Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Hello JF,
Nina wazo hilo la biashara, nataka nimwezeshe mdogo wangu afanye;

Pendekezo liwe Unga Wa Dona ukichanywa na aidha Unga Wa mtama au Ngano halisi. Kisha nitafunga au pack ktk ujazo Wa kuanzia kg 1 hadi 15kg.

Masoko tarajiwa ni Supermarkets, mini markets, maduka kawaida, migahawa, hotelini na mashuleni nk.

Hili ni wazo tu, naomba ushauri wako Wa nyongeza ktk hili. Na pia unayependa wazo hili Jaribu, Tanzania bado kubwa.

Karibu.
 
Wadau. Nimeisha anza mchakato wa hiyo kitu kwa maana ya jengo ambayo mi nimeiita phase one sasa ndo najipanga kuezeka.

Phase two ni kununua machines ambazo ni full set kusaga na kukoboa pamoja na mizani mikubwa na midogo na packaging materials bila kusahau mahindi ambayo mdo mtaji.

Phase three ni kuanza kazi.

Naomba muongozo au ushauri kwa ambaye either anafanya au anauzoefu na hii biashara japo kwa reaserch ndogo niliyofanya inalipa na nimeamua kuanza at a medium level scale walau nipate market share kias fulan lakin naona changamoto ni nyingi mf kupata mahindi fake, unga au mahindi kuharibika ama kuoza, n.k nk.

Hizo picha ndo mjengo wa kiwanda na bahati nzuri nina eneo kubwa hapa kwangu so nimeona bora nijenge hapa kupunguza gharama na iwe rahisi kusimamia.

Ntashukuru kwa ushauri.
View attachment 174571
View attachment 174572
View attachment 174573

Mkuu tunaomba mrejesho umefikia wapi na hii mega project
 
This is the best idea,,,for those who are expert in this business could you give us the challenges and how to overcome them
 
Wakati tunasubiri wataalamu wa hiyo kada, mimi ningependa nikupongeze kwa hiyo hatua uliyofikia... HONGERA SANA.

Katika biashara chache ambazo ni very promosing for the future mart demands ni 'food processing'. There's hopes in this enterprise.

Kuna makala flani nilisoma, huko Mwanza kuna kampuni flani ya kupack na kusambaza unga, ilianza na capital ya almost 1.5M lkn ndani ya miaka mi5 ilikua na turnover ya around 8 bn. Nahisi hiyo kampuni ilikua 1st runner ktk shindano la best mid-sized companies in Tz 2014.

Cha msingi ujue demand ya wateja wako, ujue jinsi gani utaweza kupata resouces za kurun biashara yako non-stop, biashara yako ijitangaze, produce more than the needs of your consumers ili uwe aggresive kupanua biashara yako zaidi na zaidi.

Just a few.
Ndugu. Kila biashara ina siri zake. Wàsagaji wa nafaka wamewahi kuibuka wakiwa na mashine nzuri na miundombini bora ya usambazaji, lakini wengi hoi au wamefilisika. Kampuni ya Bhakhresa, Scandnavia na moja iko Kibaha zote hoi kwenye usagaji wa mahindi.

Nyumba ya pazia la kila buashara inayokua kwa spidi kuna siri kubwa.
 
Hongera kwa hatua uliyofikia mkuu, hivi kwa wajuzi gunia la kilo 100 la mahindi kwa wastani huwa linatoa unga wa sembe kilo ngapi na pumba kilo ngapi?
 
Hongera kwa hatua uliyofikia mkuu, hivi kwa wajuzi gunia la kilo 100 la mahindi kwa wastani huwa linatoa unga wa sembe kilo ngapi na pumba kilo ngapi??
Kutegemeana na mahindi, unaweza pata uwiano wa Unga 50 % mpaka 70% inayobaki pumba. Yani unga kilo 50 mpaka 70 na pumba kilo 30 mpaka 50. Mahindi ya ubora wa wastani yanatakiwa kukupa at least 65kg na pumba 30 kg.
 
By experience!

Nenda mikoa ya Iringa au Mbeya, nunua mahindi moja kwa moja kwa wakulima, sogeza mahindi kwenye mashine ya kusaga iliyo karibu ili kupunguza carriage cost!

NB: hapa uwe umeshaongea na watu wa mashine, ikiwezekana uwe unawaachia pumba ili gharama ya usagishaji iwe chini zaidi (chini ya 5000/= kwa gunia)

Mahindi yakifika kiasi unachotaka, anza kusaga na kupaki(kwa kuanza unaweza kuwa unatumia mashine ya kushonea ya kukodi na mifuko yenye nembo ya mtu mwingine (mtafute)!

Gharama ya mfuko tupu usio na nembo ni around 200-350 bei ya jumla na 400-600 wenye nembo)

Kipimo kiwe kilo 5, 10, 25 na 50 (gharama ya upakiaji kwa makuli ni around 700 kwa kila kilo 50!

Tafuta magari yanayosafirisha mizigo mikubwa, ongea nao wakuunganishie mzigo wako kwa wasafirishaji wengine (madalali are so good in this)!

Mzigo ukifika mkoa wako wa soko waombe wakushushie sehemu ambayo ni rahisi kwako!

Zambaza mzigo kwa wateja wako!
Mdau GreenCity nimevutiwa na mchango wako juu ya biashara hii. Je kwa mfumo huo bado vibali vya TBS na TFDA vinahitajika? Na leseni ya biashara ya aina hii inaweza kuchukua muda gani kuipata? Umeongea pia juu ya nembo ya mtu mwingine unadhani nahitajika kuongea na mhusika juu ya kutumia nembo yake?

Mm nina mashine tayari ya kusanga na kukoboa .ila naona kuna changamoto ya kupata vibali vya ruhusa ya uzalishaji toka kwa TBS na TFDA . Ndio maana nimeona ww una weza nipa nwanga zaidi kwa plan B ya kutumia mashine za kulupia.
 
Mm ninaifanya hii kitu kwa muda kidogo sasa ngoja niwape ujanja kidogo ingawa bado nakuza mtaji maana ndo kwanza nimetoka chuo

Ninatafuta mahindi vijijini then nayaleta mjini nikifika hapo kuna wafanyabiashara wakubwa ambao tayar wapo kwe soko la unga kwa muda mrefu na wana mashine zao ninachokifanya mm nikifika na mahindi yanga ninayasimamia yanasagwa na kufungwa kwe mifuko ya ujazo wa kg 25 then ninaiuzwa kwa jumla kwa mmiliki wa mashine then naiuza na pumba then narud vijini kusaka mahindi

Ni biashara nzur tena sana since nimeianza sijui kitu kinachoitwa hasara

Kwa wenye mitaji mikubwa unaweza tafuta soko lako mwenyewe la unga na hata kufungua mashine zako na ikakulipa zaidi

Nadhani nimetoa ABC kidogo kwa maelezo zaid 0659902425

Changamoto kubwa kwe kwe hii biashara ni variations ya bei za mahindi
 
Back
Top Bottom