Shomari
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,112
- 241
Hivi unaandika ukiwa unazifahamu tabia za Wajeruman au unaandika tu? Hata walipoanza mambo ya Computer, Umeme, usafiri wa anga, majini na hata nchi kavu, kuna wengine waliita ni kazi ya shetani. Hata kutumia Internet tulisikia sana. TV nazo zililaniwa sana na kuna nchi kama Somalia hadi leo wanalani na wanalani hata Sambusa kuwa zinawakumbusha utatu mtakatifu (ila bunduki za Mzungu hazina shida hiyo).
Mkuu, hilo ni kama JIWE tu ila tofauti yake ni MAN MADE.
Bismark Stone, Mwanza.
Sijawahi kusikia Tanzania watu Wanachukia TV ama Internet, labda itakuwa ni kipindi ambacho sikuzaliwa, kwa Somalia sishangai wakikataza vitu hivyo sababu wao wamejiundia tamaduni na sheria zao ambazo ni tofauti kabisa na mataifa mengine yenye wafuasi wengi wa kikristo, sababu mfano katika nyingi wa nchi za kiarabu kwao kitu chochote kutoka Magharibi ni ni kibaya ama haramu. Halafu huwezi kulinganisha Jiwe la Bismack ambalo ni kazi ya mikono ya MUNGU ukalinganisha na hilo jimama ambalo watu walikaa wakakubaliana kwamba tuiweke sanamu hii ndani ya bahari. lakini hebu kaa ujiulize kwanini waliamua kutengeneza sanamu kubwa namna hiyo kwa nini wasingetengeneza ndogo?. sanamu kama hilo ukiambiwa gharama yake unaweza kukimbia lakini kwanini watu au mtu awekeze pesa yake kwa kitu kisichokuwa na maana? Baada ya kuiangalia pia niligundua kwamba sanamu hiyo si ya kiume bali ni ya kike. Lengo lao ni nini?