za manunuzi.
tazama faida ya kila kifaa angalia makadirio ya mauzo ghafi na baadae faida halisi utakayopata ukikamilisha hayo angalia kamtaji kako kama kanatosha.Ili uweze kufanikiwa ni lazima ujenge network na bodaboda owners ili waje kwako na ikiwezekana walete wenzao..
Unaweza kuwa unawapa motisha wakileta wateja hata kuwapunguzia kidogo bei ilimradi isiathiri profit margin yako!
Wengine ongezeeni.
Mkuu hongera sana kwa hili na mungu akusaidie. But huja sema uko wapi. Eneway ushauri wangu.
Kama utakuwa umepata eneo la kuuzia hizo spea fanya yafuatayo.
1. Nenda kule Kariakoo, pale utakutana na waagizaji nje wa spea za piki piki wale wamespecialize kama ni toyo utakuta waagizaji wa toyo, kama ni sunlg utakuta waagizaji wa vifaa vya sunlg na kazalika kila aina ya pikipiki ina waagizaji wake wakuu wa spea nje na hawa sanasana ni wahindi
2. Ongea nao na chukua bei za kila spea za pikipiki zinazo patikana mtaani kwenu
3. Waambie unataka kufungua duka la kuuza spea na kama hutaweza kuspecialize unaweza chukua spea za kila aina ya pikipiki
4. Patana nao, hawa jamaa wanaweza kuwa wanakuletea yaani unawatumia hela benk then unawatumia sumary ya spea unazo taka wao watazichua na watazifunga kwenye box then watakutumia either kwa njia ya basi mpaka mahali unafanyia biashara means mji, haina haja ya kufuata mwenyewe bongo.
Yangu ni hayo tu
Dimma,
Kwanza kabisa hongera kwa uthubutu, pili biashara ya spear usiifanye kama hujui hata kutofautisha bearings na matumizi yake wapi inafungwa na vifaa vingine kama hivyo.
Pia biashara hyo inahitaji uwepo wako ili kuweza kutambua mzunguko mzima wa biashara yako unaendaje, hiyo ikiwa ni pamoja na kujua vifaa gani vinakuwa rahisi kutoka ili visikosekane. Hapo ndio inaweza kuwa starting point yako. Spear sio kama ubwabwa kuwa umkabidhi jungu muuzaji huku ukiamini utamuhesabia plates.
Kingine ni location; hii Ina matter zaidi hasa mwanzoni unapo fikiria kufungua. MWISHO ni aina ya spear unayonunua ni kampuni gani,kuna spear ukinunua baada ya wiki ishasagika, kufanya return hutaruhusiwa Wala kuweza, hivyo umakini unahitajika.
Fuatilia hayo kwa muhtasari ukiwa tayari karibu kkoo tukuhudumie kwa Bei ya jumla nawe ukauze kwa rejareja.
Wasalaam