Hii mitiki (teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja (wanatumia kwa nguzo za umeme, kujenga meli na fenicha za gharama), kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000.Kuna miti inaitwa mitiki,hii vipi kupanda mpaka kuvuna inachukua miaka mingapi? Je hizo pines na eucalyptus nikipanda kwenye heka 10 ninunue miche mingapi? Au unaweza kunisaidia kupanda miche ya hekari kumi?
KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda january 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
Kuna mwenye data za gharama za upasuaji na usafiri wa kuleta mbao Dar ili tuweze kulinganisha tofauti ya kuuza miti na kupasua mbao mwenyewe? Vilelive hiyo miti ya Sao Hill inayouzwa shs 50,000 ina umri gani tulinganishe na umri wa miti ya wakulima wadogo wanauuza shs 10,000 kwa mti. Je umbali kutoka kwnye barabara kubwa au Dar, kwa mfano, Njombe vs Iringa unaleta tofauti kiasi gani kwenye bei ya miti?
Asante.
hii mitiki(teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja(wanatumia kwa nguzo za umeme ,kujenga meli na fenicha za gharama) , kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000
Kwa sasa hivi sina gharama za upasuaji wa miti. Kwa kweli upasuaji karibu wote kwa sasa unafanywa pale Mafinga kwenye misitu ya serikali kwani huko vijijini ni kama miti imekwisha kabisa. Ni vigumu sana kwa mfano kupata miti kwenye plot moja ambayo unaweza kupasua na kujaza semi-trailer moja. Naweza kusema hali itakuwa hivyo kwa karibu miaka kumi ijayo kwani ni sasa tu watu wengi wameanza kupanda miti kwa wingi sana.
Miti wanayouza Sao Hill ina umri wa miaka 25 na kuendelea. Huko vijijini mti hata uwe mkubwa kiasi gani wanunuzi watanunua sana sana kwa Shs 20,000. Lakini kwa sasa hakuna miti huko vijijini, labda eucalyptus.
Wakati wa boom wa mbao kule Njombe na Makete watu wengi walikuwa wanasafirisha mbao kwa kutumia TAZARA. Hata hivyo miti mingine husakwa vijijini ambako kwingine hakuna usafiri mzuri sana. hata hivyo nimeshuhudia wanunuzi wa miti wakichimba barabara ili kutoa mbao zao.
Kuhusu kuuza mti au kuupasua mimi ningependelea kuupasua mimi mwenyewe na kuuza mbao. Lakini inategemea una miti kiasi gani. Kama unayo michache ni afadhali kuuza miti.
Tuwe tunafanya utafiti kabla hatujakosoa post za watu, kuna hadi taarifa kwamba kuna mtiki umewahi uzwa hadi $20,000!.kwa bei nyingi wana state $500 kwa cubic mita ambapo mti mmoja unaifikia na kupita, hapo bado hujauza maranda kama veneer, tatizo letu hatupendi kutafiti , bila shaka european union wasingewekeza $29million kama isingekuwa na hela nzuri, ukiachana na hayo nilisoma kwenye kijarida cha mazingira huko kilwa kuna kijiji walikuwa wanauza magogo kwa Tsh 1.2miliioni, biashara ya magogo ina hela mno ndio maana yule mtoto wa nguema ni tajiri sana.Tuwe waangalifu na utoaji wa data zenye matata ili kutunza hadhi ya jukwaa. Tunajua mitiki ni gharama ila hiyo bei (in red font) kwa mti haileti mantiki.
Assante kwa majobu yako;
Natumaini unafahamu kuwa tuna umoja wetu wa misitu wengi wetu ni members was JamiiForums. Kama hufahamu ningependa tuwasiliane ili ufahamu tunafanya nini na jinsi ya kuweza kuwasiliana. Organizer wetu ni Malila na tumepanda mamia ya ekari msimu huu. Na baadhi wamekuwa wakinunua mashamba ya wanakijiji ya ekari chache.
Kama hufahamu kuhusu kuhusu umoja wetu wa misitu na ungependa kujua tunachofanya wasiliana na Malila ili tuweze ku share information.
Asante.