Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Mizani:

Muwe waangalifu na hii kitu. Ukisafirisha mbao hasa msimu huu wa mvua zikilowa zinaongezeka uzito na ukifika kwenye mizani la haula!. Lazima upunguze mzigo na kulipa faini!
hiyo ndyo nlikua nasubiria hhehehe ilimkutaga jamaa yangu akaliaa hapo Mikese.
 
Wakati wa manunuzi kagua zile tape measures! Jamaa wajanja sana wanazikata na kupunguza urefu wa mbao! Ukiweza beba yako mwenyewe!

women-tape-measure.jpg
 
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako,vp kwa huo mzigo mkubwa wa semi trailer kwa utalaamu wako ukisafirisha kuuza dodoma utakuwa na faida nzuri?,na vp kuhusu garama za usafiri hadi Dodoma?
Jamaa wanaofanya hii biashara wanasema trip moja ya semi trailer inakuwa na faida ya milion tatu na zaid;hii biashara ni nzuri ila tafuta soko kwanza la kuuzia;mzigo wenyewe unapatikana muda wote.
 
Mkuu malila katika utafiti wangu juu ya kilimo cha miti ,kuna makala nimesoma wanasema ili kupunguza gharama za uendeshaji kama moto,ulinzi wa msitu nk wanashauri ili upate faida nzuri upande eneo kubwa au wakulima wadogowadogo wenye lengo moja waungane. Je, kwenye umoja wenu ndio munavofanya au?
 
Pia inaonekana wenzetu wa afrika ya kusini wanazo mbegu bora na hata uganda.je mushawahi kuagiza mbegu huko? Je, kuna changamoto yoyote ya kuagiza mbegu huko.
 
Eucalyptus,unaanza baada ya miaka sita hivi, ukipata Zimbabwe gereration yatatu, miaka mitano waweza vuna mirunda, factor kubwa ni sehemu ulikootesha.

Malila naomba kufahamu kwa sasa mti gani una thamani na unahitajika kwa sana sokoni kati ya eucalytus grandis ukipata generation ya 3 au pinus patula au cyprus na kama ukitupatia bei zake itafurahisha zaidi.
 
Vipi mkuranga..je kunastawi?.kuna mtu yoyote mwenye experience eneo hilo?..na ni mitiki tu au kuna aina ingine pia?

Mkuranga nina uzoefu kidogo, mitiki inataka ardhi yenye mvua za kutosha kama Kilombero, Mtibwa, Tanga, Rufiji. Mkuranga kama utaotesha ktk mabonde, mitiki inagoma sana, nimejaribu Yavayava na Msorwa mpaka Shungubweni, ila pande za Kibiti inaweza mea.

Eucalyptus inamea ila sio kwa speed kubwa.
 
Mkuu malila katika utafiti wangu juu ya kilimo cha miti ,kuna makala nimesoma wanasema ili kupunguza gharama za uendeshaji kama moto,ulinzi wa msitu nk wanashauri ili upate faida nzuri upande eneo kubwa au wakulima wadogowadogo wenye lengo moja waungane. Je, kwenye umoja wenu ndio munavofanya au

Ndio tunavyofanya.
 
Malila naomba kufahamu kwa sasa mti gani una thamani na unahitajika kwa sana sokoni kati ya eucalytus grandis ukipata generation ya 3 au pinus patula au cyprus na kama ukitupatia bei zake itafurahisha zaidi.

Kwa soko la ndani Cyprus inaongoza ila haupatikani. Saligna ndio unafuata/grandis na pinus patula na mwisho ni gums.

Unataka bei kwa futi au?
 
pia inaonekana wenzetu wa afrika ya kusini wanazo mbegu bora na hata uganda.je mushawahi kuagiza mbegu huko? je kuna changamoto yoyote ya kuagiza mbegu huko

Mara nyingi nimechukua pinus patula Nairobi, 2014 nimenunua Malawi mlingoti. Hakuna Changamoto,cha msingi agiza kwa mtu sahihi
 
LIGEDENGE 1

Kupasua na kuuza mwenyewe inalipa sana. Ila kama huna muda wa kusimamia hiyo kazi nakushauri,kama msitu uko karibu na mji uza msitu usepe. Kama una muda wa kusimamia hiyo kazi, angalia msimu mzuri ili usombaji na upasuaji usiathirike na majira.
 
Last edited by a moderator:
Safi sana, lakini sio kila sehemu miti inakubali. Kwa kanda ya ziwa kwa mfano ni Sengerema ma bukoba tu ndio maeneo pekee miti hii ya mbao inakubali. Sehemu zingine kazi kweli kweli.
 
Safi sana, lakini sio kila sehemu miti inakubali. Kwa kanda ya ziwa kwa mfano ni Sengerema ma bukoba tu ndio maeneo pekee miti hii ya mbao inakubali. Sehemu zingine kazi Kweli Kweli.

Kila sehemu kuna jamii ya miti ya mbao inayoota na kukua vizuri, kwa kuwa hapa imetajwa michache. Hata Iringa kuna maeneo pines hazikubali ila acrocarpus inafanya vizuri. Mbinga pine ipo, lakini Songea haipo,ila sederela/tiki ipo. Kwa hiyo tafuta jamii ya mti sawa na hali ya hewa ya mahali husika.
 
Back
Top Bottom