Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Kila mmoja ana makosa yake na Mkapa ndiye mwanzilishi wa maovu tunayoyaona sasa. Wengine wameiga mkumbo kumbe ukiwa rais unatakiwa uwe mwizi n.k.

Makosa ya Mkapa hayamwondolei hatia yake ya ubadhilifu na mikataba mibaya kuwahi kujiri duniani.

Nina mashaka kama 2015 tutafika salama.
 
Pamoja na uchafu wake, namkumbuka Mkapa kwa uwezo wake wa kusimama na kukemea kitu kama mwanamume. Hawa wengine wanaokemea mambo huku wanakenua meno wananikera sana.
 
Isingekuwa Mkapa leo hii mngekuwa mnagombea ving'amuzi? wakati Mkapa anaingia madarakani maduka mangapi yalikuwa yanauza tv? kulikuwa na yadi ngapi za magari? hebu acheni kufuru jamani usile ugali wa mtu halafu ukainuka kumchoma mkuki mgongoni nchi ilikwisha na kubakia matobomatobo na pale hazina haukuwepo ht mshahara wa watumishi wa mwezi mmoja. Achaneni na Mkapa kabisa ongeleeni hao walioingia na kuanza kubugia mapochopocho aliyopika Mkapa na mjue wazi tungeendelea na Mkapa leo hii tungekuwa mbali sana tusingerudi nyuma mtapiga kelele hata mpishi kuonja mboga kama ina chumvi ama laa mtasema katafuna chakula cha wageni.
 
Ni kweli kabisa hata ndani ya familia baba akiwa dhaifu ni hatari sana mkapa alisimama kiukweli kama alikwiba basi alijua kula na vipofu kiliko haya eti hata lizimoja anajichukulia tu rasilimali za watanzania kweli tz imekua shamba la bibi wezi wakubwa wanyonyaji viongozi nyinyi hamuogopi hata mungu mnajilimbimizia mali huku umati wa watanzania ukiangamia kwa umasikini vifo elimu duni afya mbovu mtanzania mtumwa ndani ya nchi yake ananyanyaswa anateswa ole wenu enyi viongozi wa dunia msotoa hukumu ya khaki kwa mara ya kwanza naichukia ccm kwa mara ya kwanza namchukia baba mkubwa huyu nilizani tabasam lile ni huruma na upendo kumbe anatumaliza huku anatuchekea nawe mama cholo msaidizi gani usiyemwambia mume hili hapana unakose mpz ktk hali ya mahaba i hate you
 
Pamoja na uchafu wake, namkumbuka Mkapa kwa uwezo wake wa kusimama na kukemea kitu kama mwanamume. Hawa wengine wanaokemea mambo huku wanakenua meno wananikera sana.

kila nikisikia jina la mkapa huwa nakumbuka alivyomsaliti mwalimu mwenzagu na watanzania kwa ujumla.mwalimu nyerere lala salama, siku akipita huko huyu mnafiki mkukung'ute viboko kumi na viwili kavu! sita vya kumpokea na sita vya kumsindikiza jehanamu akamuonyeshe baba yake shetani
 
Asiye kuwa na kosa aanze kumtupia jiwe,mi nikifanya tathimini huyu jamaa namkubali sana na rafiki zangu wakenya wana sema Ben angekuja baada ya Nyerere tungekuwa mbali sana.Jamani fedha yetu inavyoporomoka thamani kila kukicha kuna aja ya kumkumbuka.Hili weza kuweka mlinganisho wa uchumi ukifanya kazi unaishi vizuri na mshahara wako hali kadhalika ukifanya biashara unaishi vizuri na biashara yako.
 
watu wengine sijui mtajitambua lini? yaani hata kujua ngedere na tumbiri ni mtu na mpwa wake hamjui? ndo maana wenzako kule wanamsikitikia yule jambazi!
 
Pamoja na mapungufu yake ila namkumbuka kwa kuwa mtu wa NDIMI moja, akisema ni mwisho na sio kukimbia matatizo kwa kutafuta safari
 
Akumbukwe kwa nini naye huyo? Kuna tofauti gani ya maisha baina ya utawala wake na ule wa Mwinyi na Kikwete? Rumba bado ni kali tu na Tanzania hatujawahi kuwa na ahueni ya maisha hata siku moja. Na hapo wala sijagusia mambo mengine….

Hujawaelewa hawa wanaomkumbuka na mtoa Thread.

Ana maana kwamba wanamtandao wameziba ulaji wao na umehamishiwa kwa wengine. Hii haina maana kuwa wakati ule watanzania walikuwa na maisha bora bali anamaanisha kikundi chao. Namnukuu anaposema yafuatayo yanayothibitisha niyasemayo:
".......na wanaonufaika ni wachache waliokuwa vinara wa hilo genge." Jiulize ni genge lipi ndilo linauhalali wa kufaidika, jibu ni rahisi kwa muujibu wake ni kundi lile la Mkapa.

Haya watanzania ndio watoaji wa hukumu.
 
Isingekuwa Mkapa leo hii mngekuwa mnagombea ving'amuzi? wakati Mkapa anaingia madarakani maduka mangapi yalikuwa yanauza tv? kulikuwa na yadi ngapi za magari? hebu acheni kufuru jamani usile ugali wa mtu halafu ukainuka kumchoma mkuki mgongoni nchi ilikwisha na kubakia matobomatobo na pale hazina haukuwepo ht mshahara wa watumishi wa mwezi mmoja. Achaneni na Mkapa kabisa ongeleeni hao walioingia na kuanza kubugia mapochopocho aliyopika Mkapa na mjue wazi tungeendelea na Mkapa leo hii tungekuwa mbali sana tusingerudi nyuma mtapiga kelele hata mpishi kuonja mboga kama ina chumvi ama laa mtasema katafuna chakula cha wageni.

aisee babangu zile nyumba za masaki na osterbay na mikocheni na chang'ombe ziliuzwa bei ya mbege
 
Economically the guy was ok you can't compare with the present one is believing on loans to from up country this is strange presider
 
Economically the guy was ok you can't compare with the present one is believing on loans to from up country this is strange presider

Ni kweli ben aliimarisha uchumi lakini ndiye huyo huyo aliyetafuna hovyo na kujiuzia mali za umma. Ni ben aliyezaa serikali yenye kuita watz kuwa ni wavivu wa kufikiria. Ndiye aliyesababisha watumishi wa umma wawe miungu watu. Matendo ya serikali ya ben kama nyerere angerudi duniani kwa jinsi alivyomtetea angeweza kufa tena siku hiyo.
 
Mimi namkumbuka kwa yafuatayo;

1. Kuuza NBC kwa bei ya kutupa kwa makaburu
2. Kupora mgodi wa Kiwira
3. Mauaji ya wapemba
4. Kifo cha Mwalimu Nyerere
5. Vifo vya watanzania kwenye ajali za MV Bukoba na Ajali ya Treni Dodoma
6. NET Group Problem
7. Kukimbia asili yake na kwenda kuweka makazi Lushoto - jasiri haachi asili
8. Baba wa Taifa wa ufisadi wote nchi hii

Nina mengi ya kumkumbuka Mkapa hayo machache tu, kweli ninamkumbuka nadhani ametuachia urithi mzuri wa ufisadi
 
Baada ya vyombo vya
habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa
habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa
Watanzania tutamkumbuka.

Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu,
tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni
wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika
2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT
itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina
thamani tena. Ukishachenji imeisha.

Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu
sana.

Kila la kheri.....

kwa kuwa alifanya ya msing na mazur kweli tutamkumbuka na tunamkumbuka
 
Back
Top Bottom