Biashara magendo ya fedha za kigeni inashamiri kwa kasi !

Watu walitajirika sana enzi za magendo zama za Giza naona wamerudishiwa kutajirika tena
 
Unafurahia biashara ya magendo kushamiri kwenye taifa lako?
Umeshiriki magendo halafu unafurahia kabisa?
Watu kama wewe mnasitahili mjeledi kabisa ili mpate akili na uzalendo, na kama ingelikuwa ancient Bhaharat au China wewe ni wakunyongwa kabisa.
Uzalendo 0%
Jinga kweli wewe,hujui lolote zaidi ya kula na kulala sebuleni kwa Shemeji yako
 
I wish unipatie na mimi hiyo namba namba maana ninashida kinoma ya kupata dollar!!!Kama hautojali nicheki PM tuyajenge maana mzee baba kashafanya yake huku kwenye njia halali
 
Export ya bidhaa zisizo na kodi itashamiri sana mipakani watu kwenda kubadili DOLA na safari manunuzi bidhaa nje ya nchi. Hata China Kuna bureal mtaani za kutosha. China hawateseki sana na thamani Pesa yao,wao focus yao balance of trade.
Pia hawatumii nguvu kubwa kuthibiti wafanyabiashara wadogo ndio maana copy ni nyingi, hasa kwa bidhaa nchi maskini.
 
Arusha ndio michezo yao. Mwisho was siku, utakuta dola zipo mtaani na mabank hayana dola
Wafanyabiashara wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni walianzia kwenye black market serikali ilichowafanyia ni kama mmewasaidia kukuza biashara zao😎
 
Jiulize tu mitutu ya bunduki na biashara wapi na wapi
Kwa kweli inahitaji elimu ifanye kazi badala ya mitutu.
Huwezi amini kuna watu wanaishi ulaya huku wakiishi Tanzania kwa sababu ya technology ukitumia mtutu huwezi tambua.
Come on leaders wake up!
Kuna elimu kubwa sana mtaani imezagaa bila matumizi unadhani watakula vipi hawa na maelimu yao kama sio huku.
Think wide
 
Hahaha serikali imeshtuka watu wananunua dollar wanafukia, ukitunza shilingi inakula kwako.
 
Ngoja ukishikwa na hizo dollars halafu hauna risiti ya manunuzi yake. Ndiyo utaelewa uzuri wake.
Ndiyo wanakuja kulia humu sijui serikali iache unyang'anyi wa kidola..!! mara wanachukua hela za watu kimabavu kwenye A/C zao yaani sijui Watanzania tupoje..!!
 
Unafurahia biashara ya magendo kushamiri kwenye taifa lako?
Umeshiriki magendo halafu unafurahia kabisa?
Watu kama wewe mnasitahili mjeledi kabisa ili mpate akili na uzalendo, na kama ingelikuwa ancient Bhaharat au China wewe ni wakunyongwa kabisa.
Uzalendo 0%
The best solution ni kuhakikisha inawekea mifumo sahihi na thabiti ya kuzuia biashara hii ya magendo kwani kwa asili binadamu kaumbwa na ubinafsi. Sheria, taratibu, kanuni na miongozo viliwekwa ili kudhibiti mienendo ya mwanadanu ikiwemo ubinafsi
 
Unafurahia biashara ya magendo kushamiri kwenye taifa lako?
Umeshiriki magendo halafu unafurahia kabisa?
Watu kama wewe mnasitahili mjeledi kabisa ili mpate akili na uzalendo, na kama ingelikuwa ancient Bhaharat au China wewe ni wakunyongwa kabisa.
Uzalendo 0%
Wanyonge kwanza wale waliotupora kwenye EPA, IPTL, ESCROW, MEREMETA, RADAR, FERRY, MAJUMBA YA SEREKALI NK, kisha ndio mje mumalize na huyo, hapo ndio tutakuelewa. Vinginevyo ni unafiki tu hamna lolote.
 
Naona Serikali ilifanya kazi nzuri kuyavamia maduka ya fedha za kigeni. Kwa sasa DOLA ya Marekani, Euro pamoja na Pound ya Uingereza inapatikana kwa njia ya magendo tena kwa bei nzuri zaidi ya ile ya madukani (FOREX Black Market). Fedha nyingi sana zinatembea mtaani ambayo inaikosesha serikali mapato makubwa sana.

Jumamosi, nikiwa eneo Fulani maarufu hapa Arusha, jamaa mmoja aliuza kiasi cha $125,000 ndani ya gari. Mimi nilikwa nahitaji $1,300 kwa ajili ya safari yangu Zambia, Mlangoni mwa Bureau De Change, jamaa kanivuta mkono na kuninong’onezea kwamba, hapo utasumbuka.

Piga hii namba, alinipa namba na baada ya kuipiga, haikuchukua muda, kama dakika 6 nilifika sehemu fani na kupata fedha za kigeni kwa bei nafuu.

Bila kunificha, hii biashara ni nzuri mtaani kuliko kwenye maduka. Watu wengi wanauza fedha hizi kimagendo kwa maana wanaona ni usumbufu kwenda kwenye bureau de change.

Naona Serikali imeamua kujikosesha fedha makusudi
Sasa mkuu, how would you know kuwa fedha ukizouziwa sio feki? Nadhani moja ya vitu vinavyochochea rushwa/uhalifu ni willful participation kama yako
 
Kufurahia nchi kukosa mapato ni upunguani. Hata Mtanzania kukwepa kulipa kodi ni uhujumu uchumi. Kwa nini hatujifunzi kuwa wazalendo kwa taifa letu? Shame on you uliyejisifu kwa kuikosesha nchi mapato.
 
Back
Top Bottom