Biashara inataka moyo sana

Biashara matangazo.

Biashara ubunifu ...

Biashara Customer care ..

Biashara biashara biashara

Wewe si unaleta nadharia zako za kwenye vitabu ,but ushawahi kufanya kila kitu Kwa usahihi na usione matunda,mimi kuna kipindi nilihisi kwenye biashara yangu labda watu wanaona giza tuu unafunga ofisi saa mbili asubuhi na kufunga saa tano hakuna prospect wala mteja aliyeingia dukani
 
Pia hamna jipya mkuu.

Uchumi wa fremu yaani, kila mtu wazo lake ni kukodi fremu auze bidhaa/huduma fulani. Kuna nini?
Hata mentality ya viongozi wenyewe si ndio hiyo hiyo ? , mtu kama Mengi alipoomba vibali vya kuanza kuwekeza kwenye mradi wa gesi asilia ,alipewa dongo kwamba ,watanzania wana mitaji ya kuzalisha juice mambo ya gesi hawawezi .
Wanaona ni bora ngozi nyeupe aje awekeze kwenye strategic sectors kuliko mbongo ,wakati in a long run ,uchumi kuendeshwa na raia wake na kuwafaidisha kiuchumi ndio mafanikio halisi .
Angalia nchi kama Marekani , ile nchi matajiri asilimia kubwa ni wazawa wa pale na biashara kwa asilimia kubwa zinamilikiwa na wazawa na wanapewa na subsidies kabisa wakitikisika kiuchumi kwenye hizo biashara zao ,maana serikali inajua wide implications za biashara za wazawa kuteteleka .
Nchi nyingi ni hivyo hivyo
Sisi huku tupo tu bora liende
 
Matokeo yake ndio hayo sasa ,kuwa na taifa la wachuuzi badala ya uchumi ambao uko diversified
Unakuta clothing stores kumi sehemu moja , unategemea nini hapo ,ni mwendo wa kurogana tu na kupigana fitna + low purchasing power ya raia WA bongo
 
Mimi ni graduate nilipata kazi nikafanya kwa muda wa miaka kama saba hivi kupata mtaji then nikaamua kuanzisha biashara,unajua biashara kuanzisha si kazi ukiwa na mtaji,kazi ngumu kwenye biashara ni kuifanya iendelee kuwepo.

Sasa wakati biashara inaanza mara nyingi inaanza vizuri but ukifika muda unakuta mambo hayaendi kabisa number ya wateja wako basic unakuta ghafla hawapo na hakuna wateja wapya wanaoingia dukani kwako aisee hii kitu usiombe unafanya kila kitu unachoweza kufanya kwa usahihi alafu matokeo hupati apa ndio nikajua kwa nini watu wanaenda kwa waganga.

Mashekhe au kwa wachungaji ili kuweza kupata msaada, kuna kipindi biashara inakua ngumu mpaka unaona bora urudi kwenye mshahara wa laki tano kwa mwezi big up sana kwa wafanya biashara walioweza kukuza mitaji hii kitu siyo rahisi mazee
Kaka upo kwenye biashra ganj mnk tumefanan
 
Na kitu kingine watu wengi biashara tunaanzisha Kwa mawazo yetu kichwani sasa na hii mitaji midogo downfall zikitokea biashara inakua kwenye risk ya kufilisika lakini ukiwa na familia ya watu wafanya biashara ni ngumu kupitia kwenye mashimo sababu waliotangulia washajua michoro yote ya biashara na kuipata faida
Uko sahih sana
 
Tulia wewe ,hujui kitu
We unaona hizo biashara zimesimama unadhani hizo biashara ndio zinagenerate faida si ndio ?
Watu wanafanya mambo yao meusi pembeni hizo biashara ni changa la macho tu
Watu wanafanya utakatishaji pesa , ukwepaji kodi , Rushwa , kuuza bidhaa feki , kupunja na kufanya Magumashi kibao
Mfumo wa nchi hii ni wa ovyo mno
Hairuhusu private sector na ujasiriamali kuthrive ,kama unaona hizi ni stories anzisha biashara halafu ulete mrejesho hapa
Mpe ukweli
 
Matokeo yake ndio hayo sasa ,kuwa na taifa la wachuuzi badala ya uchumi ambao uko diversified
Unakuta clothing stores kumi sehemu moja , unategemea nini hapo ,ni mwendo wa kurogana tu na kupigana fitna + low purchasing power ya raia WA bongo
Mimi mmachinga hapa Posta Dsm naishuhudia sana hii hali, maana karibia wote tunaffanana . Wote tunachuuza miwani, tai, mikanda, wallet ,chaja za simu na notebooks na peni. Yaani mtu akiwa na mteja full kutoleana macho, sometimes mpaka kushikana masharti.
 
Wewe si unaleta nadharia zako za kwenye vitabu ,but ushawahi kufanya kila kitu Kwa usahihi na usione matunda,mimi kuna kipindi nilihisi kwenye biashara yangu labda watu wanaona giza tuu unafunga ofisi saa mbili asubuhi na kufunga saa tano hakuna prospect wala mteja aliyeingia dukani
Hapo bado watu wa tozo chungu zima na wengine wa mchango wa mwenge wanakusubiria.
 
Back
Top Bottom