Clara Daud
JF-Expert Member
- Sep 23, 2016
- 542
- 273
Nilikuwa shamba Njombe,
Ni kweli soko la Ulaya linataka viwango ila lipo na linakuwa sana. Wapo vijana njombe wanauza parachichi Italy, na mimi nimefika shambani kwao. Nikiwa Njombe mjini nimeshuhudia maandalizi ya kilimo cha Matunda kule Ihanga,pia Madeke Lupembe kuna nanasi la kufa mtu na kiwanda kinajengwa. Kwa sasa parachichi zinasindikwa Kiwira Mby, akina Chai bora wanalima parachichi for export kule Mby/Mufindi.
Kwa ufupi, soko la matunda huko majuu lipo sana toka huku kwetu, kama mtu yuko serious aseme nimpe simu ya vijana pale njombe aone nini kinaendelea.
njema sana hii naomba nikupm
Ni vizuri kujua mteja anataka viwango gani na wewe utimize,usichakachue. Nikiwa Iringa ktk kiwanda fulani, Waholanzi walimwaga mzigo wetu wote baharini kwa sababu tuliongeza sukari kidogo ktk pineapple rings tulizopeleka.
njema sana hii naomba nikupm mkuu