Tafadhali wadau naomba mnielimishe. Nilikuwa mwajiriwa wa benki moja nchini for about 4 years, na sasa nimeacha kazi ( resigned). Sasa swali langu ni benefits zipi ninazotakiwa kulipwa na mwajiri na ppf?
Hii inategemeana na content za mkataba wako.ERLA yetu inasema ukiacha kazi kwa kutoa notice ya muda husika ( mara nyingi huwa ni mwezi mmoja) au twenty four hrs ambapo wewe ndo unatakiwa kuilipa hiyo benk husika.
Baada ya kufanya hivyo kama ulikuwa hujaenda likizo utalipwa na sevelance allowance ya mshahara wa siku saba kwa muda miaka yote uliyokuwa na benki.
Sorry mie ningependa kujua NSSF benefits wanakulipaje? Kwa awamu? au zote kama PPF? (maana hawa nimeishawahi kulipwa nao)
Na kama ni kwa awamu ni kwa viwango au kwa muda maalumu?
Ha!ha! naona kijana upo uwanja wa nyumbani hapo.....!!
Umeacha kazi kwa matakwa yako mwenyewe yaani "resignation" kwa mwezi mmoja unapata final benifit zako ambazo ni mshahara wa mwezi mmoja,siku zako zote za likizo ulizo limbikiza,malipo ya kukusafirisha mpaka walipo kutoa "Point of hire" na sio point of recruitment "Sehemu ulipo ajiriwa".Kama ni wewe na familia yako au wewe peke yako na mizigo yako.
NSSF and PPF.
Hawa wanatakiwa kutoa pesa yote ya michango yako uliyo changa kwa muda wote uliofanya kazi na sio kwa mafungu....kukupa kwa mafungu ni ufisadi wa aina yake..wanataka uanze kubembeleza kama vile waomba mkopo.
Juzi office za mwanza...kuna mtu katoka na malalamiko ya kucheleweshewa malipo yake na hata baada kupewa check ilikuwa na kiwango nusu....na katika sheria mpya sijui mwaka gani...inawapa kitu kama huruma wafanyakazi wa sector za madini kwa kushughulikia NSSF/PPF zao kwa muda wa siku 21 au mwezi mmoja..