Mkuu! Hivi nikikukopa fedha ili nifungue biashara siku ukija kuhitaji huduma kwenye hiyo biashara yangu(ambayo mtaji nilikopa kwako) napaswa kukuhudumia bure?au ni wewe ndiye unayepaswa kufuata vigezo na masharti ya biashara yangu?Hongera JPM watakuelewa tu.
Bank zilikuwa zinatumia fedha ya Serikali kuikopesha Serikali
Asante kwa kuliona hilo... tena ukipiga hesabu vizuri unaweza kuta marejesho yatakuwa makubwa zaidi ya awaliBank wana akili sana, hapo hamna kilichopunguzwa
Wangeacha muda ule ule ndio kungekuwa na nafuu... ila hiyo ni danganya toto cha ajabu hakuna wa kuelimisha hiliNakushukru kwa kuliona hilo, unapunguza riba unaongeza muda. Ni wenye uelewa tu watakaosimama.
Naona umekimbilia kutoa hongera wakati muda wa marejesho umeongezwa! Liccm katika ubora wake wa kushangilia kila kitu.Hongera JPM watakuelewa tu.
Bank zilikuwa zinatumia fedha ya Serikali kuikopesha Serikali
HUjapata shida.Uzembe tu... mtu msomi umesoma kabsa unaenda kopa eti unaacha atm card mwsho kudhalilishwa mtaani
.
Mkuu unajua operational cost za hizi benki ?HAKUNA KILICHOPUNGUZWA HAPO... NI UHUNI TU.. MIAKA IMEONGEZWA 8 TOKA 7.. NA RIBA WAMEPUNGUZA TO 17% KITU NI KILE KILE.. FANYA MATHS UTAONA AT THE END UNALIPA KILE KKILE AU ZAIDI. Riba bado kubwa mno mnoooo... mnoooooo... 17% kwa 8 yrs..? Banks zingeweza toa kwa 11% na kupata faida kubwa sbb 1: watapata wateja wengi sana 2: kama BOT wamewashushia banks riba hadi 8% na banks binafsi ikamkopesha mwananchi kwa 11% ana faida ya 3%... Hiyo 3% ni kubwa sana sanaaaa sbb wakishusha to 11% watapata wateja wengi sana na faida yao ya 3% itakuwa kubwaa ..
17% bado kubwa mnoo mnoooooo... Hakuna kitu hapo
Bank wanapata pesa kwa njia nyingi kuna makato mengi sana, ukiuliza salio wanachukua, ukiwithdraw wanakata, ukiomba risiti wanakata, kuna monthly charges n.kMkuu unajua operational cost za hizi benki ?
Kwa ufupi
By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
- Watumishi wa umma ambao awali walikuwa wanafanya marejesho mpaka miaka sita ambayo ni sawa na miezi 72, sasa wanaruhusiwa kufanya hivyo mpaka miezi 84.
Dar es Salaam. Benki ya CRDB imeongeza muda wa marejesho kutoka miezi 60 hadi 84 huku ikishusha riba kwa asilimia nne kwa wateja wake, hasa wafanyakazi.
Benki hiyo imeshusha riba kutoka asilimia 21 mpaka 17 huku muda wa marejesho ukitofautiana kati ya wafanyakazi wa sekta binafsi na watumishi wa umma.
Wateja wa benki hiyo wameanza kunufaika na punguzo hilo tangu wiki iliyopita pindi menejimenti iliporidhia kufanya mabadiliko hayo.
Akizungumza na Mcl Digital leo Mei 13, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk Charles Kimei amesema mabadiliko hayo yanalenga kumpa mteja unafuu wa kukamilisha malengo yake kwa wakati.
“Punguzo hili linatolewa kwenye matawi yetu yote. Tangu wiki iliyopita huduma hiyo imeanza kupatikana,” amesema Dk Kimei.
Watumishi wa umma ambao awali walikuwa wanafanya marejesho mpaka miaka sita ambayo ni sawa na miezi 72, sasa wanaruhusiwa kufanya hivyo mpaka miezi 84 au miaka saba wakati wafanyakazi wa sekta binafsi waliokuwa na miaka mitano wameongezewa mpaka miaka sita.
Hatua ya CRDB imekuja baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kushusha riba ya mikopo inayotoa kwa benki za biashara mara mbili mfululizo.
Machi mwaka jana, ilipunguza riba hiyo kwa asilimia nne kutoka asilimia 16 mpaka 12.
Mwaka mmoja baadaye, BOT ilipunguza tena kwa asilimia moja na kushusha kiwango cha akiba ambacho benki hizo zinatunza kwake kutoka asilimia 10 mpaka nane ili kuzipa uwezo zaidi wa kuikopesha sekta binafsi.