Kuwa na siku 2 ndani ya siku 1 ili ujenge biashara ukiwa umeajiriwa

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,810
3,101
Rafiki yangu mpendwa,

Kukosa muda imekuwa ndiyo kisingizio kikuu cha wale walio kwenye ajira na hawajawa na biashara.

Unakuta mtu yupo kwenye ajira, ambayo inampa kipato kidogo na kisichotosheleza, lakini pia hana biashara ya pembeni ambayo ingeweza kumwongezea kipato.

Ukimshauri afanye hivyo, yaani kuanzisha biashara ya pembeni, anasema ajira inabana muda wake hivyo hawezi kufanya biashara ya pembeni.

KUWA-NA-1024x576.jpg


Rafiki, kwenye maisha kuna vitu viwili ambavyo haviwezi kupatikana au kukosekana kwa pamoja. Vitu hivyo ni MUDA NA PESA. Mtu akiwa na PESA nyingi, anakuwa na muda kidogo na akiwa na MUDA mwingi, anakuwa na pesa kidogo.

Haiwezekani ukawa huna vyote, yaani PESA na MUDA. Ninachotaka kukuambia ni kwamba kama ajira inakubana MUDA wako wote, basi inapaswa kukupa PESA nyingi kiasi kwamba unaweza kuyaendesha vizuri maisha yako.

Kama ajira yako haikupi KIPATO cha kutosheleza, inapaswa kukupa MUDA wa kufanya mambo yako mengine. Na ukweli ni kwamba kwa ajira zote ambazo hazina kipato kikubwa, huwa zinakuacha na muda mwingi.

Ni jinsi unavyopangilia na kutumia muda wako nje ya ajira ndiyo itaamua kama utaweza kujenga biashara na kuongeza kipato chako au la.

Tukirudi kwenye hesabu za muda, utazidi kuona jinsi ambavyo kama una kipato kidogo kwenye ajira na huna biashara ya pembeni basi umeamua tu kuyapoteza maisha yako.

Kila mtu ana masaa 24 kwenye siku yake, hakuna mwenye ziada wala mwenye pungufu.

Tukiondoa muda wa kulala kwa siku, muda wa juu kabisa ambao unashauriwa kiafya ni masaa 8 kwa siku. Hivyo ukitoa kwenye 24 unabaki na masaa 16.

Kama umeajiriwa, masaa ya kazi kwa siku ni kati ya 8 mpaka 10, hivyo kwenye masaa 16 unabaki na masaa 6.

Swali ni je, hayo masaa 6 kwa siku huwa unafanya nayo nini ambacho unaweza kujivunia nacho?

Sawa, tuseme unahitaji masaa mengine 2 kwa siku kwa ajili ya kula na kuwa na watu wa karibu. Bado unabaki na masa 4 ambayo huwezi kuyaelezea yanaenda wapi.

Nikukubalie pia kwamba huenda kuna masaa mengine 2 ambayo unayatumia kwenye foleni za kwenda na kutoka kazini, bado unabaki na masaa ya ziada mawili, hebu tuambie unayapeleka wapi hayo masaa?

Unajua unakoyapeleka, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii ambapo hakuna fedha unaingiza, kufuatilia maisha ya wengine, kushabikia vitu ambavyo havikulipi na kadhalika.

SOMA; BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira.

Rafiki, ninachotaka kukuonyesha ni kwamba kama kipato chako ni kidogo na huna biashara ya pembeni unayopambana nayo kukuza kipato, unapoteza muda wako na maisha yako. Iwe unakubali au unakataa, huo ndiyo ukweli.

Suluhisho ambalo nakupa hapa ni wewe kutengeneza siku 2 ndani ya siku moja.

Siku ya kwanza ni ile unayompa mwajiri wako na siku ya pili unajipa mwenyewe kwenye biashara yako ya pembeni.

Unaweza kuipanga siku ya kwanza ikawa ni saa 12 asubuhi mpaka saa 10 jioni, ambayo hiyo ni kwa ajili ya mwajiri.

Halafu siku ya pili ikawa ni kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 4 usiku ikawa kwa ajili ya biashara yako.

Ukiweza kuzipangilia na kuzitumia vizuri hizo siku zako mbili unazotengeneza kwenye siku moja, utaweza kujenga biashara nje ya ajira yako na kukuza kipato chako.

Kwenye kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA ambacho nimekiandika kwa lengo la kumwongoza kila mwajiriwa kuweza kujiongezea kipato kisicho na ukomo, nimeshirikisha mpango mzima kwako kuwa na siku mbili ndani ya siku moja.

Hicho ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kuwa nacho ili aondoke kwenye malalamiko ya kipato cha mshahara kutokutosheleza maisha.

Kama bado hujapata kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, wasiliana sasa na namba 0678977007 kupata nakala yako.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua zaidi kuhusu dhana hii ya kuwa na siku mbili ndani ya siku moja. Karibu ujifunze na kuchukua hatua ili uondoke kwenye kipato duni cha mshahara.



Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
 
Back
Top Bottom