Benjamin William Mkapa nimjuaye...

Wapi rais wangu mstaafu mh benjamin mkapa? I wish ungeingia huku uone yanayoandikwa, I wish uone haya maovu yaliyofanyika enzi za utawala wako...yumkini ulidhani watanzania hawajui kumbe wanajua yotee...dhambi hii mtatubu wapi? anyway....heri ya mwaka mpya mh.
 
Last edited by a moderator:
ni raisi mstaafu wa tanzania ambaye atakufa na laana ya watanzania kama hato omba/kutubu dhambi zake akiwa hai

We koma kabisa,hakuna mTanzania atakae mlaani Mkapa.
Kama wanataka wamlani Mbowe kwanza kwa kuigeuza cdm saccos.
Nyambaaaff sana
 
Wapi rais wangu mstaafu mh benjamin mkapa? I wish ungeingia huku uone yanayoandikwa, I wish uone haya maovu yaliyofanyika enzi za utawala wako...yumkini ulidhani watanzania hawajui kumbe wanajua yotee...dhambi hii mtatubu wapi? anyway....heri ya mwaka mpya mh.

Mngekuwa na uwezo na akili za kutosha basi haya maneno mngemueleza Mbowe basi.

Lakini sababu hamuwezi, hiki mnachokieleza humu ni unafiki wa kiwango cha PhD.

Badilikeni Nyumbu nyie
 
Last edited by a moderator:
Rais bora wa TZ next to Mwl. J. Nyerere

Aliingia madarakani kwa haki bila rushwa wala kununua vyombo vya habari. Alikuwa na hoja na alieleza WAZI nia yake ya kugombea urais.

Alianza kazi kwa kasi hakungoja wiki mbili au zaidi kupanga baraza la mawaziri.

Aliunda serikali ndogo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Alikuwa na falsafa binafsi, dira na msomi aliyependa kusoma na kujifunza.

Akapambana kijemedari kwelikweli na misukosuko ya Reli, MV Bukoba, Elnino na majanga mengine. Akapunguza mfumuko wa bei toka 48% 1994 na kubakia single digit enzi zote za utawala wake.

Akaboresha utumishi wa umma; kapunguza wafanyakazi hewa na kuboresha maslahi.

Akapunguza deni la nje na kuipa Tanzania heshima.

Akajenga miundo mbinu hususan barabara kwa kasi kubwa

Akavutia wawekezaji wenye tija kama TBL, NBC n.k

Akajenga EPZ alipanga zijengwe 22 nchi nzima

Akaimarisha majeshi yetu kwa kuwapatia motisha vitendea kazi na makazi.

Akajenga Uwanja wa Taifa

Akajenga Benki kuu Twin towers na kule Zanzibar. Twin Towers kama Bank of Canada, Toronto (kwa wanaojua)

Alikuwa na hoja zenye mashiko.

Alikuwa kiongozi kweli jasiri, mwenye kujiamini na hakuogopa mihadhara: iwe ya vyama vya siasa, vyuo vikuu au kimataifa. Alikuwa full of substance.

Ujasiri wake hata vita ingetokea enzi zake angetuongoza vyema sana kumshinda adui.

Hakuwa mwongo katika kauli na ahadi zake.

Alikuwa na maadili na na hekima na aliheshimu mamlaka na taratibu zilizopo.

Akawapa nguvu na haki zaidi wanawake.

Alipigania utandawazi kuwanufaisha wengi.

Alikuwa mchapakazi hakuwa mvivu.

Alikuwa makini na alipinga na kukwepa sana matumizi yasiyo lazima ya serikali.

Alisafiri ngambo pale tu ilipobidi. Alikaa ofisini na kufanya kazi.

Alijiheshimu hakuwa Fataki.

Hakuwa ombaomba, bali alipenda kujenga uwezo, kujitegemea na kuwasaidia ombaomba.

Akanunua ndege bora ya Rais, mafisadi wakaipinga.

Akanunua rada ya nguvu, mafisadi wakaipinga.

Alikuwa na vyeti vya nguvu na alifuzu vyema masomo yake. Alionyesha uwezo. Alikuwa na speech za kisomi.

Alihakikisha nchi inakaribia kupaa ndio akaikabidhi kwa JK. Tukadhani itapaa.

Na mengine mengi.

Huyo ndiye Benjamin William Mkapa, Rais ninayemkubali na kumrank second. Angekuwepo mpaka leo Tanzania ingekuwa emerging economy I am sure.

Mnaomsema vibaya mshindwe ka kulegea. Hamna shukrani. Ni kiongozi ambaye wanaokumbuka, tunamshukuru sana.
Naunga Mkono hoja.
RIP BWM.
P
 
HV ndivyo inavyopaswa kumuongelea marhum umefanya vyema mtoa mada.
 
hureee ...well said ..magufuli for presidency 2010!!!... mnajuwa magufuli alikuwa kwa sumaye .na alikuwa awe waziri mkuu wa sumaye...ndio maana alifungwa kweli kweli ...akapewa wizara ya ardhi ambayo ...wanaiita wizara ya kifo...akafurukuta ..., wakaunda wizara maalum ya samaki ...ambayo haina public interest ...akafurukuta...hadi juzi jk imebidi amvulie kofia[jk knows ..if you cannot fight them ..join them...].......
Daaa
 
Kumbe mkuu tupo pamoja sio?

Ebana mi namkubali Magufuli sana, ila sitamani awe rais bali Waziri mkuu... Naamini kutakuwa na changes kubwa sana!

Hivi nyakati za 2005 Magufuli na Pinda walikuwa kambi ipi? Ya JK au ya Salim? Mkuu naamini wewe unaweza kunitoa tongotongo
Hivi kaka upo,amekuwa rais aise
 
Give me a break. Magufuli waziri mkuu!!! Hivi hatuna vipimo vya kujua ni nani anaweza kuwa kiongozi bora!? Wana-JF mnaanza kumshabikia mvunjaji sheria mkubwa Bw Magufuli, au kwa vile hamkujua aliyoyafanya kwenye mabarabara kuwavunjia watu nyumba bila ya kujali haki zao za msingi, tena kwa kukataa kuheshimu sheria ambayo ilikuwa wazi! Alishauriwa kuhusu haki za wananchi kule Kigoma na Shinyanga ambao barabara iliwafuata na sio wao waliingilia kingo za barabara, akakataa kata kata, matokeo wananchi wakavunjiwa bila fidia na Mungu anajua kilichowapata wale walala hoi. ALipojaribu kufanya hivyo hivyo kule Rombo, fisadi Mramba akazuia kwa nguvu zote, na wananchi wa Rombo walilipwa na wanaendelea kulipwa fidia. WAROMBO walikuwa na msemaji, hao wengine hawakuwa na msemaji. Tena hata pale Rombo Magufuli alilkuwa akifanya vikao vya kuwakemea wananchi licha ya Mbunge wao kutafasiri sheria na kuwahakikishia haki itatendeka. Huyu ukimpa madaraka makubwa si atajeuza sheria zote ziwe kwake.

Jamani mnasahau hata ile barabara aliyoilazimisha kule jimboni kwake, yaani kuifikia barabara ya lami ya Magufuli unapita kwenye mashimo makubwa mno....kiongozi anayevuta kamba kwake, jamani jamani halafu mje mlaani tena kama mnavyomlaani kijana mtanashati mwenye sura na akili za kuvutia JK......SIONI cha kumuenzi Mkapa kwani kama raisi alitimiza wajibu wake na tukamlipa na tunazidi kumlipa, lakini hilo la kuiba na mashemeji, wakwe na wattoto wake ni lazima alilipie
Aiseee nimekuelewa sana
 
Back
Top Bottom