Benki ya Dunia imetoa mkopo wa dola 300m kwa sharti kwamba zaidi ya dola 15m zitumike kuendeleza waliopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo

Mzee wa Masauti

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
2,199
2,507
Benki ya Dunia imeridhia kutoa mkopo wa dola milioni 300 kwa Tanzania kuboresha sekta ya elimu. Moja ya masharti ni kuwa zaidi ya dola milioni 15 zitatumika katika programu mpya itakayoundwa kusaidia waliopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo. Jeuri ya masikini haidumu.

Kwanza pengine ni vema kuwafahamisha watawala wetu kwamba siamini kuwa kuna Mtanzania mwenye akili timamu anayetaka kuona Tanzania ikitengwa na jumuiya ya kimataifa au/na kunyimwa misaada.

Furaha ya baadhi ya Watanzania wanaposikia wafadhili wetu wanatishia kutunyima misaada ni MATOKEO (na si DALILI) ya tatizo kubwa zaidi: mzazi anayenyanyasa baadhi ya wanae kana kwamba hakuwazaa, siku akipatwa na janga inakuwa sherehe kwa hao wanaonyanyaswa.

Sio siri kuna section kubwa tu ya Watanzania wanaokuwa mistreated kana kwamba Utanzania wao ni kosa la jinai. Twawajua. Hawa wana kila sababu ya "kusherehekea majanga dhidi ya nchi yao."

Sio vema lakini ndio njia yao pekee. Ni wanyonge hawa, hawana pa kukimbilia wala pa kulalamikia. Siku ikitokea janga limewakumba watawala wetu basi inakuwa kama kilio cha wanyonge hao kimesikika.

La pili, sie ni masikini. Na tumekuwa hivyo tangu tupate uhuru. Hatujawahi kuwa nchi tajiri. In fact, moja ya "mapungufu" ya Baba wa Taifa yalikuwa "kufanya dili za siri" na nchi/taasisi wahisiani ilhali hadharani alikuwa anawaita kila jina baya (mabeberu, makabaila, mabwanyenye, nk). Bahati mbaya zama hizo mawasiliano kitaifa yalikuwa ya mwelekeo mmoja tu: kutoka kwa watawala kwenda kwa watawaliwa. Si Google wala Facebook iliyokuwepo enzi hizo.

Kwahiyo kwa vile sie ni masikini ni lazima tutegemee misaada. Lazima si kwa kutaka au kubweteka bali kulazimika. Sasa hizi porojo sijui za kuwaita wahisani majina mabaya ni uhuni na kudanganyana tu. Hatuwezi ku-survive bila wao.

Lakini sii sie masikini tu ambao twahitaji ushirikiano wa kimataifa. Hata nchi matajiri pia nazo zinahitaji ushirikiano na nchi nyingine, no wonder Marekani, Ujerumani, Uingereza, Japan na nchi nyingine tajiri duniani zina mahusiano wa kidiplomasia na masikini kama sie. Wao wanaweza ku-survive bila sie, ila sie hatuna jeuri hiyo.

Baada ya kukumbushana hilo, naomba kufahamisha kuwa fedha za mkopo wa Benki ya Dunia zina masharti yake. Kinyume na taarifa kuwa pesa hizo "zimetolewa tu," ukweli ni kwamba zimeambatana na masharti.

Na moja ya sharti muhimu ni kwamba zaidi ya dola milioni 15 katika mkopo huo wa dola milioni 300 zitatumika katika programu mpya ya kusaidia waliopata ujauzito mashuleni ili waweze kuendelea na masomo. Hii maana yake ni kwamba lile agizo la Jiwe kuwa kamwe mabinti waliopata ujauzito hawatorudi shuleni limekufa kifo cha asili.

Sasa badala ya kunyoosheana vidole kuwa "ah mnaoitakia mabaya nchi yetu mmeumbuka" au "hamna maana nyie, huku mwatuhadaa kuwa pesa mnazo, na kule mwajigamba kuwa mna jeuri dhidi ya mabeberu lakini mkipewa mkopo mnashangilia kama majuha," la muhimu ni kufanya jitihada za kuondoa siasa za mifarakano, kuimarisha udugu wetu, kukuza uzalendo na mwisho wa siku kila mtu kuwajibika katika nafasi yake.
 
Thanks Lord benki ya dunia inatupenda kuliko mtakatifu wetu, anaetumia misuli kwenye issues za kutumia ubongo, yaani hajui kuna wanao bakwa, wanaolaghaiwa wakiwa under-age, huyu katili tulioletewa safari hii ! namuombea sana Mungu ampende!
 
Thanks Lord benki ya dunia inatupenda kuliko mtakatifu wetu, anaetumia misuli kwenye issues za kutumia ubongo, yaani hajui kuna wanao bakwa, wanaolaghaiwa wakiwa under-age, huyu katili tulioletewa safari hii ! namuombea sana Mungu ampende!
We we we we,
Ampende zaidi yetu sio!?
 
Moja ya masharti ni kuwa zaidi ya dola milioni 15 zitatumika katika programu mpya itakayoundwa kusaidia waliopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo. Jeuri ya masikini haidumu.
 
Watoto wako na kizazi chako ndio wafanywe hivyo milele walahi
UHUNI UTAWASAIDIA NINI?
Crazy psychopath walahi
Mkuu achana na hilo jinga .usilijibu
Hata mimi limenikera muda si mrefu nilikua nimemjibu mtu fulani likadakia kuandika ushoga
 
Niliwaambia ni mapema mno kuanza kushangilia, rais anarudia kosa lile lile alilofanya alipokutana na Thornton mkiti wa Barrick hadi leo hatujapewa hata kishika uchumba tu cha $300m achilia mbali kodi ya trillion 425 tunayowadai.

Kwa lugha ya kidiplomasia ukisikia neno "agreed to review" au "agreed to work closely" usifikiri yamekwisha maana yake kajipange upya.
 
Benki ya Dunia imeridhia kutoa mkopo wa dola milioni 300 kwa Tanzania kuboresha sekta ya elimu. Moja ya masharti ni kuwa zaidi ya dola milioni 15 zitatumika katika programu mpya itakayoundwa kusaidia waliopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo. Jeuri ya masikini haidumu.
Mungu wabariki Wazungu
 
Tatizo mzee Meko aka Chakubanga anajifanya anajua yeye kila kitu..hata wenzake wameshaanza kumgeuka juzi Butiku katumwa amnyooshe kwenye suala la katiba..Meko hajiamini kwa sababu hajui ndio maana anatumia mabavu kutawala
 
Back
Top Bottom