Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Kutokana na ripoti ya umoja wa mataifa kupitia shirika la WFP, nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara zinakabiriwa na ukame, hilo huenda likasababisha ukosefu wa chakula miongoni mwa jamii maskini.

Kutokana na ripoti hizo, ndipo nikaja na wazo la ujasiliamali baada ya kuona mambo ya ajira hayasomeki, ikichukuliwa sasa hivi ndo niko mwaka wa mwisho chuoni.

Kama habari inavyojieleza kuna mikoa yenye njaa hapa nchini kama vile Simiyu, Dodoma, Singida na kwingineko.

Kwa sasa niko Kigoma likizo-nyumbani, so wakati wa mavuno mahindi huwa bei chee huku, mfano gunia la debe 6 huwa ni Tsh 35,000/= tu. Sasa ndipo nimefikilia kwa mtaji wangu wa Tsh 1,000,000/= ambayo ni kujipinda na kuweka hela ya bumu ninaimani nitaipata.

So, kwa wakazi wa mikoa hiyo na mingine, pia wazoefu wa hii biashara ya kuchukua mahindi huku na kuyasaga unga wa dona na kuyauza mikoa hiyo siwezi kupata faida?

Nawasilisha.
 
Wakati unasubiria Ushauri hebu endelea kufanya. Timiza ndoto zako kutokana na kile ambacho hisia zako zimekituma, ukitegemea hisia za MTU mwingine katika kutekeleza wazo lako utapotea. Hakuna jipya chini ya Jua kila wazo LA biashara limeshafanyiwa kazi, sasa kilichobaki ni INNOVATION+COMPETITION, ndy njia pekee ya kukufanya uweze kuishi katika biashara. Timiza Lengo lako biashara iko more theoretically haitabiriki wala haina specific definition ndy maana watu wa kitaa Layman's wanatusua wakati wasomi wanabaki na SWOT Analysis kwenye makaratasi
 
Ungawa ulio packed unaliwa sana Mijini ambapo vjjijin sana hudaga mahindi kwenye mashine.

Mjinj ni kutokana na ubize wa watu kwenda kusaga mahindi.

Kuhusu kusaga Dona inakuwa haina faida sana kwa sababu watu wanao pack ubga hupata pesa kupitia pumba ambazo kama mwaka huu mwanzoni Gunia la kilo 50 lilifika 40,000.

Sembe ndo nzuri. Pia lazima ujue consumer behaviour ya watu wa huko unako taka kuwauzia unga,
 
Ungawa ulio packed unaliwa sana Mijini ambapo vjjijin sana hudaga mahindi kwenye mashine.

Mjinj ni kutokana na ubize wa watu kwenda kusaga mahindi.

Kuhusu kusaga Dona inakuwa haina faida sana kwa sababu watu wanao pack ubga hupata pesa kupitia pumba ambazo kama mwaka huu mwanzoni Gunia la kilo 50 lilifika 40,000.

Sembe ndo nzuri. Pia lazima ujue consumer behaviour ya watu wa huko unako taka kuwauzia unga,
Nashukuru sana kijana, kumbe pumba zinafaida kubwa hivyo?
 
Hbr mr Okohi, tunashukuru kwa jitihada zako za kutupa update, hata hivyo ongera kwa jitihada zako za kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha unga, kwangu mimi nilitaka tu kukupa ushahuri kuwa utakapokuwa umekamilisha ujenzi wa majengo ya mitambo na store basi nitafute nikupe ushahuri wa mashine, katika dunia ya leo hatutumii tena roller machine kwa kukoboa kwani inakuwa na wastage kubwa ya mahindi, wastani wa gunia la kilo 108 kgs kwa roller machine utajikuta unapata kg 75 au 78 za mahindi, lakini kuna mashine za kisasa output baada ya kukoboa inakuwa kg 92 hadi 95 ktk gunia la kg 108 hii inakupa faida kubwa na tija zaidi, ukiamua kutegeneza unga wa dona machine hii ndo yenyewe, capacity yake ipo ya ton 20 kwa siku, 30tons kwa siku hadi 50tons inategemea utaaamua kutumia hammer mill au vip, hata hivyo ktka kusaga kama utaamua kutumia hammer mill ni wakati mzuli kupata vinu vizuli vya kisasa kabisa vinavyotumia motor ya HP50 vinu 3 stainless steel unga unakuwa bora sana na sio carbon steel mill,

haya bwana kazi ni kwako, thanks
Mkuu naomba ushauri kuhusu machine bora
 
Hangaika na vingine. Swala la mahindi niachie mimi, naomba tender.
 
Wadau. Nimeisha anza mchakato wa hiyo kitu kwa maana ya jengo ambayo mi nimeiita phase one sasa ndo najipanga kuezeka.

Phase two ni kununua machines ambazo ni full set kusaga na kukoboa pamoja na mizani mikubwa na midogo na packaging materials bila kusahau mahindi ambayo mdo mtaji.

Phase three ni kuanza kazi.

Naomba muongozo au ushauri kwa ambaye either anafanya au anauzoefu na hii biashara japo kwa reaserch ndogo niliyofanya inalipa na nimeamua kuanza at a medium level scale walau nipate market share kias fulan lakin naona changamoto ni nyingi mf kupata mahindi fake, unga au mahindi kuharibika ama kuoza, n.k nk.

Hizo picha ndo mjengo wa kiwanda na bahati nzuri nina eneo kubwa hapa kwangu so nimeona bora nijenge hapa kupunguza gharama na iwe rahisi kusimamia.

Ntashukuru kwa ushauri.
View attachment 174571
View attachment 174572
View attachment 174573
Mdau tunaomba mrejesho wa project yako hiyo ya kusaga nafaka.. mafanikio n.a. changamoto mkuu
 
Habari wakuu.

Natafuta mtu wakufanya nae biashara ya unga wa sembe na dona.njoo na milioni 25 tufanye Kazi hiyo pamoja .

Eneo nimeshanunua kibaha jengo nimeshajenga bado kuweka mashine na umeme wa 3 face Kiwanda ni kukubwa na kina store pia.

Nilipanga nimalize December mwaka huu kiwanda kianze kazi lakini mipango haijakaa sawa au kwa anayejua taasisi inayowezesha viwanda kama hivyo Kwa mkopo.

Kwa muhitaji tuwasiliane PM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom