Bendera za CCM zazua kizaazaa kenye Daladala Arusha

Aisee huwezi amini, juzi ccm walikuwa na mkutano wa kampeni pale mwananyamala mwinjuma, basi baada ya kampeni dala dala zilikuwa zinakataa kuwapakia watu wenye yunifomu za chama cha mafisadi
walikuwa radhi kuondoka tupu
 



Ingawa sipo huko A town ila nilisikia kwa mdau mmoja kuwa bendera nyingi za chadema zimemwagwa bure huku CCM wakizitoa kwa kuwapa hela wananchi,

mie napenda kusemaCCM khaaa huo s sidhani ni kweli watu hawapandi hizo daladala ati kwakuwa zina bendera ya CCM haiwezekani kabisa wandugu yaani mie niko kituoni niache kuwahi mjini kwakuwa daladala ina bendera ya asa uta kuwa ulimbukeni,

kwa upande wa pili hili liko wazi kuwa watu wanaonekana wamekichoka CCM ila sasa je wamejiandikisha kupiga kura au nao ndio walewale wa lile tangazo ulipiga kuraaa???? khaaa mei niache kuingiza siku nika pige kura????

wananchi wamekosa elimu ya urai esp upigaji wa kura wananchi hawaju kabisa haki zao ni wanaongea tuu huko uswahilini.


Kama wewe huwezi wengine wanaweza, usisemee nafsi za watu wengine, hata mimi gari ikitundika bendera ya mafisadi sipandi. Usiwe mwoga wa mabadiliko, uwoga na ujinga wa watz ndiyo mtaji wa CCM kuendelea kubaki madarakani, hivi sasa watu wengi wamevaa ujasiri na werevu ndiyo maana unaona watu wanaacha mizinga wanakuja kutisha wapiga kura
 
Leo nilipakia kidaladala, baada ya muda nilisikia driver akizungumza na mwenzake ndanii ya gari kuwa leo nilimtumrudishia tajiri yangu funguo za gari kwa sababu alifngia bendera ya ccm kwenye gari analoliendesha na alipomwambia tajiri yake aiondoe hiyo bendera, tajiri akamjibu gari ni lake na anauwezo wa kufanya chochote kwenye gari lake. Ndipo huyo dereva akamrudishia fungua ni kumwambia kuwa hawezi kuendesha gari lenye bendera ya ccm kwani abiria wengi kwa sasa hawapakii magari yanye bendera ya ccm, kwani wameichukia sana.

Nilipojaribu kufuatilia zaidi mazungumzo ya abiria wengine, niligudua kuwa wengi wanakerwa na tabia ya watu kubandika/kufunga bendera za ccm kwenye magari na baadhi yao walidai kuwa hapandi kabisa magari yenye bendera hiyo.

Tunataka wananchi waonyeshe hii hasira kwenye boksi la kura!!! Hawa jamaa hata wakichakachua, matokeo yatawaumbua tu...!!!
 
afu unakuta lijitu bado limeng'ang'ania thithiemu thithiemu thithiemuuu....aarghhhh!
 
Hebu acheni uzushi. mnazungumzia Arusha ipi nyinyi mandondocha wa mbowe na Lema wake? mimi nipo hapa Arusha na sijawahi ona huu ujinga mnaoongelea hape. BIG UGORO kuanzia waleta maada mpaka wachangiaji.
 



Ingawa sipo huko A town ila nilisikia kwa mdau mmoja kuwa bendera nyingi za chadema zimemwagwa bure huku CCM wakizitoa kwa kuwapa hela wananchi,

mie napenda kusema sidhani ni kweli watu hawapandi hizo daladala ati kwakuwa zina bendera ya CCM haiwezekani kabisa wandugu yaani mie niko kituoni niache kuwahi mjini kwakuwa daladala ina bendera ya CCM khaaa huo sasa uta kuwa ulimbukeni,

kwa upande wa pili hili liko wazi kuwa watu wanaonekana wamekichoka CCM ila sasa je wamejiandikisha kupiga kura au nao ndio walewale wa lile tangazo ulipiga kuraaa???? khaaa mei niache kuingiza siku nika pige kura????

wananchi wamekosa elimu ya urai esp upigaji wa kura wananchi hawaju kabisa haki zao ni wanaongea tuu huko uswahilini.



Mimi nisingepanda gari lenye bendera ya CCM kwani itakuwa ni kuunga mkono au kubariki ufisad. Tusidanganyike!
 
Juzi nimetoka Mbeya nimepanda gari ya sumry kuna dereva alivaa kofia ya ccm alipoulizwa kwanini amevaaa kofia ya ccm na wakati hakuna walichofanya akadai yeye hajavaa kwa sababu ya ccm ila nimshabiki wa yanga na ile kofia inarangi za Yanga
 
Si kwamba kupeperusha bendera ya ccm ni kuipenda ccm.
Kama kiford chako Bima imekwisha, peperusha bendera ya ccm na hukamatwi.
Bendera ya ccm hutumika pale mtu anapotaka kuvunja sheria kwa sababu hataguswa,hiyo ndo nguvu ya bendera ya ccm!
 
Wananchi wana busara kuliko tunavyodhani. Wamepiga mahesabau wakaona sasa tumetawaliwa na watu wale wale wasioweza kwa miaka 50 na hali halisi ni kama hivi:

  1. Umeme shida. Ndio maana hata viwanda inakuwa shida kuvianzisha.
  2. Maji shida. Hata maji jamani?
  3. Barabara shida. Wenzetu Kenya wanajenga barabara za lane 12 sisi ahadi tupu za kila siku.
  4. Elimu ndio usiseme. Ni sifuri kabisa. Na bila Elimu hakuna maendeleo.
  5. Vingozi mabwanyeye wa kupindukia. Ila hawana huruma hata kidogo. Wanathubutu kujenga nyumba mpya za kuishi wao za mabilioni (eg BOT Governor) wakati nyumba zenyewe wanazo tayari. Ona Sita anakataa nyumba ya Spika anapangisha ya walalahoi kulipa milioni 9 kwa mwezi!
  6. Usanii kila mahali. Taifa haliwezi hata kukusanya uchafu wake. Uongozi mbovu usioweza hata kutayarisha timu ya taifa ya soka au ya ridhaa.
Sasa wananchi wanajua fika kama tukiendelea na watu walewale, hali itakuwa ile ile. Wameamua kubadilisha chama tawala, kwa mara ya kwanza katika historia yetu. Tuna heri sisi ambao tumejaliwa kuona haya!
 
nikiona mabango na bendera za ccm napata uchungu sana,najikuta automatically nayakumbuka machungu ya ufisadi waliotufanyia, Atown HATUDANGANYIKI,lema ndio mbunge,buriani tupa kule,SLAA NDIO MPANGO MZIMA.jk MZUSHI.MREMBO,ANACHEKEA MAFISADI,HAFAI.
 
Kweli, hata mimi leo nilikuwa A town, binafsi sifurahii kupanda hiace yenye bendera ya ccm, nilikuwa naagalia kabla ya kupanda kwa sababu magari yako mengi, hivyo nina uhuru wa kuchagua.
Nahisi ni kweli bendera yaweza kuwa sababu ya kupata abiria wengi, kwani kuna hiace mmoja ilikuwa na bendera mbili, labda alitaka abiria wa vyama vyote viwili.
Ukiona hivyo ujue mwenye gari CCM na Dereva CHADEMA
 
Nilishuhudia konda akipewa tsh 5000 atoe bendera ya chadema aweke ya ccm maeneo ya sakina darajan,alipofika kituo cha kwa iddi akaitoa ile ya ccm akairudisha ya chadema,then nikamsikia konda akisema huku akiiweka ile bendera ya ccm kwenye dash board ya gari huku kukiwa na bendera zingine kama 5 hivi 'arifu,siwezi toa kura yangu kwa ccm labda nife leo,hawa jamaa hawatufai kutuongaza yani buku 5 niuze utu wangu!nikaamini kweli ccm wamechokwa hapa A town.
 
Hebu acheni uzushi. mnazungumzia Arusha ipi nyinyi mandondocha wa mbowe na Lema wake? mimi nipo hapa Arusha na sijawahi ona huu ujinga mnaoongelea hape. BIG UGORO kuanzia waleta maada mpaka wachangiaji.



Unanishangaza eti wewe haupo kwenye hilo kundi la wachangiaji, ulichokifanya nini kamasiyo kuchangia?

Jaribu kiungia kwenye Daladala, alafu ulete habari za kuisifia CCM, jibu utakalolipata ulilete hapa jamvini.
 
Man..... Ni kweli hapo A-city CCM wapo taabani. Tunasubiri kuwazika hapo oktoba 31
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom