Biashara ya kuuza genge

Inategemea unapanga kuuza nini..vitu kama nyanya ndimu na aina za matunda ni perishables
kununua na kupata hasara kwenye hivyo vitu ni kawaida tofauti na vitunguu nazi na viazi..nakushauri ufanye genge duka kwa maana pamoja na kuuza vitu vya kawaida kama nyanya na pilipili na maembe uwe pia unauza na vitu vingine kama sabuni mafuta, maji nk...anza taratibu kupata uzoefu waweza anza na vitu kama nyanya vitunguu carrot hoho dagaa chumvi samaki nk...

SOKO:.Masoko ya dsm yanatofautiana sana..unaweza pata matunda bei rahisi sana buguruni, machungwa nazi maembe mihogo viazi nk...Temeke stereo unaweza pata pia matikiti na mapapai kwa bei rahisi sana..kariakoo utapata vitunguu na mboga mboga bei chee kwa kupatana ...ILALA viazi mbatata na ndizi ni bei rahisi sana.. MTAJI..ukiondoa kodi kwa kuanzia laki 5 inatosha ila hata ukiwa na chini ya hiyo unaweza kuanza tu cha muhimu uanze na kupata uzoefu..sio biashara mbaya kama upo eneo lenye mzunguungo mzuri wa pesa na unaweza kujibana itakulipa..changamoto ni hiyo ya mgawanyiko wa masoko yenyewe ila kama mtaji ukikua utakua unaletewa hapo hapo ofisini vitu vyako...kila la kheri
Mchango mzuri sana, kwa uzoefu wako ni maeneo yapi ambayo unadhani kwa biashara hiyo ndani ya Dsm kuna mzunguko mzr wa pesa
 
Wakuu za muda huu
naombeni ushauri wa jinsiya kuanzisha genge la kisasa
ambalo nitaweka ndani ya fremu
nataka kuuza mbogaamboga zote
dagaa wa aina zote
matunda
mafuta ya kupikia
nafaka zote
na vinginevyo
mwenye mchanganua wa biashara hii na bei naomba msaada
 
Hakuna kitu inaumiza jf kuona nyuzi kama hizi na forum kama hii vijana wanapita kushoto, unakuta replies tatu over ila kwenye forum za siasa,udaku vijana wanajitutumua mno huko pahala,hakika kwa mwendo huu vijana tutazidi kuwa vibaraka wa wanasiasa ba celebrities
 
Safi sana mkuu hili ni wazi zuri sana, ushauri wangu kwanza angalia location ina walaji? Kisha fanya utafiti kwa competitors wako alaf zingatia sana ubora na usafi katika biashara yako.
 
Mkuu biashara ya Genge inalipa sana..

Zingatia eneo lisiwe "Ushuani" sana, weka eneo la wakazi wenye kipato cha kati. Nakuhakikishia baada ya miezi minne utakuja na Uzi Wa ushuhuda mwingine. Kuna MTU namfahamu ana genge kama hilo amejenga Nyumba yake ya kuishi hapa hapa Dar. Bidhaa kama nyanya,karoti,vitunguu,pilipili n.k huwa namuona anaenda kulangua ilala na siku nyingine temeke stereo.

Zamani alikuwa anaenda kulangua alfajiri sana ila siku hizi huwa namuona anaenda asubuhi SAA tatu au NNE , sababu yake anasema wafanyabiashara huwa wanawapindishia bei ya kununua kwa jumla wale wanaoenda asubuhi kwa sababu wanajua wanawauzia wafanyabiadmshara wanaoenda kuuza tena mitaani. Na pia alfajiri mrundikano ni Mkubwa sana. Ila anasema ukienda asubuhi bei mnapanga vizuri na yeye siku zote kwa muda huo huwa ananunua bidhaa kwa bei nafuuu saaaaaaana

Maelezo mengine wadau watatoa
 
Wakuu za muda huu
naombeni ushauri wa jinsiya kuanzisha genge la kisasa
ambalo nitaweka ndani ya fremu
nataka kuuza mbogaamboga zote
dagaa wa aina zote
matunda
mafuta ya kupikia
nafaka zote
na vinginevyo
mwenye mchanganua wa biashara hii na bei naomba msaada
hebu namba ulielezee hilo genge la kisasa mwonekano ake ukoje nje na ndani ili nikushauri
 
Vegetable shop
stock-vector-vegetable-and-fruit-market-stall-with-prices-farm-market-stand-with-tomato-and-carrot-pepper-552683362.jpg
 
Mkuu biashara ya Genge inalipa sana..

Zingatia eneo lisiwe "Ushuani" sana, weka eneo la wakazi wenye kipato cha kati. Nakuhakikishia baada ya miezi minne utakuja na Uzi Wa ushuhuda mwingine. Kuna MTU namfahamu ana genge kama hilo amejenga Nyumba yake ya kuishi hapa hapa Dar. Bidhaa kama nyanya,karoti,vitunguu,pilipili n.k huwa namuona anaenda kulangua ilala na siku nyingine temeke stereo.

Zamani alikuwa anaenda kulangua alfajiri sana ila siku hizi huwa namuona anaenda asubuhi SAA tatu au NNE , sababu yake anasema wafanyabiashara huwa wanawapindishia bei ya kununua kwa jumla wale wanaoenda asubuhi kwa sababu wanajua wanawauzia wafanyabiadmshara wanaoenda kuuza tena mitaani. Na pia alfajiri mrundikano ni Mkubwa sana. Ila anasema ukienda asubuhi bei mnapanga vizuri na yeye siku zote kwa muda huo huwa ananunua bidhaa kwa bei nafuuu saaaaaaana

Maelezo mengine wadau watatoa
Asante
 
Hakuna kitu inaumiza jf kuona nyuzi kama hizi na forum kama hii vijana wanapita kushoto, unakuta replies tatu over ila kwenye forum za siasa,udaku vijana wanajitutumua mno huko pahala,hakika kwa mwendo huu vijana tutazidi kuwa vibaraka wa wanasiasa ba celebrities

Dooh! Mkuu ,hivi ule usemi wa kidhungu "many are invited but few are chosen" hujawahi kuusikia
 
Swali 1:

Mimi ni mkazi wa Dar es Salaam, ningependa kufanya biashara ya kuuza genge, naomba msaada wenumwenye kujua naweza nunua wapi vitu vya sokoni kwa bei nzuri, na nikimuajiri mtu aniuzie inabidi nimlipaje?

Natanguliza shukurani..

Swali 2:

Pinkshlady
habari wana jf, nawazo lakuanzisha biashara ya genge, lakini la kitofauti kidogo na haya tuliyozoea, nikiwa na imani nitawateka watu wengi, sababu itakuwa karibu na barara kuu na paking ipo ya kutosha,

nikitarajia kuuza matunda ya aina zote, vitu vya sokoni, mayai, ikiwezekana na kuku.

Naomba ushauri wenu niwe na mtaji kiasi gani wa kuanzia? ni soko gani naweza kupata vitu kwa bei ya chini?

na kuna ulazima wa kuwa na leseni ya biashara?

Ushauri:

Mkuu ulifanikiwa kufungua?
 
Back
Top Bottom