Bhoke Munanka, Waziri wa zamani wa Nchi ofisi ya Rais akishughulika Usalama, afariki

Be a true patriot for one second and answer this question objectively:

Kwa nini Nyerere alisema namba 3 on that list of fame ni muhuni?

Kaka hapa tunaongelea UFISADI wa kiuchumi na sio wa kisiasa ama kijamii....nadhani tunalewana....

Tanzanianjema
 
Kwa nini Nyerere alisema namba 3 on that list of fame ni muhuni?

Mkuu TZ Njema,

Tizama, mimi sijui kuzunguka mibuyu huwa ni straight to the point, hiyo pint hapo inaonyesha one thing in a big picture yaani unafiki, majungu na uzandiki wetu wa-Tanzania,

Mwalimu ni kweli kwenye mkutano mmoja na wa waandishi wa habari nyumbani kwake, alimuita Malecela na Kolimba kuwa ni wahuni, kwa sababu walikuwa ni viongozi, kama wengine wote wanaopenda wanawake nje ya wake zao, lakini Mwalimu hakuwahi kumsema hivyo Kawawa,

Na besides, yeye mwenyewe Mwalimu, alikuwa na tabia hiyo hiyo chafu ya kuwa na mawahara nje ya mkewe Mama Maria, kuanzia Lucy Lameck, Mama Mary Mackeja, na Mama Doris Makene, na yule Mama Wickens, lakini haukukuwa na mwenye ubavu wa kumuuliza kuwa na wewe Mwalimu, mbona pia ni fuska na mhuni kama unavyowaita wenzio, hapana kesho yake ikawa a media fiesta na mpaka leo masikini ya Mungu, bado kuna tunaoendelea kuimba hizi nyimbo bila kuuliza ukweli wake,

Nafikiri by now unajua kuwa nia na madhumuni ya Mwalimu, ilikuwa ni moja tu katika kurusha haya maneno machafu dhidi ya hawa viongozi, ilikuwa ni kumpitisha Mkapa, ili awe rais. Malecela anasema kuwa angejua mapema kuwa hii ndio iliyokuwa sababu angempisha mapema sana, lakini Mwalimu hakusema nia yake mapema, in fact Malecela anasema kuwa aligundua nia ya Mwalimu, siku ya kuchukua fomu alipomlazimisha Mkapa kwenda kuchukua fomu na yeye ndani ya kikao cha NEC, ukumbi mzima ulipigwa na butwaa, kwa sababu hapa Mwalimu alikuwa anavunja tradition aliyoianzisha yeye mwenyewe kuwa anayemtaka tu ndio huchukua fomu, Mwinyi clear wanted Malecela kumrithi na ilikuwa inafahamiaka na viongozi wote mle ndani ya kikao,

Mwalimu alikwua akilalamikia uamuzi wa Malecela, akiwa Waziri Mkuu kujaribu kumaliza tatizo la Muungano, kwa kupitisha sheria ya serikali tatu na kuifanya kila nchi ndani ya muungano kujitegemea yenyewe, Mwalimu aliita huu kuwa ni upumbavu wa hali ya juu, na wananchi wengi tukamshangilia sana,

now look tulipo na muungano!
 
FMES said:
Mwalimu ni kweli kwenye mkutano mmoja na wa waandishi wa habari nyumbani kwake, alimuita Malecela na Kolimba kuwa ni wahuni, kwa sababu walikuwa ni viongozi, kama wengine wote wanaopenda wanawake nje ya wake zao, lakini Mwalimu hakuwahi kumsema hivyo Kawawa,

Na besides, yeye mwenyewe Mwalimu, alikuwa na tabia hiyo hiyo chafu ya kuwa na mawahara nje ya mkewe Mama Maria, kuanzia Lucy Lameck, Mama Mary Mackeja, na Mama Doris Makene, na yule Mama Wickens, lakini haukukuwa na mwenye ubavu wa kumuuliza kuwa na wewe Mwalimu, mbona pia ni fuska na mhuni kama unavyowaita wenzio, hapana kesho yake ikawa a media fiesta na mpaka leo masikini ya Mungu, bado kuna tunaoendelea kuimba hizi nyimbo bila kuuliza ukweli wake,


FMES,

..Mwalimu alipowaita Malecela na Kolimba wahuni sidhani kama alikuwa akimaanisha tabia ya kutembea nje ya ndoa. Mwalimu alikuwa akilitumia neno "mhuni" kumaanisha kiongozi mwenye maamuzi mabovu au asiye na msimamo.

..mara nyingine naomba uwasitiri hasa hawa mama zetu. wengi hapo wameshatangulia mbele ya haki. tena hata waume zao kama, Prof.Dr.William Makene, aliyepata kuwa daktari wa Mwalimu, pia ametangulia mbele ya haki.
 
Jokakuu,
Ni kweli kabisa Nyerere aliposema Malecela ni MHUMI alikuwa na maana hiyo kwani haifichiki kabisa kuwa Malecela alikuwa na msimamo wake thabiti na kila mara alikuwa akimpa shida mwalimu kama Mkandara hapa...
Tatizo la Muungano ni kwamba Malecela aliona mbali, He was RIGHT ktk mawazo yale kwa sababu tulipoondoka UJAMAA ambao maamuzi mengi ya kiuchumi yalikuwa chini ya serikali kuu ilitakiwa pia mwongozo mpya ktk Kuitazama Tanzania Kiuchumi upatikane haraka iwezekanavyo!.
Nyerere hakuweza kuona huko, akili yake ilikuwa kuuweka Muungano kama ulivyo akifikiria kwamba bado SIASA zitaweza kuendesha UCHUMI (kama wanavyofanya China) lakini hakujua mazingira yaliyokuwepo.. He was damn wrong! Tanzania ilikuwa inaelekea njia tofauti kabisa na China -UFISADI ndio ulitawala fikra za hawa viongozxi maskini wa akili na Mali. Pengine Malecela alijua haya mapema lakini hakusikiwa akaitwa Mhuni. sababu kubwa ni kwamba hawa wawili walikuwa against kundi kubwa la viongozi wengine ambao pengine waliogopa kuwa against Mwalimu.

Samahani wakuu, kipande hiki hakihusiani na mada hii lakini ningependa kusisitiza tu kitu kimoja kuwa hao watu, mwalimu aliowachagua walikuwa na mawazo tofauti kabisa na Mwalimu alivyokusudia ama kufikiri.. Mwalimu alikutana na UMDHAINAE KUMBE SIYE!.. Aliyemdharau, huyo Malecela pengine ndiye angetupeleka kuzuri, badala ya hawa viongozi waliokuja iteka CCM na kutuletea Utawala mpya wa kuchonga (art)..
Tazama, China leo ambao viwanda vyao vilikufa yakawa mapango ya nguchiro kama sisi chini ya UJAMAA waliweza kubadilisha kabisa mfumo mzima wa kiuchumi, mgao.. Hayo magofu mloyaona wakati ule mkakataa katakata kununua nguo hata dawa ya mswaki toka China ndio leo vinazalisha kishenzi.. Watu wengi wamesahau kabisa kwamba miaka ya 60, 70 na 80 hakuna mtu aliyenunua kitu China ddunia nzima tena ktk nchi za Magharibi mali za China zilipigwa marufuku..How come wao wameweza kuinuka sisi ktukachukua mkondo wa kutegemea wageni kufufua viwanda vyetu!.. Damn Nyerere.. alitu lostisha kwa Mwinyi na Mkapa!
 
..Mwalimu alipowaita Malecela na Kolimba wahuni sidhani kama alikuwa akimaanisha tabia ya kutembea nje ya ndoa. Mwalimu alikuwa akilitumia neno "mhuni" kumaanisha kiongozi mwenye maamuzi mabovu au asiye na msimamo.

Naona mkuu wangu mimi na wewe tunakazi kubwa sana ndani ya hii forum, lakini tutafika tu, ila ninaamini majibu ya Mkandara nimazito sana kuhusiana na hii hoja yako, i hope utamsoma vizuri maana amesiliba kabisaaa na hoja nzito sana, bravo Mkandara!

..mara nyingine naomba uwasitiri hasa hawa mama zetu. wengi hapo wameshatangulia mbele ya haki. tena hata waume zao kama, Prof.Dr.William Makene, aliyepata kuwa daktari wa Mwalimu, pia ametangulia mbele ya haki.

One minute unawatukana Malecela na Kolimba, the next minute unasema niwasitiri waliotangulia kwenye haki, sasa Kolimba uliyemtusi hapo juu bado yupo hapa duniani au yeye sio bin-adam anayepaswa kusitiriwa kwa your standards za High Class, au?

Again Mama Doris Makene, hakuwahi kuwa mke wa Makene hata siku moja, alikuwa hawara wa Makene (aliyezaa naye watoto wawili) na Mwalimu at the same time, Mwalimu alimzidi nguvu Makene, akamchukua jumla na kumuhamishia kwao Shinyanga, alipomaliza naye akamuweka under house arrest, marufuku kutoka nje ya Shinyanga,

Hii kwako hai-sound kuwa ni uhuni wa hali ya juu kwa aliyekuwa akiita wengine wahuni?
 
Mkandara,

..mimi nadhani matatizo ya Mwalimu na Malecela yalikuwa siasa tu.

..alichotumia Mwalimu ni mbinu za kisiasa kumchafua mgombea asiyemtaka, ili mgombea wake apite.

..Malecela naye alipaswa kujipigania kama kweli alitaka kuwa Raisi na alimini ana uwezo huo.

..yaliyomkuta Malecela yalishawakuta wenzake waliomtangulia kama Kawawa,Msuya,Warioba. pia waliomfuatia kama Sumaye wamekutana na mambo hayo hayo--majungu ya kisiasa.

..sisemi kwamba hao niliowataja hapo juu ni malaika au watendaji wazuri wa kupigiwa mfano, lakini mengi tuliyolishwa juu yao ni siasa tu. yale ya muhimu hatuna habari nayo.
 
..mimi nadhani matatizo ya Mwalimu na Malecela yalikuwa siasa tu.

..alichotumia Mwalimu ni mbinu za kisiasa kumchafua mgombea asiyemtaka, ili mgombea wake apite.

..Malecela naye alipaswa kujipigania kama kweli alitaka kuwa Raisi na alimini ana uwezo huo.

..yaliyomkuta Malecela yalishawakuta wenzake waliomtangulia kama Kawawa,Msuya,Warioba. pia waliomfuatia kama Sumaye wamekutana na mambo hayo hayo--majungu ya kisiasa.

..sisemi kwamba hao niliowataja hapo juu ni malaika au watendaji wazuri wa kupigiwa mfano, lakini mengi tuliyolishwa juu yao ni siasa tu. yale ya muhimu hatuna habari nayo.


Wwwoooow! kumbe unayajua haya mkuu!
 
Field Marshall ES,

..sikuleta majina ya Kolimba na Malecela ktk thread hii.

..hebu punguza munkari kidogo.

..mimi naomba tu hawa kina mama wasitiriwe. ni hilo tu.

..narudia: sijawahi kumtukana Malecela, Kolimba, wala mwanasiasa yeyote.

..mambo ya unyumba na "uhuni" huwa naogopa kuyagusa.
 
..Mwalimu alipowaita Malecela na Kolimba wahuni sidhani kama alikuwa akimaanisha tabia ya kutembea nje ya ndoa. Mwalimu alikuwa akilitumia neno "mhuni" kumaanisha kiongozi mwenye maamuzi mabovu au asiye na msimamo.

..mara nyingine naomba uwasitiri hasa hawa mama zetu. wengi hapo wameshatangulia mbele ya haki. tena hata waume zao kama, Prof.Dr.William Makene, aliyepata kuwa daktari wa Mwalimu, pia ametangulia mbele ya haki

Field Marshall ES,

..sikuleta majina ya Kolimba na Malecela ktk thread hii.

..hebu punguza munkari kidogo.

..mimi naomba tu hawa kina mama wasitiriwe. ni hilo tu.

..narudia: sijawahi kumtukana Malecela, Kolimba, wala mwanasiasa yeyote.

..mambo ya unyumba na "uhuni" huwa naogopa kuyagusa.

Mkuu kama nimekuelewa vizuri sana hapa, wewe umemsitiri sana Kolimba, ambaye pia ametangulia kwenye haki, naona kwako kina mama waliotangulia kwenye haki tu ndio wanatakiwa kusitiriwa, lakini kina baba kama Kolimba, hapana what a standard za ki-high class hizi au! duh!

Haya nimekusikia mkuu!
 
1. Peter Siyovelwa
2. Edward Sokoine
3. John Malecela
4. Paul Sozigwa
5. Job Lusinde
6. Amir Jamal
7. Mack Bomani
8. Adam Sapi
9. Daudi Mwakawago
10. Mhaville
11. Leader Sterling
12. Dr. Bryson
13. Said Maswanya
14. Erasto Mange'nya
15. Lucy Lameck
16. Bibi Titi Mohamed
17. Nossoro Moyo
18. Elinawinga
19. Simon Chiwanga
20. Aaaron Chiduo
21. Ibrahim Kaduma
22. Abdallah Twalipo
23. Abdallah Natepe
24. Thabit Kombo
25. Idrisa Wakil
26. Aboud Jumbe
27. David Musuguri
28. Nsa Kaisi
29. Dr. Salim Salim
30. Gisley Mapunda

Na wengineo wengi ambao siwezi kuwakumbuka vizuri, lakini hawa niliowataja ninawakumbuka sana kuwa walikuwa ni wasafi kabisa, ingawa baadaye kuna watu kama Sozigwa na Mwakawago, walishia kuchafua records zao lakini bado sio kwa ufisadi wa hali ya juu kama wengine ambao sikuwataja hapa.

Ahsante Mkuu!
Naomba kuchepuka nje ya mada kidogo,nitoe yaliyo moyoni kuhusu ni nini haswa tumerithi na kujivunia kutokana na Viongozi 'SAFI' wa zamani??

Mkuu,"History is what makes the Future",ni sentensi ambayo nimekunukuu katika maandiko yako ya awali,pamoja na listi nzito ya majina ambayo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu wengi wao hatupo nao tena hapa Duniani. Mimi ninaamini kuwa hakuna kitu kibaya kama Heshima ya Woga.Katika hiyo listi ya 'wasafi' uliyo itaja hapo juu 'usafi' wa hao jamaa haukutokana na Nafsi zao wenyewe bali walikuwa hivyo kwa 'kumuheshimu' na kumridhisha Mw.Nyerere.Walitamani sana kuwa na mali,na mbaya zaidi hata kama mali zile walizipata kihalali,ilikuwa ni kinyume na siasa za wakati ule.Nakumbuka wakati fulani Serikali ilitaifisha gari aina ya Range Rover iliyokuwa ikimilikiwa na Mzee Kaduma(UDSM) eti kwasababu ni gari ya kifahari,watu waliyo fahamika kuwa na 'Video'(kama ilivyo julikana wakati huo)ni wachache sana,(Prof.Mahalu,Mama Msikinya-Hall3manager by then)na ilikuwa siri kubwa. Mawazo ya Viongozi hao 'safi' hayakupewa nafasi kwa wakati ule fikra za Mw.Nyerere pekee ndizo zilizokuwa sahihi,kama mtakumbuka misukosuko iliyo mkuta Prof.Babu(Mungu amrehemu Mwanazuoni huyu).
'Usafi' wa wakati ule ulikuwa wa bandia haukuwa wa kweli,watu walilazimishwa kujinyima bila ya madhumuni yeyote maalumu,matokeo yake uongozi wa Kizazi cha leo na jamii nzima ya watanzania umeshindwa kuridhi dhana ya 'usafi' wa viongozi waliotangulia na badala yake kinatafsiri 'usafi' huo kama 'Umasikini',na siyo umasikini wa hali na mali tu,bali umasikini wa AKILI vilevile.
Mwinyi,Mkapa,Ngombale,Malecela..... kama kweli Mw.Nyerere alikuwa kiongozi safi,basi hawa walipaswa kuendeleza 'usafi' waliyo urithi katika uongozi wa awali,lakini tumeyaona katika nafasi zao mbalimbali madarakani,Ruksa,Mtaji wa maskini nguvu zake mwenyewe,Ari mpya kasi mpya....vurugu tupu!!
**Unajua wakati mwingine huwa najiuliza hivi Tanzania tunaposema kuwa twajivunia amani iliyo tawala,je hii ni 'amani' au ni 'Ujinga'??
 
Jokakuu,
Mkuu hapana Malecela na Nyerere hawakuwa wapinzani Kisiasa isipokuwa Nyerere alitaka kumburuza kama alivyowaburuza wengine lakini wakati huo huo alifahamu kwamba Malecela ni kichwa. Uonvi mkubwa ulowahi kutokea kati yao ni swala la Muungano na tumeona wenyewe kwamba Malecela was right at that particular moment. Malecela hakuwahi ku raise swala la Muungano wakati wa UJAMAA na kusema kweli ilikuwa shwari ktk vipindi vyote isipokuwa maswala la Udini na fikra pandikizi za baadhi ya watu.
Malecela kwa lugha ya pwani kweli mhuni maanake anajiamini, mfano mwingine wa Uhuni ni pale alipoamua kuchukua form ya kugombea Urais kipindi cha 2005 wakati NEC hawana habari kabisa. Kwa wajumbe wengi walimwona Mhuni ama kafanya Uhuni lakini hakuvunja sheria.. Alijua anayo haki ya kufanya hivyo lakini asingeweza kupita. Uhuni waliofanya kina Mkapa, Mwinyi na Kawawa kukataa kumsikiliza haikuwa siasa hata kidogo bali walijua Malecela ni moto toka enzi ya Mwalimu, lakini kwa mtazamo wao ha fit ktk profile yao ya kuwa Mtawala kwa sababu he was better than them all.
Sio kwamba namsifia isipokuwa najua kwamba watu kama Malecela, Salim, Warioba ni watu waliokuwa ktk ngazi tofauti ya Uongozi nje ya mtazamo wa viongozi wengi wa CCM. Sijui kama niseme ni chuki na UNafiki lakini trust m,e wote hawa wanafahamu kwamba Malecela, Salim, Warioba ni viongozi bora na wanaostahili nafasi za juu kuliko hawa vijana. Just imagine Mwinyi alikuwa nani?... Hata huyo Mkapa alikuwa wapi ktk nafasi za viongozi wetu, haya sasa hivi tunae Kikwete, binafsi sidhani kama walipikwa (walitayarishwa) vizuri kuweza kushiika Kiti cha IKULU isipokuwa mwalimu siku zote hakupenda challenge ya aina yoyote ile iwe kimawazo ama kiutendaji kwa sababu Nyerere alikuwa na malengo yake...KUUFIKIA UJAMAA na KUJITEGEMEA bila kujua kwamba hao kina Mwinyi na Mkapa walikuwa wakisubiri wakati tu!..
Kolimba yuko wapi mkuu, kina Malima, Mwaikambo wote hawa walikuwa chachu ya utawala uliopo na sio kisiasa.. MALENGO yao yalikuwa tofauti kabisa na mtazamo wa viongozi tuliokuwa nao.
 
Kwanza natoa pole zangu kwa familia nzima ya Mzee Munanka kwa msiba huu. Naomba mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho yake.

Kadri ninavyosoma hii thread, ndivyo ninavyopata nguvu kuwaambia Watanzania na hasa wana JF, tumepotoka kwa kushindwa kuelewa mambo mengi kuhusu nchi yetu na hasa Azimio la Arusha.

Je Mzee Munanka aliacha kuwa kiongozi wa Serikali na uwakilishi wa Bunge lini?

Je alianza biashara zake lini?

Tunapomfananisha na Rostam na Lowassa, ina maana kuwa alifanya biashara akiwa kiongozi wa Serikali na Mbunge?

Kwa ueleo wangu wa Munanka, Mkono na wafanyabiashara wengine ambao walikuwa wanasiasa wakati wa kutafuta uhuru na baada ya uhuru, wengi wao walikimbilia kuachia Uongozi na Utawala kupitia Serikali na kuendeleza kufanya biashara zao kwa kuwa Azimio la Arusha, lilitamka waziwai kuwa Kiongozi asifanye biashara.

Ndiyo maana utakuta kuwa Wahindi na Waarabu wengi walishikilia biashara na kuneemeka kuwa matajiri, na hata wazawa hasa makabila kama ya Wachaga walibobea katika biashara na kuachana na kufanya kazi Serikalini.

Ni wao pekee ndio walilielewa Azimio la Arusha na kutumia mwanya wa kukosekana ushindani na kugandamizwa na viongozi na kujijengea himaya za kitajiri, kwa kufanya kazi na si dhuluma.

Azimio la Arusha limepewa taswira mbaya na viongozi wa Tanu/CCM na watendaji wa Serikali kutokana na sheria na ukali wa kuzuia Vionggozi wa umma kutumia nafasi zao kikazi kujitajirisha au kujiingiza katika shughuli za kibiashara na kutumia upendeleo kutokana na nyadhifa zao. Viongozi wengi wa TANU/CCM ambao walitaka kutumia njia fupi za Ki-Chifu na Kitemi kujitajirisha kwa kuwa walikuwa ni viongozi, Azimio la Arusha lilikuwa ni sumu kali iliyozuia maendeleo yao binafsi.

Hawa walishindwa kuamua kujitumikia au kulitumika Taifa. Walitaka vyote wawe viongozi wa nchi, chama na Serikali na wawe wafanyabiashara wakiwa viongozi.

Sababu ya Azimio la Zanzibar la 1992, ni kuondoa lile pingamizi kwa walio viongozi wa umma na uwakilishi kuwa wafanya biashara! Wlichofanya Zanzibar, ndicho kilichoruhusu Rostam na Karamagi wafanyabiashara kuwa Wabunge. Ndicho kilichowafanya kina Mramba, Mkapa, Lowassa, Kapuya na wengine wengi ambao ni viongozi wa Chama na Serikali kushikilia madaraka huku wakiwa ni wafanyabiashara wenye makampuni au hisa katika makampuni.

Huu ndio chimbuko la Ufisadi, kutumia madaraka ya umma kuendesha biashara.

Mnakumbuka, ili kuwa mbunge, kanuni ilikuwa ni lazima uwe mkulima au mfanyakazi. Ni wafanyabiashara wachache sana baada ya Azimio mpaka karibu mwaka 1992 ambao walidiriki kuwa Wabunge!

Inabidi tuache ushabiki na hisia hasi kuhusiana na Azimio la Arusha na tulisome upya kwa mkao usio na mfungo wa kulikataa.

Naomba mlisome Azimio la Arusha kama unasoma kwa mara ya kwanza na hujui "maafa" yake au yaliyosemwa kuwa ndio chimbuko la umasikini.

Nawasikia wote, Mzee FMES, Mkandara, Jasusi na pande mbili za mdahali huu na hasa suala la ufisadi.

Naomba mnijibu maswali yangu hapo juu kabla hatujaendelea kumtupia Marehemu matusi ya nguoni.


Ndiyo Mzee Munanka alikuwa ni mfanyabiashara aliyejitajirisha kwa kujua namna ya kufanya biashara na kutumia ujuzi wake wa kikazi tangu wakati wa mkoloni mpaka baada ya Uhuru. Swali mjiulize jee alitumia madaraka yake vibaya na kuwa mafanya biashara au aliamua kuachana na Siasa na kuwa mfanyabiashara?
 
Mwinyi,Mkapa,Ngombale,Malecela.....

Hapa mkuu unepotoka tena kwa makusudi mazima kwa sababu unajua tena vizuri sana kuwa Malecela, hatakiwi kuwepo kwenye hii list,

Ila kama kawaida yako kwa sababu tatizo lako ni Malecela, uameamua kuliweka kwa makusudi, this is low politics! Na haziwezi kumsaidia m-Tanzania kwa njia yoyote ile sema ukweli tu kwani utapungukiwa nini?

Kwa sababu hata ukisema uongo hutapewa free pass hapa, Malecela hakuwahi kuiba kama hao wengine, unless unauujua wizi wake uweke hapa mkuu huna sababu ya kuzunguka mbuyu!
 
FMES,Mkandara,hauxtable,Rev.Kishoka,

..nadhani tukubaliane kwamba ilifika mahali maisha yakawa mabaya and un-comfortable.

..ilifika mahali mishahara ikawa haikidhi mahitaji na modest life style ambayo watumishi wa serikali walitaka kuishi.

..ufisadi na rushwa umeanza na watu kujitafutia njia za ku-survive na wengine kupitiliza mpaka kuwa wahujumu na wahalifu kabisa.

..huko vijijini ndiyo usiseme, hali ilivyokuwa mbaya na ya kusikitisha.


Bhoke Munanka:

..kwanza Mwenyezi MUNGU amlaze pema peponi.

..sote tunakubaliana kwamba aliacha kazi ili kufanya biashara.

..lakini kuna deals fulani fulani ambazo watu wanadai alishiriki ambazo zinaweza kumpasisha kuingia daraja la mafisadi.

Malecela:

..binafsi sikubaliani na hoja ya Baba wa Taifa kwamba Malecela hafai ktk uongozi kutokana na kuyumba ktk kushughulikia hoja ya Tanganyika.

..tatizo lililojitokeza ni kwamba hata yeye Malecela hakujitetea baada ya kuandikwa na kuitwa majina na Mwalimu.
 
Mkuu Kishoka,

Heshima mbele bro, nitajibu tu kwa vile umenitaja jina, lakini otherwsie nilikuwa nimeshamaliza hii topic, yaani ya mimi kuchangia kuwa huyu marehemu alikuwa fisadi nambari moja na ndiye hasa mmoja wa chimbuko la ufisadi Tanzania, kwa sbabu bado mpaka sasa ninapoandika ninaamini hivyo tena kwa 100%,

Inabidi tuache ushabiki na hisia hasi kuhusiana na Azimio la Arusha na tulisome upya kwa mkao usio na mfungo wa kulikataa. Naomba mlisome Azimio la Arusha kama unasoma kwa mara ya kwanza na hujui "maafa" yake au yaliyosemwa kuwa ndio chimbuko la umasikini. Nawasikia wote, Mzee FMES, Mkandara, Jasusi na pande mbili za mdahali huu na hasa suala la ufisadi.
Naomba mnijibu maswali yangu hapo juu kabla hatujaendelea kumtupia Marehemu matusi ya nguoni.

Matusi ya nguoni? hapana sijamrushia mtu, ila nimesema madhambi yake ya uwizi wa mali za serikali, nafikiri kumtukana mtu ni one thing, na kutoa maovu yake ni another thing na ndio point yangu, unless kuna mtu mwingine aliyemtukana matusi ya nguoni, not me,

Kama ni Azimio La Arusha, kwa kweli sijui linahusiana nini na wizi wa huyu marehemu alioufanya kwa muda mrefu sana, tena baada ya kusema kuwa ame-retire, kwa sababu mpaka in th early 90s, mimi ninajua for a fct kuwa bado alikuwa na title nzito serikalini ya kuwa Mthibiti wa mali za serikali, the matter of fact kabla sijajua vizuri what I know now nilikuwa nikimu-admire sana kwa kazi yake hiyo, ambayo ilikuwa ikimsafirisha kila siku, unajua alikuwa jirani yangu kwa hiyo nilikuwa ninawasikia watoto wake jinsi mkuu anavyosaifiri na biashara zake, mpaka pale nilipokuja kujua ukweli wake kuwa ni fisadi, hasa kutokana na yaliyompata huyu Mzungu M-norway, ambaye alikua ameoa mama wa kibongo yaani the late Mama Kirunda, ambaye pia alikua mshikaji wangu sana,

Sasa huyu mzungu alipopewa masaa 24 ya kuondoka bongo, huyu mama alijaribu sana kutafuta msaada wa kumuokoa yule mzungu, ndio sasa nikazipata zile habari kwa ukaribu sana kuhusu yaliyomsibu kwa sababu pia yalikuwa yanamhusisha na huyu marehemu, kuhusiana na ununuzi wa meli za maziwani na wzi wake, sasa sijui kama this has anything to do na Azimio La Arusha, kama unavyosema?

Ndiyo Mzee Munanka alikuwa ni mfanyabiashara aliyejitajirisha kwa kujua namna ya kufanya biashara na kutumia ujuzi wake wa kikazi tangu wakati wa mkoloni mpaka baada ya Uhuru. Swali mjiulize jee alitumia madaraka yake vibaya na kuwa mafanya biashara au aliamua kuachana na Siasa na kuwa mfanyabiashara?

Labda sijakuelewa, eti huyu mzee alitumia ujuzi wake wa kikazi kujitajirisha wa kutoka wakati wa mkoloni mapaka wakati wa uhuru, that I am lost, kwa sababu sina uhakika kama ina anything to do na wizi wake unaofahamika sana ndani ya serikali ya kutuibia kwa siku zote kwenda nje na kununua vitu vibovu, ndege mbovu, treni mbovu, meli mbovu, magari mabovu, silaha mbovu, kila alichonunua hakikuwa na thamani sawa na ahadi yake kwa serikali yetu, na pia likingiwa kifua na Mwalimu, aliyekuwa rafiki yake sana,

Sasa sielewi kuwa kama haya ni matusi ya nguoni kama ulivyosema, au ni Azimio La Arusha, lakini ninarudia kuwa nimeweka ushahidi wakutosha wa ni kwa nini ninaamini kuwa huyu mzee alikwua fisadi namba moja, na bado ninaamini hivyo, kama ninajibu swali lako sina uhakika lakini nipo anytime mkuu, ila ya Azimio La Arusha na faidana hasara zake, hilo ni another serious subject ambayo sina nguvu leo katika hii topic, labda uifungulie topic yake mkuu!

Ahsante Sana Mkuu.
 
FMES,Mkandara,hauxtable,Rev.Kishoka,

..nadhani tukubaliane kwamba ilifika mahali maisha yakawa mabaya and un-comfortable.

..ilifika mahali mishahara ikawa haikidhi mahitaji na modest life style ambayo watumishi wa serikali walitaka kuishi.

..ufisadi na rushwa umeanza na watu kujitafutia njia za ku-survive na wengine kupitiliza mpaka kuwa wahujumu na wahalifu kabisa.

..huko vijijini ndiyo usiseme, hali ilivyokuwa mbaya na ya kusikitisha.


Bhoke Munanka:

..kwanza Mwenyezi MUNGU amlaze pema peponi.

..sote tunakubaliana kwamba aliacha kazi ili kufanya biashara.

..lakini kuna deals fulani fulani ambazo watu wanadai alishiriki ambazo zinaweza kumpasisha kuingia daraja la mafisadi.

Malecela:

..binafsi sikubaliani na hoja ya Baba wa Taifa kwamba Malecela hafai ktk uongozi kutokana na kuyumba ktk kushughulikia hoja ya Tanganyika.

..tatizo lililojitokeza ni kwamba hata yeye Malecela hakujitetea baada ya kuandikwa na kuitwa majina na Mwalimu.

Ohhh sasa tatizo lako ni kwa sababu Malecela hakujitetea? Haya sisi tunakuangalia tu mkuu tuone mwisho, yaani kazi kweli kweeeeeli! yaani mkuu you are all over the map duh! High class bwana!
 
Jokakuu,
Hizi habari za ajira na kipato kuwa chini mkuu ni UONGO uliopandikizwa na Mafisadi..
Ukweli ni kwamba toka Walimu, Madaktari na viongozi wote wenye professinal walipewa vitu muhimu regardless ya wapi wanapelekwa...
Nyumba za makazi yao zilikuwa bure, maji na umeme hawalipi, usafiri Bure, matibabu bure wengine hata wafanyakazi wa ndani walipewa kulingana na wadhifa ulokuwa nao...Huivi hawakuona kwamba wao ndio waliangusha uchumi wa nchi badala yake wanalalamikia mishahara hiyo leo!

Sasa twende kwa mahesabu ya kweli maanake mimi niwawahi kuwa mhasibu wizara ya habari kisha Mifugo ktk miaka ya mwisho ya 70 kuingia 80..tunazo kumbukumbu vichwani nimelipa sana mishahara kina Paul Sozigwa wamepanga sana msitari ofisini siku ya payday TGIF..makao makuu! haaa haaa haaa!

Nyumba leo hii inatozwa kitu kama 500,000 kwa mwezi tena wanalipa kwa mwaka (kima cha chini kabisa), tuache maji na Umeme nje. Usafiri huwezi kununua gari chini ya millioni 20 hivyo tufanye unalipa leasing 800, 000 kwa mwezi. Mshahara kwa viongozi wa kati miaka ya 82 ilifikia 2,020 kama kima cha chini kwa graduate wakati dollar moja ilikuwa haijafika hata 20 Tsh.. Piga mahesabu mkuu hawa watu waliokuwa wakidai kipato kidogo ni kina nani?..

500,000 ni equivalent to (450 Usd) + 800,000 ni (Usd 750) kisha weka ile dollar 120 ya mshahara wa Tsh elfu mbili na Upupu wake...
Kifupi graduate wa Tanzania alikuwa akipata Dollar 1500 kwa mwezi!..
Watu wengi wanatazama kile kiasi cha Tsh 2020 na kudai ni kidogo wakati mwajiriwa wa kawaida aliyemaliza high school aliajiriwa kwa mshahara wa Tsh 910. Hizi zilitosha kula kunywa na kufanya ufuska wote..Leo hawa viongozi wanataka kutuambia kitu gani?.
Mshahara wa chini enzi za Mwalimu ilikuwa Tsh 450 lakini dollar ilikuwa kwa chenji ya I Usd kwa Tsh 17 piga hesabu mwenyewe!
 
labda kwa kumkumbuka si vibaya maana TANU yawakati ule ilijali maslahi ya nnchi,na si chama cha mafisadi (CCM) cha wakati huu ambapo wanazingatia zaidi matumbo yao,kwa njia yao ya siri ianayoitwa kwa mkato,(SHI KWA MBI),Yaani Shiba Kwa Mbinu..!!!
 
Nimeuliza tena hizo Meli mnazozitaja hapa ni zipi?.. na UFISADI wake ulifanyika vipi kwani hazikuwa (used) zimetumika zilikuwa mpya na ziliunganishwa Kisumu, Kenya...Uzinduzi wa Meli ya MV Bukoba nilikuwa Mwanza nakumbuka vizuri sana, Mkuu FMES for record nisaidie mimi maanake hii mada imefika mbali sana siwezi kurudi nyuma kutafuta ulichosema kuhusiana na UFISADI wa meli nisizozifahamu...
 
Ndiyo maana kuna sehemu nimesema itabidi tu-revisit the meaning of the word fisadi.
Marehemu Munanka alikuwa mfanyibiashara kabla ya kuingia serikalini. Na alipoona inafaa arudie biashara zake, aliacha kazi serikalini akiwa kijana kabisa. Kama alikuwa na contracts za serikali hili halimfanyi fisadi kwa mtazamo wangu. Huwezi kumweka huyu leo kwenye kundi moja na akina Lowassa ambao hata hela yao ya kwanza ya kuagizia daladala waliibia serikali, au akina Chenge ambaye kila mkataba uliopita mezani kwake alikwapua $200k na biashara nyingine za madawa ya kulevya, au akina Rostum ambao wanaunda kampuni bandia na kwenda kuchota benki mamilioni ya pesa za walalahoi. Mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani. Kufanya biashara si kosa na natamani Munanka angekuwa mfano kwa viongozi wa sasa ambao wameng'ang'ania vyeo serikalini na huku wanaendesha biashara zisizo na vichwa au miguu.

Kaka hata Valabhia na wengine wote huwa na contract za serikali....

Hata Richamond ilkuwa contract na serikali.............

Hata Lowassa husema kuwa alitoka katika utajiri......

Hivi huyu si ndio Bhoke Munanka aliyekamatwa miaka ya karibuni akifanya deal la kifaa cha Nuclear.........I mean akikuwadia looting iliyokuwa ikiendelea DRC......

Nadhani kwa wale wanao umia na hili watafanya vizuri kama watawaambia jamaa zao wanaofanya ufisadi wajitahidi kuungama mbele ya watanzania kabla ya Mwenyezi mungu ajajitwalia......I mean hata kama ni wazazi wetu maana tukumbuke kuwa laana ya ufisadi haitaishia kwao tu, hata kwa vizazi vyao....

Tanzanianjema
 
Back
Top Bottom