S V Surovikin
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 13,653
- 32,890
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema kwamba wanapaswa kuandaa jeshi kwa ajili ya vita kwa sababu ya hatari zilizoelekezwa kwa nchi yake kutoka Magharibi,
"Lazima tufunge mipaka na Magharibi, haswa Poland na Lithuania." alisema.
Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Wanawake uliofanyika Minsk-Arena, Aleksandr Lukashenko amefanya tathmini juu ya maandamano dhidi ya uchaguzi wa Rais na shinikizo dhidi yao kutoka nchi jirani.
Akielezea kwamba baada ya uchaguzi, waandamanaji na uungwaji mkono wa kigeni walitumia kila aina ya mbinu ili kuleta machafuko nchini, lakini hawakufanikiwa, Lukashenko amesisitiza kuwa sasa shinikizo la kiuchumi na kidiplomasia kutoka nje limeanza.
Akikumbushia kwamba nchi jirani hazitambui matokeo ya uchaguzi nchini Belarus, Lukashenko amebainisha kuwa kilichofanywa Venezuela kinafanywa nchini mwake.
Lukashenko amedai kuwa uingiliaji wa nje dhidi ya Belarus unakuja kutoka Poland, Lithuania na Ukraine.
Lukashenko, ambaye pia amekosoa uamuzi uliochukuliwa na Bunge la Ulaya kwa kutotambua matokeo ya uchaguzi wa Rais nchini Belarus, amesema,
"Tulifanya uchaguzi katika nchi yetu kulingana na Katiba na Sheria. Hatuhitaji wewe kutambua uchaguzi. Uchaguzi ulifanywa kisheria."
Akisisitiza kuwa wale wanaoiingilia Belarus kutoka nje hawajui nini kinaweza kufanyika katika kipindi kijacho, Lukashenko ameendelea kwa kusema:
"Kabla hatujaanzisha vita, tunajua kwamba wana mbinu chache sana zilizobaki. Kwa hivyo tunapaswa kuandaa nusu ya jeshi kuwa tayari kwa vita. Tunapaswa kufunga mipaka na Magharibi, haswa Poland na Lithuania. Kwa huzuni kubwa, lazima tuimarishe usalama wa mipaka na ndugu zetu wa Ukraine. inatubidi. "
Akisisitiza kuwa anapinga vita , Lukashenko, amenukuliwa,
"Tunakaribia janga baya sana. Ikiwa wao (Ulaya) watakuja hapa itabidi tuwajibu. Hatutapiga magoti hata tukibaki peke yetu."
Baada ya Rais wa sasa Aleksandr Lukashenko kushinda uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 9 Agosti huko Belarus, maandamano yalianza na madai kwamba uchaguzi ulichakachuliwa.