MpiganajiNambaMoja
Member
- Sep 20, 2007
- 69
- 2
Jamani swala la bei za nyumba za kupangisha inabidi liangaliwe upya. Ingawa najua ni mambo ya soko huria lakini sasa kwenye nyumba imekuwa soko holela. Nimepata simu kutoka kwa mwenye nyumba ananiambia kuanzia January kodi ni 200,000 kutoka 110,000 ambayo nilikuwa nalipa kwa mwaka huu na mwaka uliopita nilikuwa nalipa 100,000. Hii ni nyumba ambayo ina vyumba 3 na sebure na jiko, haina maji, sewage system, na haina car parking ingawa kuna kiukuta mshenzi. Ni nyumba iliyoko kinondoni uswahilini pembeni ya barabara kubwa kidogo ambayo noise level ni 100% huku vumbi ni mtindo mmoja.
Nikampigia rafiki yangu anayekaa sinza kwenye nyumba kama hii yangu maana hazitofautiani sana, akaniambia yeye amepandishiwa hadi 400,000 kutoka 250,000.
Swali langu ni kwamba hawa wenye nyumba wanatumia vigezo gani kupandisha bei za nyumba zao? Nini kifanyike maana hali hii kwa kweli hatutafika.