Biashara United yaondolewa katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiondoa timu ya Biashara United katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa kutofika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ahly Tripoli (Libya)

CAF imesema sababu zilizoifanya Biashara United kushindwa kwenda Libya kucheza hatua ya pili ya raundi ya awali hazikutokana na dharura. Mechi hiyo ilikuwa ichezwe Oktoba 23 huko Benghazi

C9FE3CEC-A6CA-41E2-B47E-BCC574C16408.jpeg
 
Ni uzembe na ujuaji mwingi ndio umewasababishia hayo. They have themselves to blame

Wakati mwingine hua nawaelewa TFF inapozibeba Simba na Yanga inapokuja suala la kuiwakilisha nchi kimataifa. Timu hizi hazijawahi na haziwezi kufanya upuuzi wa kushinwa kwenda kuwakilisha nchi pale inapokua jukumu lao kufanya hivyo kwa kisingizio cha ukata

Hivi vitimu vya msimu vinatia doa na aibu kwenye historia ya ushiriki wa vilabu vyetu michuano ya Afrika. Hii ni timu ya pili sasa baada ya Mtibwa Sugar nayo kutuaibisha 2007(kama sijakosea mwaka)
 
Kiinglish
 
Kama tatizo lilikuwa fedha so wangesema tuwachangie, lakini TFF lazima wawe accountable pia, kwanini washindwe kuisaidia timu uende kushiriki
 
Uzembe upi?inshu ilikuwa pesa sasa unaposema eti ni uzembe wangezitoa wapi hizo pesa?safari ya kwanza ilikuwa hivyo hivyo, michuano kama hiyo kama huna pesa ya uhakika lazima tu uta fail tu!!!hapa timu zinazoweza ni yanga, simba na azamu tu.kwingine huko ni lawama tu.
 
Kwani Tff, jukumu lao ni kuvisaidia virabu kwenda kwenye michuano ya kimataifa?na mbona yule msemaji wao kila siku alipokuwa akihojiwa anasema tatizo sio pesa!!bali ni mchakato tu,
 
Uzembe upi?inshu ilikuwa pesa sasa unaposema eti ni uzembe wangezitoa wapi hizo pesa?safari ya kwanza ilikuwa hivyo hivyo, michuano kama hiyo kama huna pesa ya uhakika lazima tu uta fail tu!!!hapa timu zinazoweza ni yanga, simba na azamu tu.kwingine huko ni lawama tu.
ni uzembe kwa sababu mda ulikwepo ,hawa majamaa wangeandaa hata harambe watu wangechanga ,au wangeenda hata bungeni wachangwe au kuomba msaada kwenye taasisi mbalimbali ,afisa wa TFF alipokuwa anahojiwa na Azam alisema hawakusema Wana matatizo ya kifedha na wala hawakuomba msaada
 
Nikiangalia mechi wanayocheza sasa dhidi ya mbeya city huu uwanja wanaoutumia kama wa nyumbani ni wa hovyo sana na inathibitisha hii timu ni ya hovyo.Hata kama uwanja sio wao lakini wanashindwa vipi kuwa na makubaliano na wenye uwanja hata ya kuumwagilia maji tu ili angalau nyasi ziwe na ukijani?
 
ni uzembe kwa sababu mda ulikwepo ,hawa majamaa wangeandaa hata harambe watu wangechanga ,au wangeenda hata bungeni wachangwe au kuomba msaada kwenye taasisi mbalimbali ,afisa wa TFF alipokuwa anahojiwa na Azam alisema hawakusema Wana matatizo ya kifedha na wala hawakuomba msaada
Tuwe wakweli huwezi kuendesha timu kwenye michuano ya kimataifa kwa kutegemea harambee, kama wangekuwa wakweli TFF, labda ingewakopesha tu pesa, ikaja kuwakata kwenye mgao wao wa azamu, kama ndege tu hiyo ya serikali ilikuwa ni kama $ 120, 000!!kuikodi kwenye ligi wangeishi maisha magumu sana, kulilipa hilo deni, badaye tena wangeleta zogo kuwa wanashindwa kushiriki ligi vizuri!!!mpira wa sasa kama huna pesa huuwezi.
 
Sasa kipi afadhali ,maana baada ya mda CAF wanakuja tena na nyundo ya kuwafungia miaka miwili kushiriki
 
Wawafungie tu, kwani kuna faida gani unashika nafasi ya kuliwakirisha taifa, unategemea misaada!!!mnaweza kuwa na wawakirishi watano lakini hawana faida bora muwe na wawili wanaojitambua na kufika mbali.
 
Utopolo na uzee wao wote huwa wanatembeza bakuli na maisha yanaenda, Sasa hao Biashara siwangetembeza bakuli tu
 
Uzembe upi?inshu ilikuwa pesa sasa unaposema eti ni uzembe wangezitoa wapi hizo pesa?safari ya kwanza ilikuwa hivyo hivyo, michuano kama hiyo kama huna pesa ya uhakika lazima tu uta fail tu!!!hapa timu zinazoweza ni yanga, simba na azamu tu.kwingine huko ni lawama tu.
Walisema Kama hawana nauli.wachangiwe?.
ni siku ngapi zimepita kabla ya mechi!
wangepewa hata ndege ya serikali.kwa hatua waliyofikia walikuwa wana dhaminika
 
Back
Top Bottom