Hivi wewe unadhani tumesahau kuhusu ile meli ilozama Ziwa Victoria kwa sababu ilikuwa ni meli maalumu kwaajiri ya mito lakini yeye Bhoke alikula fweza na kuruhusu inunuliwe na kutumika Ziwani??????
Watu kibao walikufa na yeye Bhoke hata hakuguswa, walioguswa ni wale walio ikagua meli mwaka mmoja nyuma na kuipa kibali cha kuendelea kufanya kazi.
Kama watoto wake wame na wana struggle kama watu wengine hiyo haiwezi kumzuia yeye kuwa Mtangulizi wa Mafisadi, ila inawaonyesha wazi mafisadi wa leo kwamba wanawachimbia mashimo ya Volkeno watoto wao. Fedha walizo iba zitakwisha wakiwa bado hai. Mungu awazishie maisha Mafisadi wote ili wapate kuuona uovu wao ukiwasambaratisha wao na vilembwe wao.
Kuupuuza ushauri wa kitaalamu kwa makusudi ili kujaza mifuko yao mapesa ni Mapungufu ya kibinadamu??
Give me a break!!
Madela-wa Madilu,
Facts, ndugu yangu, facts.
Ile meli haikuzama kwa sababu haikuwa lakeworthy. Meli ilizama kwa sababu ilipakia watu kupita kiasi. Kuna rafiki yangu aliikosa meli hiyo anasema ilipokuwa inaondoka Bukoba tayari ilikuwa imeshaanza kuelemea upande mmoja.